Nyumbani

Mafunzo katika utoaji salama wa vifaa saidizi 

Vifaa saidizi kama vile magongo, Vifaa saidizi vya kusikia, miwani ya kusomea na viti saidizi vya msalani ni vitu muhimu kwa watu wengi. Moduli hizi za mtandaoni zinalenga kuwasaidia wafanyakazi wa ngazi ya jamii wanaofanya kazi katika muktadha wowote, kufanya kazi kwa usalama na ufanisi katika kugawa vifaa saidizi mbalimbali.

Namna ya kutumia tovuti ya TAP

Anza kusoma moduli kwa kufuata hatua 4 rahisi:

1. Tazama video

Tazama video hizi ili ujifunze namna ya kutumia TAP.

2. Jisajili

3. Ingia

Ingia kwenye tovuti kwa kutumia maelezo binafsi ya kuingia.

4. Anza kujifunza

Anza kujifunza mwenyewe kuhusu Utambulisho wa moduli ya vifaa saidizi.

"TAP ni muhimu sana... sasa tunaweza kufanya kipimo na kugawa miwani ya kusomea, na kupunguza muda wa kusubiri kwenye kliniki ya wataalamu wa macho. "

Elsie

Meneja Muuguzi, Papua New Guinea

"TAP inakusaidia kufanya utafiti wa matatizo tofauti wakati mgonjwa anapokuteWakati waa. Inakupa ujuzi wa kupata ufumbuzi mpya. Mgonjwa wangu alikuja kwa shida ya kutembea na pia niliweza kumsaidia kwenye Uoni wake."

Pysha

Muuguzi, India

"Kwa uzoefu wangu ilikuwa muhimu sana kuwa na watoa huduma za afya karibu na nyumba yangu, ambao wanafuatilia kifaa saidizi changu kwa karibu."

Giovanni

Mtumiaji wa huduma, Uswisi

"Maigizo Yanatusaidia Kujiandaa kwa tathmini na watumiaji halisi wa vifaa saidizi. Ilitupa ujasiri katika ujuzi tuliojifunza kupitia moduli. "

Darsh

Mtoa huduma ya Afya katika Jamii, India

Namna ya kutumia alama za TAP imetengenezwa na Freepik leseni kutoka Flaticon.