Fomu ya vipimo
Fomu ya upimaji itakusaidia kufanya upimaji wa uwezo wa kusikia na kuona na kila mtoto na kufanya mpango.
Ikiwa mtoto tayari amekamilisha kipimo chake cha uoni na afya ya macho, ataleta fomu yake pamoja nao.
Maelekezo
Kama bado hujafanya hivyo, pakua fomu ya upimaji na uchapishe nakala.
Usiwe na wasiwasi kama hauwezi kupakua fomu. maswaliliyoko kwenye fomu yanaonyeshwa kadri unavyopitia sehemu hii ya moduli.
Angalia zifuatazo zimerekodiwa:
- Jina la mpimaji (Ikiwa zaidi ya mpimaji mmoja, ongeza majina yote mawili)
- Tarehe ya upimaji
- Mahali ambapo upimaji unafanyika.
Taarifa kuhusu mtoto
Kagua:
- Taarifa kuhusu sehemu ya mtoto imekamilika
- Thibitisha idhini kutoka kwa mzazi/mlezi ili kushiriki katika upimaji.
Endelea tu Ikiwa idhini imetolewa.
maswali awali kabla ya kuanza upimaji
Kagua kama taarifa ya upimaji kutoka kwenye maswali awali kabla ya kuanza zoezi la upimaji imenakiriwa vizuri kutoka kwenye fomu ya idhini.
Maelekezo
Angalia ufahamu wako kuhusu hatua ya kuchukua Ikiwa:
- Mtoto tayari amevaa vifaa saidizi vya kusikia au
- Mzazi/mlezi ana wasiwasi kuhusu Uwezo wa kusikia wa mtoto wao
kwa kujibu maswali. yafuatayo.
Swali
Kutana na Basir
Basir ana umri wa miaka sita na huvaa vifaa saidizi vya kusikia. Anashiriki katika programu ya upimaji wa uwezo wa kusikia na kuona shuleni.
Basir havai vifaa saidizi vyake vya kusikia wakati wa upimaji wa Uwezo wa kusikia na afya ya masikio. Mwishoni mwa upimaji Basir haipiti upimaji wa kusikia. masikio yake yote mawili yana afya.
1. Unapowajulisha wazazi wa Basir, unapaswa kupendekeza kwamba Basir afuatiliwe na wataalumu wa afya ya masikio walio sehemu anayopata huduma tumia tayari.
Je, Pendekezo hili ni sahihi?
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
Basir tayari ana vifaa saidizi vya kusikia. Afuatiliwe ili kujua kama huduma anayoitumia kwa sasa inamsaidia na kuangalia kama vifaa saidizi vya kusikia vinafanya kazi vizuri.
2. Ikiwa mzazi/mlezi ana wasiwasi kuhusu Uwezo wa kusikia wa mtoto wake, je, unapaswa kukamilisha upimaji?
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
Ni muhimu kukamilisha upimaji.
Mtoto akipitisha upimaji, jadili matokeo na mzazi/mlezi. Panga upimaji ya kufuatilia ndani ya mwezi mmoja.
Ikiwa mtoto hajafaulu upimaji
toa rufaa kwa watalaam wa masikio.