Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Mtoto ameketi kwenye kiti. Mkono mmoja unaelekeza herufi kwenye chati inayoelekeza na mkono mwingine unafunika jicho moja.
Maono

Uoni na afya ya macho kwa watoto

Moduli hii inatoa utangulizi wa uoni, matatizo ya uoni na afya ya macho na jinsi ya kutekeleza uoni na upimaji wa afya ya macho kwa watoto.

Muda wa moduli: Saa 1.5 mtandaoni, ikifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa inapohitajika

Kabla ya kuanza, Hakikisha kuwa umekamilisha moduli hii:

Rasilimali zinazohitajika wakati wa upimaji

  • Utepe wa kupimia (wenye urefu wa walau mita tatu)
  • Chati ya upimaji wa uoni (chati ya HOTV na kadi ya kuelekeza na chati E)
  • Kiziba jicho (si lazima)
  • Mkanda
  • Kiti
  • Sehemu ya kunawia mikono au kitakasa mikono

Maelekezo ya uchapishaji wa chati za uoni:

  • Chapisha chati ya ukubwa sahihi. Chagua neno chapisha ukubwa halisi. Usipunguze ukubwa wa nyaraka ili iweze kutosha kwenye karatasi
  • Chapisha kwenye kadi nyeupe ya A4 ambayo ni nene na imara
  • Hakikisha herufi zimechapishwa kwa rangi nyeusi ili kuzifanya zisomeke vizuri
  • Kama picha iliyochapishwa hainekani vizuri, au ina rangi ya kijivu, usiitumie
  • Ili kuangalia kama umechapisha chati kwa ukubwa sahihi, pima ukurasa kwa kutumia rula ya 10 cm ili kuthibitisha ukubwa wake.

Bonyeza kwenye linki hapa chini kupakua na kuchapa:

Rasilimali

Bofya kwenye yafuatayo ili uweze kupakua na kuchapa taarifa zifuatazo:

Masomo

1. Uoni kwa watoto

  1. 1.1. Maneno muhimu
  2. 1.2. Uoni na matatizo ya uoni

2. Afya ya macho

  1. 2.1. Muonekano wa macho yenye afya bora
  2. 2.2. Dalili za matatizo ya kiafya ya macho
  3. 2.3. Sababu zilizozoeleka za matatizo ya kiafya ya macho

3. Kujiandaa kwa upimaji wa mishipa ya fahamu

  1. 3.1. Maandalizi ya upimaji

4. Uoni na upimaji wa afya ya macho

  1. 4.1. Taarifa kuhusu mtoto
  2. 4.2. Upimaji wa uoni wa mbali kwa watoto wenye umri wa miaka 8 na chini yake
  3. 4.3. Upimaji wa uoni wa mbali kwa watoto wenye umri zaidi ya miaka 8
  4. 4.4. Upimaji wa afya ya macho

5. Jaribio baada ya kumaliza kusoma moduli na shukrani

Mada zote
Kunja zote