Skip to main content
Usikivu

Nani anatumia vifaa saidizi vya kusikia?

Somo: 1 ya 6
Mada: 2 ya 5
 Imekamilika  kwa 0%

Watu waliopoteza usikivu

Kupoteza usikivu ni hutokea pale mtu anapokuwa hawezi kusikia vizuri kama anavyoweza mtu mwenye usikivu wa kawaida

Maelekezo

Pima Uwezo wako wa uelewa wa aina mbalimbali za Kupotea kwa usikivu kwa kujibu swali lifuatalo.

Swali

Kutana na Delroy

Delroy ana umri wa miaka 79. Amepoteza usikivu kwa kiwango kikubwa kwa masikio yote mawili.

Ni mambo gani kati ya mambo yafuatayo ni kweli kwa Delroy?

Chagua majibu mawili.




Uko sahihi Ikiwa umechagua a na c kama majibu sahihi!

Kiwango cha Kupotea kwa usikivu wa Delroy ni kati ya kiwango kidogo na kikubwa. Hii inaitwa ugumu wa kusikia. Watu ambao wanapata shida ya kusikia hupata taabu kushiriki kwenye maongezi na watu wengine.

Maelekezo

Iwapo hukupata Jibu sahihi, soma moduli ya bidhaa saidizi za TAP Hearing .

Vifaa saidizi vya kusikia hufanya baadhi ya sauti kuwa kubwa zaidi ili mtu aliyepoteza usikivu aweze kusikia, kuwasiliana, na kushiriki zaidi katika shughuli za kila siku.

Vifaa saidizi vya kusikia vinaweza kutumiwa na watu wa rika zote ambao wamepoteza usikivu.

mtu anaweza kuhitaji vifaa saidizi vya kusikia Ikiwa:

  • Hawezi kusikia kwa kiwango cha kusikia cha mtu mwenye usikivu wa kawaida
  • Anapata shida kusikia sauti na kuelewa mazungumzo
  • Anapata shida kushiriki kwenye mazungumzo wakati akiwa kwenye mazingira tulivu na/au yenye kelele.

Kifaa cha plastiki chenye umbo linalokiruhusu kukaa nyuma ya sikio. Ndoano ya sikio inashikamana na kifaa saidizi cha kusikia pamoja na Kifinyazi cha sikio.

Adults

Kutana na Malika

Malika ana umri wa miaka 70. Ni bibi ambaye anaishi na familia yake. Malicka ana shida ya kusikia na anapata shida kuelewa familia yake inasema nini.

Malika alifanyiwa kipimo cha usikivu na alifanyiwa tathmini ya vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari. Malika amefurahi sana. Sasa anaweza kusikia kile ambacho familia yake inasema na kushiriki kwenye mikusanyiko ya familia.

Kutana na John

John alistaafu baada ya kufanya kazi katika kiwanda chenye kelele kwa miaka 34. Akiwa nyumbani mara nyingi anaongeza sauti ya televisheni. Mara nyingi alikuwa hana Uwezo wa kumsikia mkewe Mary, pale mke wake alipomuuliza swali.

John alipimwa usikivu na alifanyiwa tathmini ya vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari.

Sasa anatazama televisheni kwa sauti ya kawaida na anaweza kumsikia mke wake, Mary.

Children

Kutana na Basir

Basir ana umri wa miaka sita na huenda shuleni na dada yake, Siti. Basir aligundulika kuwa na Uwezo wake wa kusikia umepungua baada ya programu ya upimaji wa usikivu shuleni.

Baada ya kipimo cha kusikia, kwa ruhusa kutoka kwa wazazi wake, Basir aliwekewa vifaa saidizi vya kusikia vinavyoweza kusetiwa.

Sasa anazungumza zaidi nyumbani na anashiriki darasani.

Maelekezo

Moduli hii inalenga vifaa saidizi vya kusikia kwa watu wazima. Jifunze zaidi kuhusu jinsi watoto wanavyonufaika kutokana na vifaa saidizi vya kusikia katika Moduli ya Vifaa saidizi vya kusikia vinavyoweza kusetiwa vya TAP .

Majadiliano

Je, unamfahamu mtu yeyote anayetumia vifaa saidizi vya kusikia? Je, vifaa hivi vinawasaidiaje katika maisha yao ya kila siku?

0%
Nani anatumia vifaa saidizi vya kusikia?
Somo: 1 ya 6
Mada: 2 ya 5