Ni muhimu :
- Eleza faida za kutumia vifaa saidizi vya kusikia
- Mfundishe mtu jinsi ya kutumia vifaa saidizi vyake vya kusikia kwa usahihi.
Ikiwa mtu anahitaji usaidizi wa kutumia vifaa saidizi vyake vya kusikia, mhimize kuwashirikisha wanafamilia au mlezi wake.
Faida za kutumia vifaa saidizi vya kusikia
Eleza kwamba vifaa saidizi vya kusikia vitakusaidia kusikia na kuelewa usemi.
Kuna faida nyingi za kutumia vifaa saidizi vya kusikia. Vinaweza:
- Rahisisha kuwasiliana na familia, marafiki na wafanyakazi wenzake
- Kukulinda dhidi ya hatari zinazoweza kutokea kama vile kukuepusha kugongwa na magari
- Kuongeza Uwezo wako wa kujiamini kushiriki katika shughuli za kijamii, kuboresha afya yako ya akili na ustawi wako
- Faidisha afya ya ubongo wako na kupunguza uwezekano wa kuwa kwenye hatari ya shida ya akili.
Kujenga matumizi
Eleza kwamba inachukua muda kuzoea kuvaa vifaa saidizi vya kusikia kwa mara ya kwanza. Mara ya kwanza, sauti zingine zinaweza kuwa kubwa sana au zisizo wazi. Hii ni kawaida.
Unaweza kukabiliana na kuvaa vifaa saidizi vya kusikia kwa kuvitumia mara kwa mara na kwa kusikiliza sauti yako na sauti nyinginezo.
Maelekezo
Pata maelezo zaidi katika vidokezo vya kipeperushi cha watumiaji wa kifaa saidizi cha kusikia .
Kutumia vifaa saidizi vya kusikia
Ni muhimu kumfundisha mtu jinsi ya kutumia visaidizi vyake vya kusikia Ikiwa ni pamoja na jinsi ya:
- Tambua sehemu mbalimbali za vifaa
- Kuwasha na kuzima kifaa saidizi
- Kuongeza ua kupunguza sauti
- Kukivaa na kukivua
- Kukibadilisha na kutunza betri.
Sehemu za vifaa saidizi vya kusikia
Anza kwa kueleza kava ya kifaa saidizi cha kusikia Ikiwa na sehemu za kifaa saidizi zinazofanya kazi.
Onyesha sehemu tofauti za kifaa saidizi cha kusikia:
- Kipaza sauti ambayo hukusanya sauti
- Ndoano ya sikio ili kuunganisha kifaa saidizi cha kusikia na sehemu iliyoundwa kuingia kwenye mfereji wa sikio
- Kifinyazi cha sikio
- Fungua mlango wa betri ili kuonyesha betri ambayo huwezesha kifaa saidizi cha kusikia na kuiwasha/kuzima
- Sehemu ya kuongeza na kupunguza sauti
- Swichi ya programu inayotumika wakati wa kupanga kifaa saidizi cha kusikia.
Onyesha ni kifaa saidizi kipi wa kusikia kwa kila sikio. Alama ya rangi inaonyesha upande gani:
- Alama nyekundu ni ya sikio la kulia
- Alama ya bluu ni ya sikio la kushoto.
Kazi
Angalia vifaa saidizi vya kusikia vinavyopatikana katika huduma yako.
Je, Unaweza kuonyesha rangi nyekundu na bluu ikiashiria kifaa saidizi cha kusikia cha upande wa kulia na kushoto ?
Kuwasha na kuzima
Washa na uzime kifaa saidizi cha kusikia kwenye sehemu ya betri. Utahitaji kuweka betri kwenye sehemu ya betri.
- Kuwasha kifaa saidizi: Funga sehemu ya betri.
- Zima: Fungua sehemu ya betri kikamilifu. Hakikisha kifaa saidizi cha kusikia kimezimwa wakati hakitumiki.
Kuongeza ua kupunguza sauti
Baadhi ya vifaa saidizi vya kusikia huRekebisha kiotomatiki sauti kulingana na mazingira ambayo mtu yuko.
Kwa kuongeza kupunguza sauti kwa mkono:
- Bonyeza swichi ya kufuli kwa juu na zungusha kigurudumu cha sauti ili kuongeza sauti
- Bonyeza sehemu ya chini swichi ya kufuli au rudisha nyuma kigurudumu ili kupunguza sauti.
kifaa saidizi cha kusikia kinaweza kutoa sauti kuashiria Mabadiliko ya sauti.


