Maelekezo
Soma ili kujua Otoskopu ni nini na namna ya kuitumia kukagua masikio ya mgonjwa
Otoskopu ni nini?
Otoskopu inakusaidia kuangalia Matatizo ya sikio kwa kurahisisha kuona vizuri ndani ya sikio la mtu.
Kabla ya kutumia otoskopu Hakikisha mwanga wa otoskopu unafanya kazi.
Swali
Ni mambo gani yanaweza kusaidia Ikiwa mwanga wa Otoskopu haufanyi kazi vizuri?
Chagua majibu mawili.
Uko sahihi Ikiwa umechagua a na c kama majibu sahihi!
Ni muhimu kuwa na betri na balbu za ziada. Kubadilisha betri au balbu kUnaweza kusaidia.
b sio Jibu sahihi.
Usiguse Otoskopu. Unaweza kuiharibu.
Spekulamu ni nini?
Spekulum ni kiambatisho kwenye Otoskopu kinachoingia ndani ya mfereji wa sikio la mgonjwa.
Spekulamu za ukubwa tofauti zinaweza kuunganishwa kwenye Otoskopu.
Swali
Je, ni ukubwa gani wa kifaa cha kupanua viungo unapaswa kutumika kukagua ndani ya sikio la mgonjwa?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua " b" kama Jibu sahihi
Mifereji ya sikio ina ukubwa tofauti. Chagua spekulamu kubwa zaidi ambayo inatosha vizuri kwenye mfereji wa sikio la mgonjwa.
Kabla ya kutumia otoskopu:
- Safisha spekulamu kwa pamba na dawa ya kuua vijidudu
- Weka kifaa cha kupanua viungo (spekulamu) kwenye Otoskopu.
Maelekezo
Tazama Video juu ya kujiandaa kutumia Otoskopu.
Kazi
Mkiwa watu wawili wawili, fanya mazoezi ya kuangalia na kuandaa otoskopu.
Namna ya kukagua sehemu ya ndani ya sikio.
Muandae mtu atakayefanyiwa kipimo
Kila wakati omba ruhusa kabla ya kukagua sehemu ya ndani ya sikio la mgonjwa na ueleze kile utakachofanya.
Ikiwa mtu huyo atakubali, Hakikisha mtu huyo ameketi na kwamba uko kwenye urefu sawa na sikio lake.
Ikiwa mgonjwa huyo ni mtoto mdogo, inaweza kuwa rahisi kwake kukaa kwenye goti la mmojawapo wa wanafamilia wake.
Ikiwa mtoto ana shida kuweka kichwa chake sehemu moja, mwanafamilia anaweza kukishikilia taratibu wakati wa upimaji.
Nawa mikono yako
Onyo
Osha mikono yako kila wakati kwa sabuni na ikaushe kabla na baada ya kukagua sikio.
Kagua maumivu na uchafu ambao mgonjwa anaotokwa
Kabla ya kuangalia ndani ya sikio la mtu:
- Bonyeza tragusi taratibu na angalia kama mgonjwa anasikia maumivu yoyote. Maumivu yanaweza kuashiria tatizo la sikio. Ikiwa mtu anapata maumivu, epuka kutumia Otoskopu au uitumie taratibu sana
- Kama kuna dalili yoyote ya kutokwa na uchafu, usafishe kwanza.
Maelekezo
Utajifunza zaidi kuhusu namna ya kusafisha uchafu unaotoka sikioni Katika mada inayofuata.
Tayarisha sikio
Kiasili mfereji wa sikio umepinda na haujanyooka. Kwa kutumia mkono ambao haujashikilia Otoskopu, vuta sehemu ya nyuma ya sikio kuelekea juu na nyuma ili kunyoosha mfereji wa sikio la mgonjwa. Hii inarahisisha kuona ndani ya sikio la mgonjwa.
Kama ni mtoto mdogo vuta pinakwa nyuma (sio juu). Hakikisha pina imeshikiliwa vizuri wakati wa otoskopu.
Kila mara zingatia kuvuta pina taratibu. Inaweza kumsababishia mgonjwa maumivu!
Kushikilia Otoskopu
Shikilia Otoskopu katika mkono wako wa kulia wakati unakagua sikio la kulia la mgojwa, na mkono wako wa kushoto kama unakagua sikio la upande wa kushoto wa mgonjwa.
Shikilia Otoskopu kama unavyoweza kushikilia kalamu.
Dokezo
Kuweka kidole kimoja kwenye mfupa wa shavu la mgonjwa kUnaweza kusaidia kuingiza otoskopu vizuri.
Weka kifaa cha kupanua viungo (Spekulamu)
Usichomeke spekulamu ndani sana kwenye mfereji wa sikio. Usiingize zaidi ya nusu ya urefu wa spekulamu.
Maumivu yanaweza kusababishwa na kutoelekeza kifaa cha kupanua viungo kwa usahihi au kwa kuiingiza kwa undani sana. Maumivu yanaweza pia kusababishwa na maambukizi ya sikio la nje.
Onyo
Kila mara chomeka otoskopu taratibu ili kuepuka kusababisha maumivu au uharibifu. Sitisha upimaji Ikiwa mgonjwa anapata maumivu.
Angalia ndani ya sikio. Ikiwa huwezi kuona ngoma ya sikio, yawezekana nnta ya sikio imeziba na hivi kutokuweza kuona ndani au yawezekana otoskopu haijawekwa vizuri.
Taratibu Rekebisha nafasi ya spekulamu kwa kuelekea upande wa juu na mbele (kuelekea jicho la mgonjwa).
Dokezo
Kila mara kagua masikio yote mawili !
Fanya mazoezi kutumia otoskopu
Maelekezo
Tazama Video ya mtu akionyesha nama ya kutumia Otoskopu kuangalia sikio a mgonjwa.
Swali
1. Baada ya kutazama Video pangilia hatua vizuri kwa kuziweka nambari 1 hadi 3. Huenda ukahitaji kutazama Video kwa mara nyingine tena.
Weka katika mpangilio sahihi:
- Mwelezee mgonjwa kile utakachofanya na omba ruhusa kuendelea na zoezi.
- Vuta pina taratibu ili kunyoosha mfereji wa sikio
- Shikilia Otoskopu kama kalamu
2. Ni mkono gani unapaswa kushikilia otoskopu wakati unapokagua sikio la upande kushoto wa mgonjwa?
Chagua jibu moja.
Mkono wa kushoto ndio Jibu sahihi!
Shikilia otoskopu kwa mkono wako wa kushoto Ikiwa unakagua sikio la upande wa kushoto wa mgonjwa
3. Unapokagua sikio la mtoto, unavuta pina taratibu kuelekea upande gani?
Chagua jibu moja.
Jibu la Nyuma moja kwa moja liko sahihi!
Vuta sikio la mgonjwa taratibu ili kunyoosha mfereji wa sikio.
Dokezo
Weka otoskopu vizuri kwa kuegemeza kidole chako kidogo kwenye shavu la mgonjwa.
Kazi
Jipangeni wawili wawili, na muwe na otoskopu:
- Chagua ukubwa sahihi wa spekulamu inayotosha vizuri ndani ya mfereji wa sikio la mgonjwa.
- Bonyeza tragusi ya mgonjwa taratibu kila upande ili kuangalia upole
- Jizoeze kushikilia otoskopu na sikio la mgonjwa kwa usahihi
- Angalia ndani ya mfereji wa sikio na ngoma ya sikio.
Je, Unaweza kuona sikio la mwenzako vizuri kwa kutumia otoskopu?