Dalili za matatizo ya afya ya sikio
Matatizo ya afya ya masikio
Katika Upimaji wa hisia za kusikia na kuona, ni muhimu kuangalia:
- Sehemu ya nje ya sikio
- Sehemu ya kati ya sikio
Sehemu ya ndani ya sikio haichunguzwi wakati wa upimaji.
Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kukagua afya ya masikio katika Somo la nne .
Swali
Je, dalili zipi zitaonyesha kuwa mtoto ana tatizo la afya ya sikio?
- Maumivu katika sikio
- Uvimbe
- Mabadiliko ya rangi (sehemu yoyote ya sikio)
- Kutokwa na uchafu (damu, usaha, maji)
- Sikio lililoziba (nnta ya sikio au kitu kutoka nje ya mwili)
- Uharibifu/jeraha.
Maelekezo
Soma vizuri kazi zinazohusika ili kujifunza zaidi kuhusu dalili za tatizo la afya la sikio.
Dalili za matatizo ya afya ya sikio kwa nje
Kazi
Tazama picha za masikio hapa chini na uchague ni masikio gani yanaonekana kuwa na afya bora.
Chagua ili kuona majibu .
Si sahihi. Sikio la mtu huyu lina dalili ya maambukizi , lina uvimbe na mabadiliko ya rangi.
Si sahihi. Kuna ishara ya kuumia na uvimbe na kuvuja damu.
Si sahihi. Kuna dalili za maambukizi nyuma ya sikio na uvimbe pamoja na mabadiliko ya rangi.
Si sahihi. Kuna uchafu unaotoka kwenye sikio.
Sahihi! Sikio la mhusika huyu lina afya. Hakuna dalili ya kuumia wala maambukizi na mfereji wa sikio upo.
Dalili za matatizo ya njia ya sikio na ngoma ya sikio
Kazi
Tazama picha hizi zinazoonyesha ndani ya sikio. Je, sikio linaonekana kuwa na afya bora?
Hapana, kuna matobo mawili kwenye ngoma ya sikio na ina rangi nyekundu.
Hapana, mfereji wa sikio ni mwekundu na umevimba.
Hapana, mfereji wa sikio umezibwa na na kitu kutoka nje ya mwili
Hapana, mfereji wa sikio umezibwa na nnta ya sikio.
Ndiyo, mfrereji wa sikio ni saafi. Ngoma ya sikio ni safi na ina rangi nyeupe/kijivu hafifu.
Onyo
Ni muhimu kutambua matatizo ya afya ya sikio mapema .
Ikiwa matatizo ya afya ya sikio hayatatibiwa kikamilifu, yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa masikio ya mhusika. Hii inaweza kusababisha upotezaji wa kusikia.