Maelekezo
Baadhi ya Maneno muhimu yaliyotumiwa katika Moduli hii yameelezewa hapa chini. Unaweza kuyachapisha ili uweze kuyatumia wakati unasoma Moduli hii
Apu - Ni ufupisho wa neno linalomaanisha programu. Zana ya kidijitali inayotumika kwenye simu janja au kompyuta mpakato kufanya kazi mahususi.
Odiogramu - Grafu ya Uwezo wa kusikia wa mtu inayoonyesha sauti ya chini kabisa ambayo mtu anaweza kusikia (kiwnago cha kusikia) katika masafa tofauti ya sauti.
Kipima sauti - Kifaa cha kupima kusikia kinachotumika kupima Uwezo wa kusikia.
![Hearing test device with dials, buttons and headphones attached. One headphone is red for the right ear and one headphone is blue for the left ear.]](https://www.gate-tap.org/wp-content/uploads/2024/01/Audiometer-1024x719.png)


Kiwango cha wastani cha Uwezo wa kusikia - Hesabu inayoongeza viwango vya juu vya kusika vya 500 Hz, 1000 Hz, 2000 Hz na 4000 Hz kisha kugawanywa na nne.
Mtaalamu wa masikio na uwezo wa kusikia - Wataalamu wanaopima, kudhibiti na kutibu matatizo ya sikio na kusikia.
Mwangwi (mluzi) - sauti ya "filimbi" inayotolewa na kifaa saidizi cha kusikia wakati sauti inatoka sikioni na inachukuliwa na kipaza sauti cha kifaa saidizi cha kusikia.
Masafa - Ni mara ngapi wimbi la sauti hutembea juu na chini kwa sekunde moja. Kuna aina tofauti za sauti Ikiwa ni pamoja na sauti za ndani zaidi (masafa ya chini) kama vile ngoma na sauti kali (masafa ya juu) kama vile filimbi. masafa hupimwa kwa Hezi (Hz).
Kiwango kidogo cha sauti kinachoweza kusikika - sauti ya chini kabisa ambayo mtu anaweza kusikia katika masafa tofauti ya sauti.
Hezi (Hz) - Njia ya kupima ni mara ngapi kitu kinatokea katika sekunde moja. Kwa mfano, Ikiwa wimbi la sauti linatetemeka mara 100 kwa sekunde moja, lina mzunguko wa 100 Hz.
Sauti za Lingi - Seti ya sauti sita. Hizi hujumuisha safu kamili ya sauti za matamshi kutoka kwa masafa ya chini hadi ya juu.
Fomula ya maagizo - Hesabu ya kiwango bora cha ongezeko la sauti (kikuzaji) kinachotumika kwa kila marudio kulingana na matokeo ya upimaji wa uwezo wa kusikia wa mtu.
Kisikio cha kawaida - Kisikio kilichotengenezwa tayari kilichotengenezwa kwa ukubwa tofauti ili kutoshea ndani ya sikio la mtu. Inaunganishwa na vifaa saidizi vya kusikia kupitia bomba na kutoa sauti kwenye sikio la mtu.
Stetoklipu (bomba la kusikiliza) - Pia inajulikana kama bomba la kusikiliza, inaruhusu mtu mwenye Uwezo wa kawaida kufuatilia Ikiwa kifaa saidizi cha kusikia kinafanya kazi vizuri.
Maelekezo
Kama kuna maneno mengine ambayo huyaelewi vizuri, muulize mwenzako au mshauri wako.