Mwanamke Aliyeva miwani ya kusomea Wakati wa akiremba kitu.
Moduli

Miwani ya kusomea

Moduli hii inafundisha namna ya kugawa miwani ya kusomea ya kawaida

3 Masomo

Maelezo ya moduli

Moduli hii inafundisha namna ya kugawa miwani ya kusomea.

Kiwango cha ugumu: Rahisi

Muda wa moduli: Saa moja mkondoni, ikifuatiwa na mazoezi yaliyosimamiwa kama inahitajika

Kabla ya kuanza kusoma moduli hii, hakikisha kuwa umekamilisha moduli zifuatazo:

Tafsiri inaendelea

Moduli hii kwa sasa inahaririwa. Maudhui hayawezi kuwa sahihi katika lugha yako.

Kumbuka: Hatua ya kwanza katika kutathmini ikiwa mtumiaji anaweza kuhitaji miwani ya kusomea; ni kukamilisha kipimo cha uoni cha TAP (au kipimo cha uoni kinachofanana nacho). Namna ya uchunguzi huu hii imeelezewa vyema katika moduli ya vifaa saidizi vya uoni ya TAP.

Kwa kutumia kipimo cha uoni cha TAP unaweza kutambua kama mtu ana tatizo la uoni:

  • Anahitaji kupewa Rufaa kwenda kumuona mtaalamu wa afya ya macho au daktari wa tiba ya macho
  • Anaweza kufaidika na miwani ya kusomea (haijazungumziwa kwenye TAP)
  • Anaweza kufaidika na Vifaa saidizi vya uoni ambavyo vinaweza kugawiwa katika ngazi ya jamii (kama vile miwani ya kusomea\)

Rasilimali ambazo utahitaji

  • Miwani ya kusomea yenye Uwezo kuanzia +1 hadi +3
  • Vifaa na vipuri kwa ajili ya matengenezo ya msingi na marekebisho ya miwani ya kusomea
    • Misumari midogo (nati) ambayo inafanana na misumari iliyoko kwenye miwani ya kusomea ambayo umeigawa
    • Kioo kuza(kinachosaidia kuona misumari midogo)
    • Vipuri kwa ajili ya miwani ya kusomea ambayo unameigawa kwa mgonjwa ikiwemo misumari na sehemu za kingo za miwani

Bonyeza kwenye linki hapa chini ili kupakua na kuchapa maneno yafuatayo:

Jukwaa la majadiliano

Uliza maswali na tumia jukwaa hili kujadiliana kuhusu moduli hii na kubadilishana uzoefu na wenzio.