Upimaji wa Uoni na kusikia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule

Karibu kwenye kozi ya Shirika la Afya Duniani inayohusu upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule!

Kozi hii ina moduli tatu:

Kozi hii inalenga makundi gani?

  • Watu wanaoratibu programu ya upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wa umri wa kwenda shule.
  • Watu ambao watafanya upimaji wa Uoni na kusikia. Kwa mfano, watu wanaofanya kazi kwenye afya na elimu, ikiwa ni pamoja na wauguzi, watoa huduma ya afya ya kwenye vituo vya afya vya awali, walimu, wafanyakazi wa kwenye jamii.

Kozi imendaliwa ili kufundishwa kwa namna mbili zinazofuatana. Maudhui ya mtandaoni yanapaswa kufuatiwa na mafunzo ya ana kwa ana ili kuweza kufanya mazoezi ya ujuzi wa kimatibabu na kisha mazoezi mahali pa kazi chini ya usimamizi.

Kozi hii imeandaliwa ili ifundishwe kwa kwendana na kitabu cha utekelezaji juu ya upimaji wa Uoni na kusikia kwa watoto wa umri wa kwenda shule.