Skip to main content
Uwezo wa kusikia

Kutambulisha Mada ya Uwezo wa kusikia

Somo: 1 ya 5
Mada: 2 ya 5
 Imekamilika  kwa 0%

kusikia ni nini?

kusikia ni uwezo wa kutambua na kuelewa sauti katika mazingira.

masikio yetu mawili hufanya kazi pamoja ili kutusaidia kuelewa:

  • Kama sauti ni kubwa au laini
  • Mwelekeo wa sauti inapotokea.

masikio yetu pia hufanya kazi pamoja ili kutusaidia kutambua maongezi ya watu katika mazingira tofauti.

Kwa nini tunahitaji kusikia?

kusikia:

  • Hutusaidia kuwasiliana na familia na marafiki zetu kwa mahitaji yetu ya kila siku
  • Ni muhimu kwa ukuaji wa Uwezo wa kuongea kwa watoto
  • Hututahadharisha kuhusu hatari iliyo karibu nasi (treni au gari likikaribia na maeneo tuliyopo au kengele).

Swali

Ni hali gani kati ya hali zifiuatazo hutumia kusikia kututahadharisha juu ya hatari inayoweza kutokea?

Chagua majibu sahihi tu.





uko sahihi kama umechagua a, b, c na d kama majibu sahihi!

Hizi zote ni tahadhari za hatari inayoweza kutokea ambazo hutumia kusikia.

Jibu e sio sahihi.

Hii hutumia uoni kutahadharisha juu ya hatari.

Je, tunasikiaje?

masikio yetu yanatusaidia kusikia. masikio hukusanya mitetemo ya sauti na kuibadilisha kuwa miali ya umeme inayotumwa kwenye ubongo. Wakati miali hii ikifika kwenye ubongo, tunasikia sauti na tUnaweza kuitambua. Sehemu zote za sikio lazima ziwe zinafanya kazi vizuri ili kuweza kusikia vizuri.

Sehemu tatu za sikio zinahusika katika namna tunavyosikia.

  1. Sehemu ya nje ya sikio hukusanya sauti kutoka angani na kuielekeza kwenye mfereji wa sikio
  2. Sehemu ya kati ya sikio huongeza ukubwa wa sauti
  3. Sehemu ya ndani ya sikio hubadilisha sauti kuwa miali ya umeme.

Ubongo hupokea na kuchakata sauti.

Maelekezo

Soma ili ujifunze kuhusu sehemu mbalimbali za sikio.

Sehemu ya nje ya sikio

Sehemu ya nje ya sikio inajumuisha pina na mfereji wa sikio .

Mbele ya pina ni tragusi . Tragusi iko kwenye mlango wa mfereji wa sikio.

Mfereji wa sikio hutoa nnta. Nnta husaidia kulinda sikio na kulisafisha kutokana na uchafu. Kawaida uchafu hutoka wenyewe ne kupitia mfereji wa sikio.

Kazi

Tafuta tragusi kwenye sikio lako na ubonyeze taratibu ili kufunga mfereji wa sikio. Je, unahisi maumivu?

Hupaswi kusikia maumivu iwapo sikio lina afya bora wakati unapobonyeza tragusi taratibu.

Onyo

Maumivu au hali ya kutokujisikia vizuri inaweza kuwa dalili ya tatizo la sikio.

Sehemu ya kati ya sikio

Sehemu ya kati ya sikio inajumuisha ngoma ya sikio (utando wa timpaniki) na nafasi ya kati ya sikio  mifupa midogo ya sehemu ya kusikia .

Ngoma ya sikio hutenganisha mfereji wa sikio na sehemu ya kati ya sikio.

Sauti zinaongezwa ukubwa zaidi katika sehemu ya kati ya sikio wakati zinapopita kwenye mifupa maalum ya kusikia.

Tafakari

Sehemu ya kati ya sikio imeunganishwa na nyuma ya pua kwa sehemu ya mwili yenye umbo mithili ya bomba. Unapokuwa na mafua, Unaweza kuhisi kuziba kwa sikio na maumivu katika sikio lako.

  • Je, umewahi kuhisi kuziba kwa sikio mojawapo au yote mawili wakati ukiwa na mafua?
  • Je, unapata maumivu katika sikio lako?

