Maneno muhimu
Maelekezo
Baadhi ya maneno muhimu yaliyotumika katika moduli hii yamefafanuliwa hapa chini. Unaweza kuchapisha hizi ili uyatumie unapoSoma moduli:
Bidhaa saidizi - Bidhaa saidizi ni bidhaa zinazotumiwa na watu kutekeleza kazi ambazo kwa namna fulani hawawezi kufanya vizuri, au hawawezi kuzifanya kabisa.
Kipima sauti - Kifaa cha kupima kusikia kinachotumika kupima uwezo wa kusikia.
Brele - Aina ya lugha ya maandishi kwa vipofu. Herufi zinawakilishwa na mifumo ya alama zilizoinuliwa na zinazoweza kugusika. Alama hizi husikika kwa ncha za vidole.
Kifaa saidizi cha kusikia - Kifaa kinachovaliwa kwenye sikio na watu ambao wana shida ya kusikia. Vifaa saidizi vya kusikia hufanya baadhi ya sauti kuwa kubwa zaidi ili mtu asiye na uwezo wa kusikia aweze kusikiliza, kuwasiliana, na kushiriki kikamilifu zaidi katika shughuli za kila siku.
Otoskopu - Chombo cha kukuza chenye mwanga unaotumika kukagua sikio la mtu kwa macho.
Wafanyakazi - Watu wanaofanya kazi katika sehemu za kutoa huduma au shirika. Hii inajumuisha watu ambao wamepata mafunzo katika nyanja mahususi inayohusiana na afya ambao huenda hawana sifa za kitaaluma.
Mpimaji - Mtu anayefanya upimaji.
Upimaji wa hisia za kusikia na kuona - Utaratibu wa kuangalia ikiwa macho na masikio ya mhusika yana afya na kutambua matatizo yoyote ya kuona au kusikia.
Maelekezo
Ukipata maneno mengine ambayo huyaelewi vizuri, muulize mwenzako au mshauri wako.