Picha kwa hisani ya: © WHO / Mitasha Yu
Moduli

Upimaji wa awali wa huduma ya macho

Moduli hii inatoa utangulizi wa uoni, matatizo ya kuona na afya ya macho na jinsi ya kutekeleza upimaji wa huduma ya msingi ya macho.

Muda wa moduli: masaa 2 mtandaoni, yakifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa na mwezeshaji kama itahitajika

7 Masomo

Maelezo ya moduli

Moduli hii inatoa utangulizi wa uoni, matatizo ya kuona na afya ya macho na jinsi ya kutekeleza upimaji wa huduma ya msingi ya macho.

Muda wa moduli: masaa 2 mtandaoni, yakifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa na mwezeshaji kama itahitajika

Rasilimali ambazo utahitaji wakati wa upimaji

  • Kiti
  • Kiziba jicho (si lazima)
  • oftalmoskopu
  • Tochi ndogo yenye umbo la kalamu
  • Utepe wa kupimia (wenye urefu wa walau mita tatu)
  • Mkanda

Bonyeza kwenye linki iliyo hapa chini ili kuweza kupakua na kuchapa:

Maelekezo ya uchapishaji wa chati za Uoni:

  • Chapisha chati ya ukubwa kamili. Chagua chapisha Ukubwa halisi. Usipunguze saizi ya nyaraka ili iweze kutosha kwenye karatasi
  • Chapisha kwenye kadi nyeupe ya A4 ambayo ni nene na imara
  • Hakikisha herufi zimechapishwa kwa rangi nyeusi ili kuzifanya zisomeke vizuri
  • Kama picha iliyochapishwa hainekani vizuri, au ina rangi ya kijivu, usiitumie
  • Ili kuangalia kuwa umechapisha chati kwa ukubwa sahihi, pima rula ya 10 cm kwenye ukurasa ili kuthibitisha usahihi wake.