Maneno muhimu
Maelekezo
Baadhi ya maneno muhimu yaliyotumika katika moduli hii yamefafanuliwa hapa chini. Unaweza kuyachapisha ili uyatumie unapopitia moduli:
Astigmatism - Watu wenye ugonjwa wa astigmatism wana shida ya kuona vizuri vitu vilivyo mbali na karibu.
Ugonjwa wa kisukari - Ugonjwa ambapo sukari ni nyingi katika damu. Hii inaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupoteza hisia sehemu za mwili (hasa miguu) na matokeo yake majeraha ya mguu, kupoteza uwezo wa kuona taratibu, kuharibika kwa figo, kukosa mkojo na ugumu wa kukumbuka mambo.
Hyperopia - Watu wenye hyperopia wana 'uoni ya umbali mrefu'. Wanaweza kuona vitu vilivyo mbali vizuri, hata hivyo, wanapata taabu kuangalia vitu vilivyo karibu.
Kutokuwa na uwezo wa kujifunza - Mtu mwenye changamoto ya kujifunza anaweza kuwa na mapungufu katika kujifunza ujuzi mpya, ikiwa ni pamoja na mawasiliano na kujitunza.
Myopia - Watu wenye myopia 'wana uoni fupi'. Wanaweza kuona vitu vilivyo karibu kwa uwazi, hata hivyo, vitu vilivyo mbali zaidi vina ukungu.
Kiziba jicho - Kitu ambacho kinatumika kufunika jicho kabisa.
Wafanyakazi - Watu wanaofanya kazi katika sehemu za kutoa huduma au shirika. Hii inajumuisha watu ambao wamepata mafunzo katika nyanja mahususi inayohusiana na afya ambao huenda hawana sifa za kitaaluma.
Hitilafu katika kuakisi - Sababu ya kawaida ya matatizo ya uoni, ambayo kwa kawaida hurekebishwa na miwani sahihi au lenzi za zinazowekwa juu ya mboni ya jicho. Kuna aina tofauti za hitilafu katika kuakisi inayopelekea matatizo tofauti ya kuona. Baadhi ya mifano ni pamoja na astigmatism, uoni wa mbali na uoni wa karibu.
Maelekezo
Ukipata maneno mengine ambayo huyaelewi vizuri, muulize mwenzako au mshauri wako.