Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
 Imekamilika  kwa 0%

Baada ya mahojiano ya tathmini, fanya mpango na mtoto na mlezi wao. Mpango huo unaweza kujumuisha:

  • Ufuatiliaji wa usikivu
  • Kupewa rufaa
  • Utoaji wa Vifaa saidizi vya usikivu
  • Kumfundisha mtoto na mlezi wao jinsi ya kutumia Vifaa saidizi vya usikivu kwa usalama
  • Kufanya uteuzi wa kufuatilia.

Fuatilia usikivu

Unapaswa kufuatilia watoto wenye kiwango cha kawaida cha kusikia na kupanga ufuatiliaji katika mwaka mmoja kwa kuwapima tena usikivu.

Mhimize mtoto na mlezi kurudi haraka ikiwa kuna mabadiliko katika kusikia.

Unamkumbuka Anju?

Matokeo ya upimaji wa usikivu wa Anju yalikuwa ndani ya masafa ya kawaida ya kusikia katika masikio yote mawili.

Mhudumu wa afya anaeleza kuna baadhi ya mambo rahisi ambayo yatasaidia kuweka masikio ya Anju kuwa na afya bora ikiwa ni pamoja na:

  • Epuka kuweka chochote ndani ya masikio
  • Epuka kuogelea kwenye maji machafu
  • Tumia viziba masikio unapokuwa katika mazingira yenye kelele.

Mhudumu wa afya anamwomba Anju na wazazi wake warudi baada ya mwaka mmoja kufanya tena kipimo cha usikivu kama njia ya kumfuatilia Anju. Anawaelezea kuwa wanaweza kurudi mapema ikiwa Anju atapata maumivu ya sikio, atatokwa na uchafu au kutakuwepo na mabadiliko katika kusikia.

Toa rufaa

Watoto wengine wanahitaji tathmini ya kitaalamu zaidi na mtaalamu wa masikio na usikivu.

Hupaswi kutoa Vifaa saidizi vya usikivu kwa:

  • Watoto waliopoteza usikivu kwa kiwango kati ya kikubwa hadi kiwango kikubwa sana.
  • Watoto walio na upotezaji wa kusikia usio na usawa -wa zaidi ya dB 15 tofauti kati ya sikio la upande wa kulia na la upande wa kushoto.

Kwa ruhusa ya mlezi toa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na usikivu.

Ikiwa hujiamini kuhusu matokeo ya kipimo, jadiliana na mshauri wako na toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na usikivu.

Swali

Soma visa mkasa vifuatavyo.

1. Beth ana umri wa miaka 13. Kiwango cha wastani cha kusikia kwa sikio lake la kulia ni dB 67. Kiwango cha wastani cha kusikia katika sikio lake la kushoto ni dB 69.

Angalia jedwali la kiwango cha upotevu wa usikivu.

DarajaWastaniPendekezo
Ndani ya kiwango cha kawaidaWastani wa chini ya dB 20Watu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu hazihitajiki. Kufundisha utunzaji wa sikio. Tathmini upya baada ya mwaka 1 au mapema zaidi ikiwa mtu au mlezi atagundua mabadiliko katika kusikia au Afya ya masikio.
Kupoteza kusikia kwa kiwango kidogoWastani wa 20-34 dBWatoto: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa. Watu wazima: Fuatilia na tathmini upya katika mwaka 1. Kufundisha utunzaji wa sikio.
Kupoteza usikivu kwa kiwango cha wastaniWastani wa 35-49 dBWatu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu.
Kupoteza usikivu kwa kiwango kikubwa hadi cha wastaniWastani wa 50-64 dBWatu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu.
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwaWastani wa 65-79 dBWatoto: Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia. Watu wazima: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa.
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwa zaidiWastani wa zaidi ya 80 dBWatu wazima na watoto: Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia

Ni kitu gani unapaswa kufanya baadaye?

Chagua jibu moja.



Kutoa rufaa ni sahihi!

Beth amepoteza usikivu kwa kiasi kikubwa. Kwa ruhusa ya walezi wake, anapaswa kupewa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na usikivu ili afanyiwe tathmini ya kitaalamu zaidi.

2. Jampa ana umri wa miaka 11. Kiwango cha wastani cha kusikia kwa sikio lake la kulia ni 23 dB. Kiwango cha wastani cha kusikia katika sikio lake la kushoto ni 55 dB.

Ni kitu gani unapaswa kufanya baadaye?

Chagua jibu moja.



Kutoa rufaa ni sahihi!

Jampa ana tofauti zaidi ya dB 15 kati ya sikio lake la upande wa kulia na la upande wa kushoto. Kwa ruhusa ya walezi wake, anapaswa  kupewa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na usikivu kwa ajili ya tathmini ya kitaalamu zaidi.