Sehemu ya ndani ya sikio

Sehemu ya ndani ya sikio ina sehemu mbili:

  • Koklea inahusika na kusikia. sauti hubadilishwa kuwa miali ya umeme, ambazo husafiri kutoka nevu ya kusikia hadi kwenye ubongo.
  • Mfumo wa vestibula hutuma habari kwenye ubongo, ambayo hutusaidia kupata uimara bila kutetereka. Matatizo katika eneo hili yanaweza kutufanya tuhisi kizunguzungu au kutokuwa na Uwezo wa kusimama imara bila kutetereka.

Nini maana ya Kupoteza uwezo kusikia na ukiziwi?

Kupoteza kusikia ni pale ambapo mtu hawezi kusikia vizuri ukilinganisha na mtu mwingine mwenye Uwezo wa kusikia wa kawaida. Anaweza kupata shida kufanya mazungumzo katika mazingira tulivu pamoja naye mazingira yenye kelele.

Kupoteza uwezo wa kusikia kUnaweza kuanza taratibu hadi kuwa tatizo kubwa.

  • Watu walipoteza Uwezo wa kusikia kwa kiwango kidogo , wastani , au kikubwa kwa sikio moja au yote mawili watakuwa wanapata taabu kushiriki kwenye mazungumzo. Hii inajulikana kama 'taabu katika kusikia'.
  • Watu waliopoteza Uwezo wa kusikia kwa kiwango kikubwa hadi kikubwa zaidi kwa masikio yote mawili ni wanajulikana kama viziwi.

Maelekezo

Watu ambao ni Viziwi hawajajumuishwa kwenye Moduli hii. Wana mahitaji makubwa zaidi. Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia.

Jifunze zaidi kuhusu Kupotea kwa uwezo wa kusikia kwa kiwango kidogo, wa wastani, mkubwa zaidi katika Moduli ya Vifaa saidizi vya TAP vya kusikia vilivyosetiwa tayari.

Dokezo

Mtu aliyepoteza Uwezo wa kusikia anaweza kufaidika kwa kupata rufaa kwenda kwenye huduma zingine za utengamo ili kupata njia mbadala za kumsaidia kwenye Mawasiliano yake.

Kazi

Washiriki wakiwa kwenye jozi:

  • mtu mmoja ameziba masikio yake pande zote kwa kubonyeza tragusi au kwa kutumia vifaa maalum vinavyowekwa masikioni kuzuia sauti
  • Mtu mwingine anatumia sauti yake ya kawaida na anajaribu kufanya mazungumzo.

Hivi ndivyo unavyohisi unapopopoteza Uwezo wa kusikia kwa kiwango kidogo hadi kiwango cha wastani.

Je, uwezo wa kusikia unapimwaje?

Kipima sauti ni kifaa cha kupima Uwezo wa kusikia kinachotumika kupima Uwezo wa kusikia. Inaweza kuwa mashine au programu kwenye kishikwambi au simu janja.

Kifaa cha kupima Uwezo wa kusikia kilicho na namba za kupiga, vitufe na spika za masikioni zilizounganishwa pamoja. Spika ya masikioni yenye rangi nyekundu kwa ajili  sikio la kulia na spika za masikioni ya bluu kwa ajili ya  sikio la kushoto.

Kipima sauti cha kwenye kishikwambi kilicho na spika za masikioni zilizoambatishwa. Spika moja ya upande wa kulia ina rangi nyekundu, na nyingine  iliyo katika sikio la upande wa kushoto ina rangi ya bluu. Kuna kitufe cha majibu kilichochomekwa upande wa kishikwambi.

Programu ya kipima sauti zilzounganishwa na simu janja kwa kutumia spika za masikioni . Spika za masikioni ni nyekundu kwa sikio la kulia, ni bluu kwa sikio la upande wa kushoto.

Mashine ya kupima sauti

Programu ya kipima sauti kwenye kishikwambi

Programu ya kipima sauti iliyoko kwenye simu janja

Maelekezo

Pata maelezo zaidi kuhusu kupima Uwezo wa kusikia katika Moduli ya TAP kuhusu vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari.

0%
Kutambulisha Mada ya Uwezo wa kusikia
Somo: 1 ya 5
Mada: 2 ya 5