Viti saidizi vya msalani
Kuna Aina tofauti za viti vya msalani vinavyotumika duniani kote
Vyoo vinawekwa katika namna ambao watu wanaweza kuvitumia kwa kuchuchumaa au kwa kukaa.

Kuchuchumaa

Kuketi
Majadiliano

Choo cha shimo/kuchuchumaa

Choo cha kukaa/kumwaga Maji
katika eneo lako, je, kuna vyoo vya kuchuchumaa au vyoo vya kukaa vinavyotumiwa kwa wingi?
Kiti saidizi cha msalani kinaweza kuwekwa juu ya aina vyoo vya aina nyingi ili kuwasaidia watu kutumia vyoo hivyo kwa urahisi zaidi.

Kiti saidizi cha msalani kikiwa juu ya choo cha kuketi
Wakati mwingine, ni rahisi zaidi kutumia kiti saidizi cha msalani kwenye eneo la faragha kuliko kuwekwa juu ya choo.
katika hali hii kiti saidizi cha msalani chenye ndoo inayoweza kuondolewa ndio kinatumika. Ndoo yaweza kusafishwa mara tu baada ya choo kutumiwa.

Kiti saidizi cha msalani chenye ndoo
Swali
Taja sababu ambazo zinaoonyesha kuwa ni rahisi zaidi kutumia kiti saidizi cha msalani chenye choo chake
Yawezekana kuwa mojawapo ya sababu zifuatazo:
- Mtu anayekaa juu ya choo kwa taabu au kuingia msalani kwa shida.
- Kiti saidizi cha msalani hakiwezi kuwekwa juu ya choo kwa usalama
- Watu wengi hutumia choo kimoja.
Kuna aina nyingi za viti saidizi vya msalani.
Kila wakati hakikisha sifa za msingi zifuatazo; zinakuwepo Wakati wa kuchagua kiti saidizi cha msalani.
Sifa muhimu
Ili kiti saidizi cha msalani kiwe salama na fanisi katika kazi yake, kinapaswa kuwa:
- Imara na vinavyodumu
- kutokushika kutu wala kulowana na Maji
- Vimetengenezwa kwa ustadi ili kuweza kuzuia mtumiaji kuumia
- Kuwa na mpira kwenye miguu (isipokuwa kama kina magurudumu)
- Kuwa na breki (ikiwa kina magurudumu, na wala sio miguu)
- Miguu ina urefu ambao unaweza kupunguzwa au kuongezwa
- Vimetengezwa maalum kwa kuweza kubeba uzito wa mtumiajimiaji.
Sifa nyingine
Sifa nyingine ambazo ni muhimu, hasa kwa watu ambao hawawezi kutembea au wanahitaji Msaada zaidi ni:
- Ndoo inayohamishika
- Magurudumu (magurudumu Yanayogeuka pande mbalimbali)
- Sehemu ya kugemesha mikono yenye urefu unaoweza kuongezwa au kupunguzwa
- Sehemu ya kuegesha mikono inayoweza kusogezwa kwa Wakati wa
- Sehemu ya kuegesha miguu yenye urefu unaoweza kuongezwa au kupunguzwa.
- Sehemu ya kukaa au kuegesha mikono iliyowekewa kitu cha kuzuia msuguano
- Sehemu ya kuegesha mgongo aliyowekewa kitu juu yake cha kuzuia msuguano
Kazi
angalia kwa makini viti saidizi vya msalani vilivyo karibu na eneo unalofanyia kazi au kwenye eneo lako unaloishi.
- Je ni sifa ngapi muhimu zilizoorodheshwa hapo juu ambazo kila kiti saidizi cha msalani kinazo?
- Je ni sifa gani "nyingine muhimu" ambazo kila kiti saidizi cha msalani kinazo?
- Je, viti saidizi vya msalani vina sifa zingine ambazo hazijaorodheshwa hapo juu?
Jukwaa la majadiliano Inafungua ukurasa mpya / dirisha jipya