Wakati wa kufuatilia
Inashauriwa kumfuatilia mgonjwa mapema katiya wiki mbili na miezi miwili ili kumsaidia mtumiaji kuzoea vifaa saidizi vyake vya kusikia na kupata faida kubwa. Inapaendekezwa kupima wa mara nyingine kila baada ya miaka miwili kwa watu wazima.
Enelo la kufanya ufuatiliaji
ufuatiliaji waweza kufanyika:
- Kwa mbali kupitia Mawasiliano ya simu au simu ya Video; au
- Kwa kibinafsI - Mhusika kufika kwenye kituo
Ufuatiliaji unaofanyika kwa mgonjwa kufika kituoni
Kwa ujumla, uamuzi kuhusu namna ya kufanya ufuatiliaji wa mbali au wa mtu mwenyewe kufika kwenye kituo, unategemea kile kinachofaa zaidi kwa kulingana na hali ya mhusika. Hatahivyo, baadhi ya ufuatiliaji lazima mgonjwa awepo mwenyewe kituoni. Kwa mfano, miadi ya kutathmini kwa mara nyingine.
Kwa nini tunafanya ufuatiliji?
Ufuatiliaji wa vifaa saidizi vya kusikia utakusaidia kujua kama:
- Vifaa saidizi vya kusikia vinakidhi mahitaji ya mtumiaji
- Vifaa saidizi vya kusikia vinahitaji kurekebishwa au kubadilishwa
- Vifaa saidizi vya kusikia bado vinafaa vizuri
- mtumiaji anahitaji utatuzi wa shida yoyote kwa matumizi salama na sahihi.
Swali
Matatizo ya vifaa saidizi vya kusikia yanaweza kusababishwa na:
Chagua majibu matatu sahihi.
uko sahihi kama umechagua b, c na d, kama majibu sahihi!
Mfundishe mtumiaji jinsi ya kusafisha na kutumia vifaa saidizi vyake vya kusikia kwa usahihi ili kuepuka Matatizo.
a Sio sahihi.
Kujisikia aibu kuhusu kuvaa vifaa saidizi vya kusikia hakusababishi tatizo la vifaa saidizi vya kusikia. Hata hivyo, itaathiri ni kiasi gani mtu ananufaika kwa kutumia vifaa saidizi vya kusikia. Daima eleza faida za kutumia vifaa saidizi vya kusikia.
Nini cha kuangalia wakati wa ufuatiliaji
Angalia Ikiwa vifaa saidizi vya kusikia vinakidhi mahitaji ya mtu
Uliza maswali ili kujua kama mtu huyo ananufaika na visaidizi vyake vya kusikia katika maisha yake ya kila siku.
Angalia hali ya kifaa saidizi cha kusikia
Angalia kila kifaa saidizi cha kusikia ili kuona kama kitu chochote ni chafu au kimeharibika.
Maelekezo
Soma ili upate maelezo zaidi kuhusu matengenezo na uRekebishaji wa vifaa saidizi vya kusikia.
Angalia kifaa saidizi cha kusikia kinafaa
Angalia kila kifaa saidizi cha kusikia :
- Kinamfanya mvaaji kujisikia vizuri anaokiweka katika mfereji wa sikio lake
- Kinakaa vizuri sehemu ya nyuma ya sikio la mtumiaji.
Tatua tatizo
Iwapo mtu huyo anapata shida yoyote na vifaa saidizi vyake vya kusikia, angalia jedwali la Utatuzi wa matatizo ili kutafuta suluhu pamoja.
Weka mpango wa mambo ya kufuatilia
Tumia taarifa iliyokusanywa kuamua na mhusika kama:
- Kumfundisha zaidi/kutatua Matatizo kunahitajika
- Vifaa vya kisasa vya kusikia vinahitaji kurekebishwa au kubadilishwa
- Vifaa tofauti vya kusikia vinahitajika Ikiwa ndio, je, vinaweza kupatikana ndani ya nchi au mhusika anapaswa kupata rufaa ?
- Rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia inahitajika.
Weka miadi ya ufuatiliaji unaofuata.