Watu hupoteza Uwezo wa kusikia kwa sababu tofauti. Baadhi ya sababu zilizozoeleka ni pamoja na:
- Matatizo yanayotokea kabla, wakati au mara baada ya kuzaliwa
- Magonjwa ya masikio ni kama vile:
- Maambukizi kutoka kwa surua, matumbwitumbwi, ugonjwa wa uti wa mgongo
- Maambukizi ya sikio
- Matatizo ya masikio kama vile kuziba kwa masikio kutokana na nnta ya sikio
- Kupotea kwa uwezo wa kusikia kutokana na kuwa na umri mkubwa
- Uharibifu wa Uwezo wa kusikia, kwa mfano kutokana na kufanya kazi kwenye mazingira ya kelele
- Uharibifu wa kusikia kutokana kutumia aina fulani ya dawa au kemikali.
Athari ya Kupoteza uwezo wa kusikia
Kupoteza uwezo wa kusikia huathiri watu kwa njia mbalimbali.
Watoto waliopoteza Uwezo wa kusikia
Vichanga na watoto wanahitaji kusikia sauti za maongezi ili waweze kukuza Uwezo wa kusikiliza na kuzungumza.
Wazazi wa watoto ambao hawana Uwezo wa kusikia wanaweza kugundua changamoto hiyo ya mtoto :
- Kama mtoto haonyeshi kuiitikia sauti
- Kama mtoto ana maendeleo duni au anachelewa kuanza kuongea.
Ukosefu wa Uwezo wa kuongea unapaswa kutambuliwa na kudhibitiwa mapema. kama hatutatambuliwa mapema, mtoto anaweza kupata shida:
- Nyumbani
- Shuleni
- Wakati anapokuwa na marafiki
- Wakati akijiifunza.
Swali
Kutana na Suhaila
Suhaila ana umri wa miaka miwili na anaishi na mama yake, baba yake, pamoja na mbwa wao.
Suhaila alizaliwa akiwa kiziwi na ana hana Uwezo wa kusikia kwa kiwango kikubwa kwa masikio yote mawili.
Haonekani kama anasikia wala hamwangalii mbwa wake pale anapobweka. Bado hajaanza kuongea neno lolote.
Kwa nini Suhaila hawezi kusikia?
Chagua jibu moja.
uko sahihi kama umechagua "a" kama Jibu sahihi!
Suhaila alizaliwa akiwa kiziwi.
Dokezo
Mtu ambaye amepoteza uwezo wa kusikia kwa kiwango kikubwa anaweza kufaidika na rufaa kwenda kupata huduma nyingine za utengamo zinazoweza kumsaidia kwenye Mawasiliano. Mifano ni pamoja na Kusoma midomo na matumizi ya lugha ya alama.
Watoto waliopoteza Uwezo wa kusikia wanaweza kupata shida kujifunza shuleni.
Ikiwa mzazi hajui mtoto wake ana shida ya kusikia, anaweza kudhani mtoto wake hafanyi vizuri shuleni au hajali.
Swali
Kutana na Patryk
Patryk ana umri wa miaka sita na huenda shuleni. Patryk amekuwa na maambukizi ya mara kwa mara ya sikio.
Anaweza kusikia lakini akakosa maneno au sehemu za maneno. Mara nyingi haelewi mwalimu anasema nini darasani. Patryk huona ugumu sana kusikia mwalimu anapotazama kando au anapoketi nyuma ya darasa.
Patryk huona ugumu wa kujifunza na anarudi nyuma shuleni.
1. Je Patryk ni Kiziwi?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni hapana!
Patryk anapata shida kusikia na ana shida kufuata mazungumzo.
2. Kwa nini Patryk anaweza kuwa anapoteza Uwezo wa kusikia?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua " b" kama Jibu sahihi
Patryk hupata maambukizi ya sikio mara kwa mara . Matatizo ya sikio yanaweza kusababisha Kupoteza uwezo wa kusikia.
3. Je, kupoteza kusikia kunamwathirije Patryk shuleni?
Chagua majibu sahihi tu.
majibu yote ni sahihi!
Kupoteza kusikia kunamwathiri Patryk katika kujifunza, kushiriki na kufurahia shule.
Kujitenga na watu wengine
Mtu mwenye ulemavu wa kusikia anaweza kupata shida kushiriki kwenye mazungumzo na anaweza kuanza kuepuka mikusanyiko ya familia au ya kijamii.
Watu walio na upotezaji wa kiwango cha kusikia wanaweza kupata kutengwa na jamii.
Vipimo vya kusikia mara kwa mara ili kutambua na kudhibiti upotezaji wa kiwango cha kusikia mapema ni muhimu.
Swali
Kutana na Malika
Malika ana umri wa miaka 70 na ni bibi ambaye anaishi na familia yake. Ana shida ya kusikia na anaweza kusikia kwa taabu na anapata shida kuelewa kile ambacho mwanafamilia anasema. Malika hupata shida hasa pale wanapafamilia wanapokuwanazungumza pamoja au pale muziki unapochezwa.
Wakati mwingine Malika hukaa chumbani kwake wakati familia yake inapoburudika. Hilo humfanya ajisikie mpweke.
Kwa nini Malika amepoteza Uwezo wa kusikia?
Chagua jibu moja.
uko sahihi kama umechagua c, kama Jibu sahihi!
Malika anasikia kwa taabu. Labda hii ni kwa sababu ya Kupoteza uwezo wa kusikia. Tatizo lilitokana na kuwa na umri mkubwa.
Kupoteza uwezo wa kusikia taratibu
Mtu anaweza Kupoteza uwezo wa kusikia taratibu baada ya muda. Kupoteza uwezo wa kusikia kwa aina hii kunaitwa Kupoteza uwezo wa kusikia taratibu.
Kama mtu ataanza Kupoteza uwezo wa kusikia taratibu, ndugu. jamaa au marafiki wa karibu ndio watagundua wakiwa wa kwanza kuwa mhusika hasikii vizuri au anaongea kwa sauti kubwa kuliko kawaida.
Swali
Kutana na John
John alistaafu kazi baada ya kufanya kazi katika kiwanda chenye kelele kwa miaka 34. Akiwa nyumbani mara nyingi huongeza sauti ya televisheni. Mara nyingi huwa hamsikii mkewe Mary anapomuuliza swali.
John analalamika kwamba watu wanazungumza taratibu kwenye mazingira ya kelele. Hii inafanya iwe vigumu kwake kuwasikia wanapozungumza.
Kwa nini John anapoteza Uwezo wa kusikia?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua "d" kama Jibu sahihi!
John alifanya kazikwa muda mrefu katika kiwanda chenye kelele. Yaelekea kelele hizi ziliharibu Uwezo wake wa kusikia.
Onyo
Kelele kubwa zinaweza kuharibu Uwezo wa kusikia. Hii Inaweza kusababisha Kupotea kwa uwezo wa kusikia na sauti au milio katika masikio ya mgonjwa. Kila mara yakinge masikio yako dhidi ya sauti kubwa kwa kutumia vizibaji masikio au kinga nyingine ya sikio.
Tafakari
Je! unamjua mtu yeyote ambaye:
- Huhitaji kurudia maneno au sentensi mara kwa mara wakati wa mazungumzo
- Anapata shida kushiriki katika mazungumzo hata katika vyumba tulivu
- Husikiliza televisheni au redio kwa kuweka sauti ya juu
- Hajibu vizuri maswali wakati wa mazungumzo.
Kama jibu kwa mojawapo ya maswali hapo juu ni ndiyo, ni ishara ya uwezekano wa Kupotea kwa uwezo wa kusikia.