Ridhaa

Watoto wengine watafaidika na Vifaa saidizi vya usikivu.

Eleza faida zinazowezekana za Vifaa saidizi vya usikivu na utoe fursa kwa mtoto kupata uzoefu wa kutumia Vifaa saidizi vya usikivu kabla ya kuamua.

Ikiwa mtoto au mlezi wao anapendelea kutopewa Vifaa saidizi vya usikivu, wahimize kurudi kwenye huduma ikiwa watabadilisha mawazo yao wakati wowote.

Rekodi ikiwa mtoto na mlezi watatoa idhini ya kutoa Vifaa saidizi vya usikivu.

Apewe Vifaa saidizi vya usikivu

Kwanza chagua aina ya Vifaa saidizi vya usikivu inayoweza kupangwa kutoka kwa chaguo zilizopo.

Rekodi maelezo kwenye fomu ikiwemo:

  • Kifaa saidizi cha usikivu
  • Sehemu ya kifaa saidizi inayochomekwa kwenye mfereji wa sikio
  • Betri.

Dokezo

Kagua namna kifaa kilivyofungwa na mwongozo wa mtumiaji ili kuona namba za utambulisho wa kifaa. Namba ya utambulisho ya kifaa saidizi kinachoweza kusetiwa inayoweza kurekodiwa kwenye programu wakati Kifaa saidizi cha usikivu kinapokuwa kimeunganishwa.

Kufundisha namna ya kutumia Kifaa saidizi cha usikivu

Ili mtoto apate manufaa zaidi kutokana na Vifaa saidizi vya usikivu, ni muhimu kumweleza mtoto na mlezi wake:

  • Faida za Vifaa saidizi vya usikivu
  • Jinsi ya kutumia na kutunza Vifaa saidizi vya usikivu
  • Jinsi ya kuangalia chaji ya betri na wakati wa kubadilisha betri
  • Namna ya kuboresha uelewa wa maneno.

Maelekezo

Jifunze zaidi katika Somo la nne kuhusu jinsi ya kutumia Vifaa saidizi vya usikivu.

Ufuatiliaji

Watoto wanahitaji muda wa kuzoea kutumia Vifaa saidizi vya usikivu. Ushauri juu ya utatuzi rahisi wa shida unaweza kusaidia.

Ni muhimu kufuatilia ana kwa ana na mtoto na mlezi wao ndani ya wiki mbili ili kuangalia jinsi mtoto anavyoendelea.

Maelekezo

Jifunze zaidi katika Somo la tano kuhusu ufuatiliaji wa Vifaa saidizi vya usikivu.

Maelekezo

Pima uelewa wako kwa kutengeneza mpango wa Basir.

Swali

Unamkumbuka Basir?

Basir ana umri wa miaka sita na anaenda shuleni pamoja na dada yake wa miaka mitano, Siti. Baada ya kupimwa shuleni Basir alipewa rufaa ya kwenda kupimwa usikivu. Basir aligundulika kuwa amepoteza usikivu. Matokeo yanaonyesha Basir ana kiwango cha wastani cha kusikia cha dB 53.75 katika sikio lake la upande wa kulia na dB 56.25 katika sikio lake la upande wa kushoto.

Angalia jedwali la kiwango cha upotevu wa usikivu.

DarajaWastaniPendekezo
Ndani ya kiwango cha kawaidaWastani wa chini ya dB 20Watu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu hazihitajiki. Kufundisha utunzaji wa sikio. Tathmini upya baada ya mwaka 1 au mapema zaidi ikiwa mtu au mlezi atagundua mabadiliko katika kusikia au Afya ya masikio.
Kupoteza kusikia kwa kiwango kidogoWastani wa 20-34 dBWatoto: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa. Watu wazima: Fuatilia na tathmini upya katika mwaka 1. Kufundisha utunzaji wa sikio.
Kupoteza usikivu kwa kiwango cha wastaniWastani wa 35-49 dBWatu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu.
Kupoteza usikivu kwa kiwango kikubwa hadi cha wastaniWastani wa 50-64 dBWatu wazima na watoto: Vifaa saidizi vya usikivu.
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwaWastani wa 65-79 dBWatoto: Toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia. Watu wazima: Kifaa saidizi cha usikivu unaofaa.
Kupotea kwa usikivu kwa kiwango kikubwa zaidiWastani wa zaidi ya 80 dBWatu wazima na watoto: toa rufaa mtaalamu wa masikio na kusikia.

Je, ungependekeza hatua gani kwa Basir?

Chagua jibu moja.



Kutoa Vifaa saidizi vya usikivu ni sahihi!

Basir amepoteza usikivu kwa kiwango cha kati kwa masikio yote mawili. Endelea kutafuta kipimo sahihi kama itashauriwa kutumia Kifaa saidizi cha usikivu

Umekamilisha somo la pili!