Skip to main content
 Imekamilika  kwa 0%

Ni muhimu kufundisha udumishaji na ukarabati wa vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari na vinavyoweza kusetiwa.

Maelekezo

Soma ili ujifunze kuhusu sehemu za kifaa saidizi ambazo kwa kawaida zinahitaji matengenezo au kubadilishwa.

Marekebisho yaliyozoeleka

Uchafu, unyevunyevu au nnta ya sikio kwenye kifaa saidizi cha kusikia inaweza kusababisha matatizo.

  • Ondoa uchafu au unyevunyevu:
    • Ondoa betri na kausha kwa kitambaa ili kuondoa unyevu wowote
    • Tumia kitambaa au brashi kusafisha kifaa saidizi cha kusikia na sehemu ya betri.
  • Ondoa nnta ya masikio: Tumia waya na brashi kuondoa nnta yoyote iliyoziba sikio.

Onyo

Usitumie maji wakati wa kusafisha. Inaweza kuharibu kifaa saidizi cha kusikia.

Maelekezo

Tazama Video tena kuhusu jinsi ya kusafisha kifaa saidizi cha kusikia.

Sehemu za kifaa saidizi ambazo huwa zinabadilishwa

Sehemu za kifaa saidizi ambazo huwa zinahitaji kubadilishwa ni pamoja na:

  • Betri
  • Ndoana ya kifaa saidizi cha kusikia
  • Sehemu ya kifaa saidizi inayochomekwa kwenye mfereji wa sikio
  • Bomba la sehemu ya kifaa saidizi inayochomekwa kwenye mfereji wa sikio.

Betri

Betri zinazotupwa baada ya matumizi kwa kawaida zinahitaji kubadilishwa kila baada ya wiki mbili. Inasaidia kuwa na betri za ziada, za kutosha kudumu kwa mwezi mmoja hadi miezi miwili.

Betri zinazoweza kuchajiwa hazihitaji kubadilishwa mara kwa mara. Inasaidia kuwa na angalau betri moja ya ziada inayoweza kuchajiwa tena.

Kifinyazi cha sikio, Bomba na kifaa saidizi na ndoana zinazoshika sikio

Kagua ili kuona kama kuna dalili za kuharibika na badilisha kama kuna ulazima.

Badilisha sehemu ya kifaa saidizi inayoingia kwenye kwenye mfereji wa sikio au sehemu nyingine kwa kutenganisha sehemu ya kipa sauti inayoshikilia kwenye sikio na sehemu inayoingia kwenye mfereji wa sikio.

Badilisha bomba au ndoana kama zimepasuka.

  • Epuka kukunja bomba wakati wa kulinganisha na sehemu ya nje ya kifaa saidizi
  • Fungua ndoano ya sikio ili kuondoa kwenye kifaa saidizi cha kusikia.
Kifinyazi cha sikio chenye ufa katikati ya sehemu ya sikioni.
Ufa kwenye sehemu ya kifaa saizi inayoingia kwenye sikio
Ufa kwenye bomba ka kifaa saidizi

UnamKumbuka Delroy?

Delroy anahudhuria ufuatiliaji wake wa miaka miwili. Mhudumu wa afya anasafisha vifaa saidizi vyake vya kusikia na kufanya ukaguzi wa usikivu kwa kutumia bomba la kusikiliza. vifaa saidizi vya kusikia vinafanya kazi vizuri.

Mhudumu wa afya anaona bomba la kifaa saidizi limekuwa gumu na liko katika hatari ya kupasuka. Bomba linabadilishwa.

Badilisha kifaa saidizi cha kusikia

Badilisha kifaa saidizi cha kusikia Ikiwa:

  • Kia nyufa kubwa
  • Kimeharibiwa na maji.

Ikiwa kifaa saidizi cha kusikia kinafanya kazi mara kwa mara au hakifanyi kazi, jaribu Utatuzi wa matatizo na ubadilishe Ikiwa ni lazima.

Dokezo

Ikiwa kifaa saidizi kitarekebishwa au kubadilishwa, inapaswa kuwekwa na kurekebishwa tena ili kuHakikisha kuwa kinafaa kwa mtu huyo.

0%
Ukarabati na matengenezo
Somo: 5 ya 6
Mada: 3 ya 4