Kifaa saidizi cha usikivu kitadumu kwa muda mrefu na kitakuwa salama zaidi iwapo kitatunzwa vizuri.
Ili kuzuia uharibifu wa vifaa saidizi hivi, ni muhimu kuvitunza. Hii ni pamoja na:
1. Kusafisha
2. Kuepuka uharibifu wa maji
3. Kuhifadhi kwa usalama.
Kifaa saidizi cha usikivu knaweza kudumu kwa miaka 3-5 Ikiwa kitatunzwa vizuri.
Dokezo
Mjulishe mlezi wa mtoto ambaye anaweza kuwasiliana na mtoto ikiwa atahitaji vipuri vya kifaa saidizi
Usafishaji wa Vifaa saidizi vya usikivu
Maelekezo
Tazama video hii ili kujikumbusha jinsi ya kusafisha Kifaa saidizi cha usikivu.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusafisha na kutunza Vifaa saidizi vya usikivu rejea kwenye moduli ya vifaa saidizi vya usikivu vilivyosetiwa tayari vya TAP .
Swali
Ni sehemu gani ya Kifaa saidizi cha usikivu inaweza kusafishwa kwa maji?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni mdomo wa kifinyazi cha sikio!
Mdomo wa kifinyazi cha sikio ndiyo sehemu pekee inayoweza kusafishwa kwa maji. Ondoa mdomo huu kutoka kwenye bomba kabla ya kusafisha.
Kazi
Andaa kifaa cha kusafisha Kifaa saidizi cha usikivu:
- Kitambaa
- Brushi
- Waya
- Bakuli na maji ya sabuni na tishu.
Jizoeze kusafisha kila sehemu ya Kifaa saidizi cha usikivu kwa usahihi.
Epuka uharibifu wa maji
Maji yanaweza kuharibu Vifaa saidizi vya usikivu. Kinga Vifaa saidizi vya usikivu dhidi ya mvua.
Kuhifadhi kwa usalama
Mfundishe mtoto na mlezi wao jinsi ya kufanya salama:
- Kuhifadhi Vifaa saidizi vya usikivu wakati wa usiku
- Kuvitunza wakati wa usafirishaji.