Ni muhimu :
- Eleza faida za kutumia Vifaa saidizi vya usikivu
- Mfundishe mtoto na mlezi wake jinsi ya kutumia na kutunza Vifaa saidizi vya usikivu kwa usahihi.
Ikiwa mtoto anahitaji usaidizi wa kutumia vifaa saidizi vyake vya kusikia, washirikishe walezi wao.
Faida za kutumia Vifaa saidizi vya usikivu
Unapozungumza na mtoto na mlezi wao, eleza Vifaa saidizi vya usikivu:
- Rahisisha kujifunza na kuelewa mambo shuleni
- Saidia kwa kuzungumza na kucheza na marafiki
- Saidia kwa kuzungumza vizuri na kujifunza maneno mapya na kurahisisha sauti kusikika.
Kujenga matumizi
Eleza kwamba inachukua muda kuzoea kuvaa Vifaa saidizi vya usikivu kwa mara ya kwanza.
Mara ya kwanza, sauti zingine zinaweza kuwa kubwa sana au zisisikike kwa uwazi. Hii ni kawaida.
Unaweza kukabiliana na kuvaa Vifaa saidizi vya usikivu kwa kuvitumia mara kwa mara na kwa kusikiliza sauti yako na sauti nyinginezo.
Maelekezo
Pata maelezo zaidi katika vidokezo kwa watumiaji wa Vifaa saidizi vya usikivu .
Namna ya kuboresha uelewa wa maneno
Inaweza kusaidia kwa wazazi na walimu kuelewa njia mbalimbali za kumsaidia mtoto akiwa nyumbani na shuleni:
- Simama katika eneo lenye mwanga mzuri na uwe katika mkao ambao wanaweza kuona uso wako vizuri unapozungumza
- Ongea kawaida - usipaze sauti yako au kuongeza chumvi kwa namna unavyozungusha midomo yako
- Hamasisha mtu mmoja azungumze baada ya mwingine ili kumsaidia mtoto kuzingatia ni nani anayezungumza
- Mkalishe mtoto mbele ya darasa ili kumsaidia kusikia na kuona vyema
- Punguza kelele zinazotaka nje ya darasa kwa kadri uwezavyo
- Hamasisha mtoto kukujulisha ikiwa ana matatizo katika ufanyaji wa shughuli shuleni.
Maelekezo
Baadhi ya watoto wanaweza kuwa na ugumu wa kusikia vizuri katika mazingira ya darasa yenye kelele. Jifunze jinsi ya kuboresha matumizi ya Vifaa saidizi vya usikivu katika mazingira yenye kelele katika moduli ya mifumo ya kipaza sauti cha mbali ya TAP binafsi.
Kutumia Vifaa saidizi vya usikivu
Ni muhimu kumfundisha mtoto na mlezi wao jinsi ya kutumia Vifaa saidizi vya usikivu ikiwa ni pamoja na jinsi ya:
- Tambua sehemu mbalimbali za vifaa
- Kuwasha na kuzima kifaa saidizi
- Kuongeza ua kupunguza sauti
- Kukivaa na kukivua
- Kukibadilisha na kutunza betri.
Sehemu za Vifaa saidizi vya usikivu
Onyesha na ueleze sehemu tofauti za Kifaa saidizi cha usikivu.
Onyesha ni kifaa kipi cha kusikia kwa kila sikio.
Hamasisha mtoto atafute alama nyekundu ya Kifaa saidizi cha usikivu cha upande wa kulia na alama ya bluu kwa Kifaa saidizi cha usikivu cha upande wa kushoto.
Kuwasha na kuzima
Eleza: Washa na uzime Kifaa saidizi cha usikivu kwenye sehemu ya betri.
Swali
1. Je, ni njia gani unapaswa kuweka betri kwenye sehemu ya betri?
Chagua majibu mawili.
Uko sahihi Ikiwa umechagua a na c kama majibu sahihi!
Alama ya kuongeza (+) inapaswa kuelekezwa juu. Ikiwa betri imepanuka kwa upande mmoja na uko tambarare kwa upande mwingine, upande tambarare unapaswa kuwa juu. Hii inaruhusu mlango wa betri kufungwa.
2. Ni nini huwasha Kifaa saidizi cha usikivu?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua " b" kama Jibu sahihi
Ingiza betri na ufunge mlango ili uwashe. Kuweka mlango wazi huzima Kifaa saidizi cha usikivu.
Onyo
Mweleze mlezi na mtoto kwamba betri zinaweza kuwa hatari. Kama betri itamezwa, hili ni jambo la dharura ya matibabu.
Fuata Sheria za eneo ulaoishi kuhusu Sheria za utupaji salama wa betri iliyotumika.
Kuongeza ua kupunguza sauti
Onyesha jinsi ya kuongeza na kupnguza sauti.
Kukivaa na kukivua
Kabla ya kufundisha jinsi ya kuvaa na kuondoa Kifaa saidizi cha usikivu hakikisha kuwa mlango wa betri uko wazi ili kuzuia sauti yoyote ya kupuliza mluzi (mwangi).
Eleza kwamba kifinyazi cha sikio huingia ndani ya masikio yao na Kifaa saidizi cha usikivu hukaa nyuma ya masikio yao.
Mhakikishie mtoto kuwa haitamuumiza na umtie moyo kugusa kifinyazi cha sikio ili ajisikie vizuri zaidi.
Mfundishe mtoto na mlezi wao jinsi ya kuvaa na kuvua Vifaa saidizi vya usikivu kwa usahihi.
Maelekezo
Tazama video hii ili kujikumbusha jinsi ya kuvaa na kuvua Kifaa saidizi cha usikivu.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Vifaa saidizi vya usikivu rejea kwenye moduli ya vifaa saidizi vya usikivu vilivyosetiwa tayari TAP .
Dokezo
Kutumia klipu za Vifaa saidizi vya usikivu kunaweza kusaidia kuzuia Kifaa saidizi cha usikivu kuanguka. Hii ni muhimu hasa kwa watoto wadogo.
Badilisha na kutunza betri
Maelekezo
Tazama video hii ili kujikumbusha jinsi ya kubadilisha betri ya Kifaa saidizi cha usikivu.
Jaribu ujuzi wako wa kutunza betri za Kifaa saidizi cha usikivu kwa kujibu maswali yafuatayo.
Swali
1. Kwa wastani, betri ya Kifaa saidizi cha usikivu hudumu kwa muda gani?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni Wiki 2!
Betri kwa kawaida itaweka Kifaa saidizi cha usikivu kikiwa na nguvu kwa hadi wiki mbili kabla ya kuhitaji kubadilishwa.
2. Je, ni ishara gani za betri ya chini?
Chagua majibu matatu sahihi.
Uko sahihi Ikiwa umechagua a, b na e!
Kifaa saidizi cha usikivu kinaweza kuwa na ishara ya tahadhari au kisisikike kwa sauti kubwa kama hapo awali wakati betri iko chini. Inaweza pia kuacha kufanya kazi.
Dokezo
Hifadhi betri mpya mahali pa ubaridi. Daima hakikisha kuwa una seti ya betri za ziada.