Maelekezo
Katika Mada hii utajifunza jinsi masikio yenye afya bora yanavyoonekana na dalili za Matatizo ya Afya ya masikio.
Ni muhimu kutambua jinsi masikio yenye afya na yasiyofaa yanavyoonekana kama sehemu ya upimaji wa uwezo wa kusikia na kuona.
Sehemu za sikio
sikio lina sehemu tatu:
- Sehemu ya nje ya sikio
- Sehemu ya kati ya sikio
- Sehemu ya ndani ya sikio
Sehemu ya nje ya sikio
Sehemu ya nje inaundwa na:
- Pina
- mfereji wa sikio
- Tragusi.
Tragus (sehemu ya sikio inayoziba mfereji wa sikio) iko kwenye mlango wa mfereji wa sikio.
mfereji wa sikio huunganisha sikio la nje na la kati.
Sehemu ya kati ya sikio
sikio la kati linaundwa na:
- ngoma ya sikio (utando wa timpaniki)
- Mifupa midogo ya kusikia.
ngoma ya sikio hutenganisha sikio la nje na la kati.
Tafakari
Sehemu ya kati ya sikio imeunganishwa na nyuma ya pua kwa sehemu ya mwili yenye umbo mithili ya bomba. Unapokuwa na mafua, Unaweza kuhisi kuziba kwa sikio na maumivu katika sikio lako.
- Je, umewahi kuhisi kuziba kwa sikio mojawapo au yote mawili wakati ukiwa na mafua?
- Je, unapata maumivu katika sikio lako?
Sehemu ya ndani ya sikio
sikio la ndani hubadilisha sauti kuwa kwenye mfumo wa umeme, ambao husafiri kutoka kwenye nevu ya kusikia hadi kwenye ubongo.
Haiwezekani kuona sikio la ndani wakati wa upimaji.
masikio yenye afya bora
Sehemu ya nje ya sikio lenye afya bora (pina) ina umbo na ukubwa tofauti kidogo. masikio yote yenye afya bora yana mfereji wa sikio.
Maelekezo
Angalia mifano ya pina zenye afya bora hapa chini.
Hakuna dalili za:
- Uharibifu/jeraha
- Uvimbe
- Mabadiliko ya rangi (nyekundu / zambarau)
- Utokwaji (damu, usaha, maji).
Ikiwa Pina au mfereji wa sikio haupo au una umbo tofauti sana, mtu huyo ana mahitaji makubwa zaidi na anapaswa kupewa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na kusikia.
masikio yenye afya bora hayana dalili hizi:
- Maambukizi
- sikio lililoziba.
Ngoma ya sikio inapaswa kuwa:
- Safi(waweza kuangalia ndani bila kuzuiwa na kitu chochote)
- Rangi nyeupe / kijivu nyepesi
- Hakuna matobo.