Mweleze mtu huyo kwamba utauliza maswali kadhaa. majibu yake atakayotoa yatakusaidia kwenye kutengeneza mpango.
Shirikisha wanafamilia au walezi pale panapofaa.

Vifaa saidizi vya usikivu
Maelekezo
Uliza: Je, kwa sasa unatumia vifaa saidizi za Usikivu ambazo ulipewa ulipoenda kwenye huduma ya Usikivu?
Kama mtumiaji tayari anatumia vifaa saidizi za Usikivu, mpima afya ya masikio. Kisha:
- Weka kumbukumbu ya aina ya vifaa saidizi za Usikivu wanazotumia
- Angalia kama wanapata Matatizo yoyote wanapotumia bidhaa zao.
Kama mtu ana matatizo katika kutumia bidhaa saidizi yake ya Usikivu, kwa ruhusa yake, mpe rufaa kwenda kuonana na mtoa huduma katika eneo alipopata bidhaa hiyo.
Swali

Kutana na Kaleisha
Kaleisha ana umri wa miaka 79 na anatembelea familia yake. ana matatizo wakati wa kutumia vifaa saidizi vyake vya Usikivu.
Kaleisha ameacha kuvaa vifaa saidizi vyake vya Usikivu na ana matatizo ya Usikivu. Anapata ugumu wa kujiunga na mazungumzo ya familia.
Kaleisha ametembelea kituo cha afya. Mhudumu wa afya amempima afya ya masikio. masikio yake yana afya bora.
Je, ungependekeza hatua gani baadaye?
Chagua jibu moja.
Umepatia iwapo umechagua " b" kama Jibu sahihi

Ni muhimu kumrejesha Kaleisha kwenye huduma ambayo ilitoa vifaa saidizi vya usikivu ikiwezekana. Huduma inaweza kurekebisha vifaa saidizi vya usikivu na kutoa vipuri ikihitajika.
Lugha inayozungumzwa
Maelekezo
Uliza: Je, una shida kufanya mazungumzo wakati wa kuwasiliana?
Baadhi ya watu wazima na watoto wanapata shida kungumza kama njia ya kuwasiliana.
mtu ambaye hawezi kufanya mazungumzo kama njia yao ya kawaida ya kuwasiliana ana mahitaji makubwa zaidi. Mpe rufaa kwa mtaalamuu wa masikio na Usikivu.
Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu watu wanaopata shida katika Mawasiliano katika Moduli ya bidhaa saidizi za Mawasiliano za TAP.
Mabadiliko ya ghafla katika Usikivu
Maelekezo
Uliza: Je, katika miezi 3 iliyopita umekuwa na Mabadiliko ya ghafla kuhusu Uwezo wako wa Usikivu?
Kwa kawaida mtu hupoteza Usikivu taratibu baada ya muda mrefu.
Onyo
Ikiwa mtu aTAPata Mabadiliko ya Usikivu kwa ghafla ndani ya muda mfupi (kama miezi mitatu iliyopita), inaweza kuashiria tatizo kubwa la afya. Mpe rufaa mara moja kwa mtaalamuu wa masikio na Usikivu .
Kutokwa na uchafu kwenye masikio mara kwa mara
Maelekezo
Uliza: Je, kuna uchafu (majimaji)hutoka kwenye sikio/masikio yakomara kwa mara?

Kama mtu anatokwa na uchafu kwenye masikio yake mara kwa mara , inaweza kuwa ishara ya maambukizi ya sikio yanayojirudia.
Uchafu unaotoka waweza kuwa na rangi isiyo ya kawaida. Uchafu huu Unaweza pia kutoa harufu.
Maambukizi ya masikio ya mara kwa mara yanaweza kuharibu masikio na Usikivu kwa mhusika. Kwa idhini yao toa rufaa kwenda kumuona mtaalamu wa masikio na Usikivu kwa ajili ya kufanyiwa tathmini.
UnamKumbuka Garret?

Garret ana umri wa miaka 9 na anaishi katika kijiji cha wavuvi. Anapenda kuongelea pamoja na marafiki zake. Garret alipata maumivu kwenye sikio na anatokwa na uchafu mara kwa mara.
Swali
Je, mtu anayepata maambukizi ya mara kwa mara ya masikio anapaswa kupata rufaa kwa mtaalamuu wa masikio na Usikivu?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
mtu anayepata maambukizi ya masikio mara kwa mara na anatokwa na uchafu anapaswa kupelekwa kwa mtaalamuu wa masikio na Usikivu.
Majadiliano
Je , ni wataalamu gani wa masikio na Usikivu wanaopatikana katika eneo unaloishi Unaweza kutoa rufaa kwa wahitaji kwenda kuonana nao?
Je! unajua jinsi ya kutoa rufaa kwenda kupata huduma hizi?