Baadhi ya bidhaa saidizi za kusikia hazijajumuishwa.
Maelekezo
Soma ili ujifunze kuhusu aina hizi za Bidhaa saidizi wa kusikia.
Vifaa saidizi vya kusikia vinavyowekwa ndani ya sikio
Hiki ni kifaa kilichotengenezwa maalum kusaidia kusikia. Kifaa hiki huwekwa ndani ya mfereji wa sikio la mhusika.
Vifaa hivi vinahitaji uelewa na ujuzi zaidi wa kuvigawa kwa wahitaji.
Vipandikizi vya Koklea
Watu waliopoteza Uwezo wa kusikia kwa kiwango kikubwa hadi kikubwa zaidi wanaweza kutumia vipandikizi vya Koklea
Vipandikizi hivi vina sehemu mbili:
- Sehemu moja inakuwa nje ya sikio la mtumiaji. Kichakataji sauti hukusanya sauti na kuituma kwenye kipandikizi
- Kipandikizi huwekwa ndani ya koklea kwa njia ya upasuaji. Miali ya umeme hupita kutoka sehemu moja kwenda nevu ya kusikia hadi kwenye ubongo.
Ubongo hutambua sauti hizi au mazungumzo. Hii husaidia mtu kusikia.
Hizi ni bidhaa za kiwango cha juu ambazo zinahitaji maarifa na ujuzi zaidi wakati wa kuzigawa kwa wahitaji.
Sehemu ya nje ya kifaa
Sehemu ya ndani ya kifaa
Kengele zinazotoa ishara
Tahadharisha watu ambao ni viziwi au wasiosikia vizuri kuhusu Mabadiliko katika mazingira yao kwa kutumia mtetemo au mwanga unaomulika. Kwa mfano, kutahadharisha kuhusu mtoto anayelia au kengele ya mlangoni ikilia.
Simu janja nyingi zimetengenezwa na viashiria vya kengele ndani yake.
Mifumo ya kitanzi
Aina ya mfumo wa sauti. Mfumo wa kitanzi hutumiwa na watu wenye Vifaa saidizi vya kusikia. Mfumo huwekwa kwenye majengo/vyumba na humsaidia mtu kusikia sauti anazotaka kusikia, huku akikata kelele za chinichini.
Mifumo ya kitanzi sio bidhaa inayotolewa kwa ajli ya matumizi ya mtu binafsi.
Alama ya kitanzi cha kusikia
Mfumo wa usambaji sauti
Kuongeza ukubwa wa sauti ya mwalimu darasani. sauti ya mwalimu inaweza kusikika kwa urahisi zaidi pamoja na kuwepo kwa kelele za chinichini. Mifumo hii inawanufaisha watoto wote darasani, wakiwemo watoto wenye Matatizo ya kusikia.
Mifumo ya usambaji sauti sio bidhaa inayogawiwa kutumika kwa matumizi binafsi.