Matatizo ya masikio yanaweza kuathiri Uwezo wa kusikia. mtu aliye na shida ya masikio anaweza kupata:
- Maumivu
- Kupoteza uwezo wa kusikia
- Kutokwa na uchafu kwenye sikio, mara nyingi hutokana na maambukizi.
Hata hivyo, Matatizo mengi ya masikio yanaweza kutibiwa na Uwezo wa kusikia kwa mhusika kuwa bora zaidi au kurejeshwa kabisa katika hali yake ya kawaida.
Dokezo
Baada ya kuondoa chanzo ya Kupoteza uwezo wa kusikia, mhusika anaweza kuhisi kana kwamba anasikia inavyotakiwa kwa mara nyingine. Kila wakati Hakikisha masikio ya mgonjwa yana afya na endelea kufanya kipimo ch akusikia ili kuweza kutathmini Uwezo wake wa kusikia.
Maelekezo
Hebu tuangalie baadhi ya sababu za zilizoeleka za Matatizo ya kusikia na namna sababu hizi zinavyoweza kutibiwa au kuzuiwa.
Nnta ya sikio iliyoziba ngoma ya sikio
Sisi sote tuna nnta masikio. Nnta hii inasaidia kulinda masikio yetu. Nnta mpya inapozalishwa, nta ya zamani huondolewa kwenye sikio kwa njia ya kawaida. Hakuna haja ya kuisafisha.
Kwa kawaida nnta ya sikio huwa na rangi ya njano au au kahawia. Wakati mwingine inaweza kuwa nyeupe na dhaifu.
Ni pale tu nnta ya sikio inapoongezeka na kuziba mfereji wa sikio tunapoliona kama tatizo.

Swali
Je, ni kauli gani kati ya hizi kuhusu nnta ya sikio ni sahihi?
Chagua majibu manne.
uko sahihi kama umechagua a, c, d na e kama majibu sahihi
Nta ya sikio ni ya kawaida. Nnta ya sikio huondolewa wakati tu inapojikusanya na kuziba mfereji wa sikio.
b sio Jibu sahihi.
Nnta ya sikio ni ya kawaida na kwa kawaida hutoka yenyewe nje kupitia mfereji wa sikio.
Kutana na Pedro
Pedro ana umri wa miaka 45 na anafanya kazi katika ofisi ya serikali. Anatumia kiti cha magurudumu cha umeme.
Pedro amegundua hasikii vizuri anapokuwa anatumia simu. Anaamua kusafisha sikio lake kwa kutumia pamba.
Baada ya wiki anagundua hapati ahueni kwenye kusikia kwake.
Pedro ametembelea kliniki yake ya afya. Mhudumu wa afya anakagua Afya ya masikio la Pedro. Wakati akikagua ndani ya sikio lake kwa kutumia otoskopu anagundua kuwa sikio la Pedro limezibwa kwa nnta ya sikio
Mhudumu wa afya anasafisha masikio. Baada ya kuosha masikio, Pedro anaweza kusikia kama kawaida tena.
Onyo
Usitumie pamba kusafisha ndani ya masikio. Pamba yaweza kuifanya nnta sikio iliyoziba kuziba zaidi au waweza kugonga ngoma ya sikio na kuiharibu.
Kitu kutoka nje ya mwili kilichokonasa kwenye sikio
Kitu kutoka nje ya mwili kilichokwama kwenye mfereji wa sikio ni shida katika sikio.

Maelekezo
Utajifunza zaidi kuhusu namna ya kuondoa nta ya sikio kwa usalama au kitu kutoka nje ya mwili kilichokwama sikioni katika somo la tatu.
Maambukizi ya sikio
Maambukizi ya sikio husabibisha shida kwenye sikio. Maambukizi mengi yanaweza kutibiwa kwa matibabu rahisi tu.
Dalili za maambukizo ya sikio ni pamoja na rangi nyekundu /kubadilika rangi, uvimbe na tundu kwenye sikio. Yawezekana pia kutokwa uchafu kwenye kwa sikio.



Onyo
Kama ugonjwa wa sikio hautatibiwa, ngoma ya sikio inaweza kupasuka.
Kutana na Garret
Garret ana umri wa miaka 9 na anaishi katika kijiji cha wavuvi. Anapenda kuogea kwenye maji na marafiki zake. Garret amekuwa na maumivu ya sikio lake mara kadhaa.
Mwalimu wa Garret anawaambia wazazi wake kwamba wamegundua Garret anazungumza kwa sauti kubwa na anaweza kuwa na shida ya kusikia.
Garret anatembelea kituo cha afya na wazazi wake kwa upimaji wa afya ya masikio. Mhudumu wa afya anakagua ndani ya masikio ya Garret kwa otoskopu. Ana matundu kwenye masikio yake kwa pande zote mbili.
Kwa ruhusa ya mzazi wake, Mhudumu wa afya anampeleka Garret kwa mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.
Kama mtu ana dalili za maambukizi ya sikio
mpe rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia ili kufanyiwa tathmini na kupewa matibabu.Kuharibika kwa kusikia
Kuwa kwenye kelele kubwa mara kwa mara kUnaweza kuharibu kusikia.
Ili kuzuia Kupoteza uwezo wa kusikia, mtu anapaswa kukinga masikio yake dhidi ya sauti kubwa:
- Akiwa kazini
- Akiwa katika mazingira
- Kwa kutumia spika za masikioni kwa muda mrefu.
UnamKumbuka John?
John alistaafu kufanya kazi katika kiwanda chenye kelele kwa muda wa miaka 34. John hakuwa anavaa vifaa vya kukinga masikio dhidi ya kelele wakati akiwa kazini.
John ni mfano wa mtu ambaye amepoteza Uwezo wa kusikia kwa sababu ya kuwa kwenye kelele kubwa mara kwa mara.
Onyo
Kama utakuwa umeweka spika za masikioni Hakikisha kuwa unaseti sauti yako ya juu chini ya 60%.