Maelekezo
Katika mada hii utajifunza kuhusu afya ya masikio.
masikio yenye afya bora
Ni muhimu kukagua nje na ndani ya masikio ya mtu anayepimwa kwa pande zote mbili.
Sehemu ya nje masikio iliyo katika afya bora ina:
- Pina ambayo ina umbo na ukubwa tofauti kidogo
- Mfereji wa sikio
- Hakuna dalili za kuwa na jeraha au maambukizi.

Maelekezo
Angalia mifano ya pina zenye afya bora hapa chini.
Ikiwa hakuna pina au mfereji wa sikio haupo au umbo tofauti sana na ilivyozoeleka, mhusika anakuwa na mahitaji makubwa sana.
Toa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na kusikia.
masikio yasiyo na afya bora
Ikiwa sikio la mtu anayepimwa lina jeraha au maambukizi hiyo inaonyesha kuwa halina afya bora. Dalili za maambukizi ni pamoja na:
- Uvimbe
- Mabadiliko ya rangi (nyekundu / zambarau)
- Utokwaji (damu, usaha, maji).
Daima angalia sikio la mtu kwa kutokea mbele na nyuma.
Swali
Tazama picha hizi zinazoonyesha sehemu ya nje ya sikio. Je, sehemu hizi zinaonekana kuwa na afya njema?
Hapana. sikio la mhusika lina dalili za maambukizi na uvimbe na limebadilika rangi.
Hapana. Kuna dalili ya jeraha na uvimbe na linatokwa damu.
Hapana. Sehemu ya nyuma ya sikio kuna dalili ya maambukizi na uvimbe na pia limebadilika rangi.
Hapana. sikio linatokwa na uchafu
Ndiyo! sikio la mtu huyu lina afya njema. Halina dalili ya kuumia wala maambukizi na mfereji wa sikio upo.
Ndani ya masikio
Otoskopu inakusaidia kuangalia Matatizo ya sikio yaliyo ndani ya sikio. Otoskopu ni kifaa kuza, ambacho huangaza mwanga ndani ya sikio.
Maelekezo
Katika somo la tatu utajifunza zaidi kuhusu namna ya kutumia otoskopu
Unapotazama ndani ya sikio, utagundua kuwa sikio lina afya bora kama:
- mfereji wa sikio ni safi (haujaziba)
- ngoma ya sikio ni:
- Safi(waweza kuangalia ndani bila kuzuiwa na kitu chochote)
- Rangi nyeupe / kijivu nyepesi
- Haina matobo
- Hakuna dalili za maambukizi (uvimbe, Mabadiliko ya rangi, kutokwa na uchafu).

Swali
Tazama picha hizi zinazoonyesha ndani ya sikio. Je, sikio linaonekana kuwa na afya bora?
Hapana. Kuna matundu mawili kwenye ngoma ya sikio na inaonekana kuwa nyekundu na imevimba.
Hapana. mfereji wa sikio una rangi nyekundu na unaonekana kujeruhiwa.
Hapana. Kuna kitu kutoka nje ya mwili kwenye mfereji wa sikio.
Ndiyo! mfereji wa sikio ni safi. ngoma ya sikio ni safi na una rangi nyeupe/ kijivu nyepesi.