Teknolojia saidizi
Pata maarifa juu ya teknolojia saidizi na namna bora ya kugawa bidhaa saidizi kwa wahitaji.
22 Moduli
Watu bilioni 2.5 wanahitaji bidhaa saidizi
Katika baadhi ya nchi ni 3% tu ya watu wanaoweza kufikia bidhaa muhimu saidizi kama vile vifaa saidizi vya usikivu, vijiti na miwani ya kuona karibu. Bidhaa nyingi saidizi zinaweza kutolewa katika ngazi ya huduma ya msingi. Kutoa bidhaa saidizi Kunaweza kuzuia Matatizo ya kiafya na kuongeza uhuru kwa watu wanaohitaji.
Kozi
Kozi ya teknolojia saidizi ya TAP inafundisha jinsi ya kutambua, kutoa rufaa na kutoa anuwai ya bidhaa saidizi. Ili kutoa bidhaa saidizi kwa usalama na kwa ufanisi kuna hatua nne:
Chagua
Bidhaa inayomfaa mtu zaidi.
Tafuta kipimo sahihi
Rekebisha na upate kipimo sahihi cha bidhaa kulingana na mhitaji.
Matumizi
Mfundishe mtu jinsi ya kutumia na kutunza bidhaa.
Ufuatiliaji
Kagua mahitaji ya mtu, tunza na urekebishe bidhaa.
Moduli
Kozi ya teknolojia saidizi ya TAP inajumuisha Moduli za utambuzi, Mawasiliano, kuona, Usikivu, kujitunza, uhamaji na dharura. Kila moja ya hizi zina Moduli ya utangulizi na Moduli maalum za bidhaa.
Je, umehusika katika utayarishaji wa mafunzo?
Ikiwa wewe ni sehemu ya kozi iliyopangwa ya mafunzo, unaweza kuombwa ukamilishe uandikishaji wa kozi au upimaji wa maoni. Tafuta utafiti unaofaa kwa nchi yako .
Kozi zaidi
Gundua kozi zetu mbalimbali shirikishi
Jinsi ya kuanza kujifunza
Kuanza kusoma ni rahisi. Jiandikishe, ingia kwenye akaunti yako, na uanze kujifunza.
Jifunze mtandaoni
Gundua kozi mbalimbali zinazokidhi malengo yako binafsi na ya kitaaluma.
Angalia koziWasiliana Nasi
Iwapo ungependa kujua zaidi kuhusu kazi ya WHO kwenye teknolojia saidizi, tembelea tovuti ya teknolojia saidizi ya WHO , jiunge na jumuiya ya GATE na ufuate timu kwenye LinkedIn !