Kuweka kifaa saidizi cha kusikia
Kabla ya kuweka kifaa saidizi cha kusikia, kinapaswa kuzimwa kwa kufungua kidogo mlango wa betri.
Wakati wa kuvaa kifaa saidizi anza kwanza na kifaa kinachochomekwa kwenye mfereji wa sikio kwanza:
- Shikilia kifaa saidizi cha kusikia kwa sehemu ya chini ya kifinyazi cha sikio
- Tumia mkono wako wa kulia wakati ukiweka kifaa saidizi ch akusikia kwenye sikio la kulia na mkono wa kushoto wakati ukiwa kifaa saidizi kwenye sikio la kushoto
- Kwa mkono wako mwingine vuta sikio lako taratibu kwa juu na nyuma - hii itarahisisha kuingiza kifaa kwenye sikio
- Sukuma taratibu kifaa saidizi kwenye mfereji wa sikio lako - kizungushe kidogo hadi kikae vizuri.
Kisha, tumia mkono wako mwingine kutelezesha kifaa saidizi cha kusikia juu ya sehemu ya juu ya sikio lako.
Dokezo
Tumia kifaa cha maonyesho kumfundisha mtu kuvaa na kuvua kifaa saidizi cha kusikia.
Kioo kinaweza pia kusaidia mtu anapojifunza kuvaa kifaa saidizi cha kusikia.
Kuondoa kifaa saidizi cha kusikia
- Kwanza inua kifaa saidizi cha kusikia na ukitelezeshe juu ya sehemu ya juu ya sikio lako
- Kisha ushikilie bomba karibu na sehemu ya kifaa saidizi inayochomekwa kwenye wa sikio na uitoe nje taratibu.
Maelekezo
Tazama Video hii ili ujifunze jinsi ya kuvaa na kuvua kifaa saidizi cha kusikia.
Kazi
Zoea kueleza sehemu za kifaa saidizi cha kusikia na kufundisha namna ya kukiwasha na kuondoa kwenye.
Muda wa kutumia betri
Eleza: Kwa wastani, betri itaweza kutumika kwenye kifaa saidizi cha kusikia kwa muda hadi wiki mbili kabla ya kubadilishwa. Betri inayoweza kuchajiwa inaweza kuhitaji kuchajiwa kila siku.
Mfundishe mtumiaji jinsi ya:
- Kuongeza muda wa matumizi ya betri
- Kubadilisha betri.
Kukagua na kuiwezesha betri kutumika vizuri
Pale chaji ya betri inapoisha na sauti inakuwa dhaifu au utasikia ishara ya tahadhari.
Ili kuongeza muda wa matumizi ya betri:
- Ondoa betri usiku kucha na uhifadhi kwenye kisanduku cha vifaa saidizi vya kusikia
- Ondoa betri Ikiwa huna nia ya kutumia kifaa saidizi cha kusikia kwa siku kadhaa.
Dokezo
Weka kibandiko cha betri au dokezo kwenye kalenda siku utakayobadilisha betri. Wakati betri inaisha Unaweza kuangalia kujua muda ambayo betri hiyo ilitumika.
Badilisha betri
Ili kuondoa betri ya zamani:
- Fungua mlango wa betri
- Sukuma betri nje kupitia sehemu ya chini au tumia zana ya sumaku ya betri ili kuiinua.
Ili kubadilisha betri ya zamani kwa betri mpya:
- Ondoa kibandiko cha kinga kilicho juu, pamoja na (+) upande wa betri unayotaka kuitumia
- Ingiza na alama ya kuongeza (+) inayotazama juu kwenye mlango wa betri.
Baadhi ya betri zina umbo maalum. Weka vizuri:
- Sehemu tambarare kwa juu
- Sehemu yenye nundu kwa chini.
Baada ya kuingiza betri, sauti itasikika wakati wa kuwasha kifaa saidizi. Punguza sauti kabla ya kuvaa kifaa saidizi cha kusikia.
Maelekezo
Tazama Video hii kuhusu jinsi ya kubadilisha betri ya kifaa saidizi cha kusikia.
Dokezo
Ikiwa mlango wa betri haufungi vizuri, kagua kama betri imeingizwa kwa usahihi.
Dokezo
Hifadhi betri mpya mahali pa ubaridi. Daima hakikisha kuwa una seti ya betri za ziada.
Onyo
Kumeza betri ni hatari. Weka betri mbali na watoto wadogo na wanyama. Ikitokea kwa bahati mbaya kuna mtu/mnyama amemeza betri, hili ni suala la dharura linahitaji matibabu ya dharura.
Fuata Sheria za eneo ulaoishi kuhusu Sheria za utupaji salama wa betri iliyotumika.