Moduli hii inajengwa juu ya kile ulichojifunza katika moduli ya Vifaa saidizi vya usikivu vilivyosetiwa tayari vya TAP.
Maelekezo
Soma ili ujifunze kuhusu kutoa Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa kwa watoto.
Athari za Vifaa saidizi vya usikivu
Vifaa saidizi vya usikivu huwasaidia watoto waliopoteza usikivu maongezi na sauti katika mazingira yao.
Vifaa saidizi vya usikivu vinaweza kupunguza athari za Kupoteza usikivu. Wanasaidia mtoto:
- Kujifunza shuleni
- Kutegeneza mahusiano kati ya watu kupitia mazungumzo na urafiki
- Kutengeza uwezo wa kuongea na lugha.
Tathmini ya Vifaa saidizi vya usikivu
- Watoto wenye umri wa miaka mitano na zaidi wanaweza kutathminiwa na kuwekewa Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa
- Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wanaweza pia kutumia Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa. Walakini, zinahitaji tathmini kutoka kwa mtu aliye na mafunzo ya kitaalam zaidi. Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia.
Kutana na Basir
Basir ana umri wa miaka sita na huenda shuleni na dada yake Siti,mwenye umri wa miaka mitano. Mwalimu wa Basir aliona kuwa Bashir amekuwa mkimya shuleni na hainui mkono wake juu kujibu maswali. Baada ya programu ya upimaji wa shuleni iligundulika kuwa Basir amepoteza usikivu.
Baada ya upimaji wa usikivu, kwa ruhusa kutoka kwa wazazi wake, Basir aliwekewa Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa. Kwa hivi sasa Bashir ndiye mzungumzaji zaidi nyumbani na anashiriki vizuri darasani.
Swali
Kutana na Suhaila
Suhaila ana umri wa miaka miwili na anaishi na mama yake, baba yake, pamoja na mbwa wao.
Haonekani kama anasikia wala hamwangalii mbwa wake pale anapobweka. Bado hajaanza kuongea neno lolote.
Je, ungeendelea kumtathmini Suhaila ili apewe Vifaa saidizi vya usikivu?
Jibu sahihi ni hapana!
Suhaila ana umri wa chini ya miaka mitano. Apelekwe kwa mtaalamu wa masikio na usikivu kwa ajili ya kufanyiwa tathmini.
Tathmini ya Vifaa saidizi vya usikivu inahitaji upimaji wa usikivu.
Kabla ya kufanya kipimo cha usikivu kwa watoto pima afya ya masikio ili kuangalia kama masikio yao yote mawili yana afya bora.
Matatizo ya masikio yanaweza kuathiri uwezo wa mtoto kusikia. Matatizo mengi ya masikio yanaweza kutibiwa na kusikia kwa mtoto kuboreshwa au kurejeshwa kikamilifu.
Kupima upotevu wa usikivu
Watoto waliopotoeza usikivu hawawezi kusikia vizuri kama wawezavyo watoto wenye usikivu wa kawaida.
Matokeo ya Kipimo cha usikivu yanaweza kupangwa hadi viwango sita tofauti kwa kila sikio.
Daraja | Wastani | Pendekezo |
Ndani ya kiwango cha kawaida | Wastani wa chini ya dB 20 | Watu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu hazihitajiki. Kufundisha utunzaji wa sikio. Tathmini upya baada ya mwaka 1 au mapema zaidi ikiwa mtu au mlezi atagundua mabadiliko katika kusikia au Afya ya masikio. |
Kupoteza kusikia kwa kiwango kidogo | Wastani wa 20-34 dB | Watoto: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa. Watu wazima: Fuatilia na tathmini upya katika mwaka 1. Kufundisha utunzaji wa sikio. |
Kupoteza usikivu kwa kiwango cha wastani | Wastani wa 35-49 dB | Watu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu. |
Kupoteza usikivu kwa kiwango kikubwa hadi cha wastani | Wastani wa 50-64 dB | Watu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu. |
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwa | Wastani wa 65-79 dB | Watoto: Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia. Watu wazima: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa. |
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwa zaidi | Wastani wa zaidi ya 80 dB | Watu wazima na watoto: toa rufaa mtaalamu wa masikio na kusikia. |
Swali
Je, unapendekeza watoto wapewe Vifaa saidizi vya usikivu wakati wakiwa wamepoteza usikivu kwa kiwango gani?
Chagua majibu matatu sahihi.
Kupoteza usikivu kwa kiwango kidogo, cha wastani na kikubwa ni majibu sahihi!
Kupoteza usikivu kwa kiwango kidogo kunaweza kuathiri ukuaji wa uwezo wa mtoto kuongea na uwezo wake wa kujifunza. Ni muhimu kupendekeza Vifaa saidizi vya usikivu kwa watoto waliopoteza usikivu kwa kiwango kidogo hadi kiwango kikubwa.
Watoto waliopoteza usikivu kwa kiwango kikubwa na wa kikubwa zaidi cha kusikia wana mahitaji mengi zaidi na wanapaswa kupewa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na usikivu.
Majadiliano
Je! unawafahamu watoto wanaotumia Vifaa saidizi vya usikivu? Je, vinawasaidiaje katika maisha yao ya kila siku?
Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa
Ikiwa mtoto amepoteza usikivu, anashauriwa kutumia Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa.
Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa pia vyaweza kutumiwa na watu wazima.
Maelekezo
Ikiwa mtu mzima anahitaji Vifaa saidizi vya usikivu inayoweza kusetiwa toa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na usikivu.
Sehemu za kifaa saidizi
Maelekezo
Pima ujuzi wako wa sehemu za Vifaa saidizi vya usikivu katika kazi hii.
Kazi
Kwa visaidizi vya usikivu vinavyoweza kuratibiwa vinavyopatikana katika huduma yako, unaweza kupata sehemu zifuatazo za Kifaa saidizi cha usikivu?
- Kipaza sauti
- Ndoana ya Kifaa saidizi cha usikivu
- Kifinyazi cha sikio ya ukubwa wa kawaida
- Betri
- Swichi ya sauti
- Swichi ya programu
- Sehemu ya kuungaisha programu iko wapi?
- Je, Kifaa saidizi cha usikivu kinaunganishwa vipi kwenye simu/kishikwambi au kompyuta?
Tumia mwongozo wa bidhaa saidizi kupata majibu ya maswali haya.
Maelekezo
Iwapo huna uhakika kuhusu sehemu yoyote na kile wanachofanya, kagua Somo la kwanza katika moduli ya Vifaa saidizi vya usikivu vilivyosetiwa tayari kwa TAP .
Marekebisho ya Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa
Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa vinarekebishwa kulingana na mahitaji ya mtu binafsi.
Vinaweza kurekebishwa kwa:
- Programu maalum ya kwenye kompyuta
- Programu kwenye simu.
Vinatoa vipengele vya ziada kwenye kuseti ili kufanya sauti isikike vizuri zaidi. Hii ni muhimu ili kusaidia watoto kujifunza na kuongeza stadi za lugha.
Swali
Ni aina gani ya Vifaa saidizi vya usikivu inapendekezwa kwa watoto?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua " b" kama Jibu sahihi
Watoto wanapaswa kupewa Vifaa saidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa kwa masikio yote mawili.