Mhudumu wa afya akikagua kiatu tiba.
Moduli

Viatu tiba

Kuna aina nyingi tofauti za Viatu tiba . Moduli hii inazingatia Viatu tiba na baadhi ya huduma za kawaida.

Masomo 5

Maelezo ya moduli

Moduli hii inafundisha namna ya kugawa Viatu tiba kwa wahitaji kwa kufuata hatua Nne za utoaji huduma.

Kiwango cha ugumu: Wastani

Muda wa moduli: masaa 2 mtandaoni, yakifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa na mwezeshaji kama itahitajika

Kabla ya kuanza, angalia kwamba umekamilisha moduli zifuatazo:

Rasilimali ambazo utahitaji

Upatikanaji wa baadhi ya aina za Viatu tiba vilivyoelezewa kwenye moduli hii kwa ajili ya kufanya mazoezi:

  • Kiatu tiba kilichofunikwa kote
  • Viatu tiba ambavyo viko wazi kwenye sehemu ya vidole
  • Kiatu tiba ambacho sehemu ya kisigino iko wazi.

Utahitaji pia:

  • Vipande vikubwa vya karatasi (ukubwa wa miguu)
  • Kalamu ya wino mzito.

Bonyeza kwenye linki iliyo hapa chini ili kuweza kupakua na kuchapa:

Jukwaa la majadiliano

Uliza maswali na tumia jukwaa hili kujadiliana kuhusu moduli hii na kubadilishana uzoefu na wenzio.