Maelekezo
Katika Mada hii utajifunza kuhusu baadhi ya sababu zilizozoeleka za Matatizo ya Afya ya masikio.
Sababu za matatizo ya Afya ya masikio
- sikio lililoziba
- Maambukizi ya sikio
- Vihatarishi vinavyotokana na mfumo wa maisha na mazingira.
sikio lililoziba
masikio yaliyoziba yanaweza kusababisha kupotea kwa Uwezo wa kusikia kwa muda.
sikio la mtu linaweza kuziba kwa mkusanyiko wa nnta ya sikio au kitu kutoka nje ya mwili.
Nnta ya sikio
mfereji wa sikio hutoa nata ya njano au kahawia ambayo husaidia kulinda sikio. Nnta mpya inapozalishwa, nnta ya zamani hutoka kwenye sikio kwa kawaida. Hakuna haja ya kulisafisha.
Wakati mwingine nnta hujilimbikiza kwenye sikio. Hii inaweza kuzuia mfereji wa sikio. Nnta ya sikio inayozuia mfereji wa sikio inapaswa kuondolewa kwa usalama.
Kitu kutoka nje ya mwili kwenye sikio
Hiki ni kitu kisichohitajika ambacho kimekwama kwenye sikio lakini hakipaswi kuwa humo.
kitu kutoka nje ya mwili katika sikio unapaswa kuondolewa kwa usalama.
Swali
Je, ni kauli gani kati ya hizi kuhusu nnta ya sikio ni sahihi?
Chagua majibu matatu sahihi.
uko sahihi kama umechagua b, c na d, kama MaJibu sahihi!
a Sio sahihi. Nnta ya sikio ni ya kawaida na kwa kawaida iTAPita nje ya mfereji wa sikio yenyewe. Ni wakati tu nta ya sikio inapojijenga na kuziba mfereji wa sikio ndipo inapaswa kuondolewa.
Nta ya sikio au vitu kutoka nje ya mwili inapaswa kuondolewa na wafanyakazi wa huduma ya sikio. Ikiwa mtu anajaribu kuondoa kitu kinachozuia sikio peke yake, inaweza kuwa mbaya zaidi na kusababisha madhara.

Maambukizi ya sikio
Maambukizi ya sikio yanaweza kusababisha upotezaji wa kiwango cha kusikia kwa muda.
- Maambukizi mengi yanahitaji matibabu rahisi tu
- Wakati mwingine yanahitaji upasuaji.
Baadhi ya maambukizi ya sikio ni vigumu kutambulika. KUnaweza kuwa hakuna usumbufu au kutokwa na uchafu, lakini maambukizi yanaweza kudumu kwa muda mrefu.
Dalili pekee ya tatizo inaweza kuwa kupoteza kusikia. Hii inaweza kuathiri ujifunzaji wa mtoto Ikiwa haitatibiwa.
Ikiwa haijatibiwa, maambukizi ya sikio yanaweza kusababisha kupasuka kwa ngoma ya sikio ya mtoto, na kusababisha uharibifu wa kudumu wa sikio.
Vihatarishi vya mtindo wa maisha na mazingira
Baadhi ya vitu kwenye mtindo wetu wa maisha na kwenye mazingira yetu, vyaweza kutuweka katika hatari ya kupata Matatizo ya kusikia na afya ya masikio.
UnamKumbuka Garret?
Garret ana umri wa miaka 9 na anaishi katika kijiji cha wavuvi. Anapenda kuogelea baharini na marafiki zake. Garret amepata maumivu na kutokwa na uchafu katika sikio lake mara kadhaa.
Garret ni mfano wa mtoto aliye katika hatari ya kupata magonjwa ya sikio kutokana na kuogelea kwenye maji machafu.
Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu hatari za maisha na mazingira katika Mambo ya kuzingatia ili kuwa na macho na masikio yenye afya bora .