Skip to main content
 Imekamilika  kwa 0%

Maelekezo

Katika Mada hii utajifunza jinsi ya kufanya upimaji wa Afya ya macho.

Sehemu ya afya ya macho ya fomu ya upimaji.

Kuosha mikono kwa kutumia maji ya bomba na sabuni.

Fanya maandalizi

  • Osha na kukausha mikono yako kila wakati (kwa sabuni au gel ya sanitizer) kabla na baada ya kila upimaji wa Afya ya macho
  • Epuka kugusa macho ya mhusika huyo
  • Mkumbushe mtoto kuwa utaangalia machoni mwao na tochi.

Upimaji wa Afya ya macho

  • Inama chini na uangalie macho ya mtoto kwa kutumia tochi, ili uweze kuona macho yake vizuri zaidi
  • Muulike jicho la kulia na kushoto kwa tochi. Epuka kuangaza tochi kwenye macho ya mtoto kwa muda mrefu zaidi ya sekunde chache
  • Rekodi matokeo kwenye fomu ya upimaji.

Matokeo:

  • Ikiwa macho yote mawili yanaonekana kuwa na afya bora chagua jibu la Ndiyo
  • Ikiwa jicho moja au yote mawili hayaonekani kuwa na afya nzuri, chagua jibu la Hapana na uandike sababu ya kwanini umechagua hivyo.

macho yote mawili lazima yawe na afya ili kurekodi matokeo ya ufaulu . Ikiwa macho moja au zaidi hayana afya rejea .

Maelekezo

Tazama Video ya upimaji wa Afya ya macho.

Kazi

Katika vikundi jizoeze kufanya upimaji wa macho kwa kila mmoja kwa kutumia tochi. angalia kwa:

  • Tongotongo au usaha kwenye ukope/kope
  • Rangi nyekundu kwenye sehemu nyeupe ya jicho
  • Inatokwa na uchafu
  • Sehemu yenye rangi ya jicho isiyo kuwa safi/ rangi ya maziwa
  • macho hayatazami uelekeo mmoja.

Je, umepata dalili zozote za Matatizo ya afya ya macho?

Maelekezo

Unaweza kutaka kurejea Somo la pili ili kujikumbusha dalili za macho yasiyo na afya bora.

Huenda isiwezekane kutekeleza uoni/upimaji wa Afya ya macho kwa mtoto.

Wakati mwingine Unaweza kuanza upimaji, lakini usiweze kuumaliza. Ikiwa haiwezekani kutekeleza sehemu yoyote ya upimaji, Mpeleke mtoto kwa wafanyakazi wa huduma ya macho.

Maelekezo

Jifunze jinsi ya kutekeleza upimaji wa kusikia na ukamilishe mpango wa upimaji katika Moduli ya kusikia na afya ya masikio kwa watoto .

Umekamilisha somo la nne!

0%
Upimaji wa Afya ya macho
Somo: 4 ya 5
Mada: 4 ya 4