Weka kiti saidizi cha msalani au bafuni mahali ambapo kiTatumika
mahali pa kukagulia
Jadili na mtumiaji (na mlezi wake au familia inapofaa\) ambapo wangependa kiti saidizi cha msalani au bafuni kiwekwe.
Kagua kama:
- Kuna njia nzuri kwenda eneo linapotumika na njia haina vikwazo vyovyote
- Liko eneo la faragha
- Lina nafasi ya kutosha
- Miguu yote miNne ya kiti saidizi iko kwenye usawa na sakafu
- Kuna mahali pa kunawa mikono (kwa kiti saidiz cha msalani).
Ikiwa mtumiaji atahitaji Msaada, chumba cha ziada kitahitajika kwa mtumiaji atakayesaidia kusonga na kugeuka.
Kazi
UnamKumbuka Bi Sofia?
Sofia hutumia rolata kutoka sehemu moja hadi nyingine.
angalia choo cha Sofia.
Je, kinafaa kwa ajili yake?
Ni kitu gani kinakifanya kimfae?
Ndio, choo cha Sofia kinaonekana kuwa kinafaa.
- Kuna njia nzuri na isiyo na vikwazo
- Liko eneo la faragha
- Lina nafasi ya kutosha
- Miguu yote miNne ya kiti saidizi cha msalani imefika kwenye sakafu
- Kuna mahali ambapo Sofia anaweza kuosha mikono yake
- Lina taa nzuri.
Kazi
Je unamKumbuka Cali?
Cali ina Maumivu kwenye maungio na hupata kutembea kwa uchungu.
angalia bafuni kwa Cali.
Je, bafu la Cali linafaa?
Ni kitu gani kinakifanya kimfae?
Ndio bafu ya Cali inaonekana inafaa.
- Liko eneo la faragha
- Lina nafasi ya kutosha
- Miguu yote miNne ya kiti saidizi cha msalani na bafuni limefika kwenye sakafu.
- Lina mahali ambapo Cali anaweza kuosha mikono yake
- Lina taa nzuri.
Vyoo na sehemu za kuoga katika makazi ya dharura
Tafakari
Watu wenye ulemavu walitoa dukuduku zao kuhusu makazi yao ya dharura. Waliripoti kwamba wangependa kukaa nyumbani kuliko kuwa kwenye makazi ya dharura, licha ya kuwepo hatari Wakati wa mafuriko na vimbunga. Wasiwasi wao ni pamoja na:
- Matope na njia mbaya
- Hakuna vifaa vya kupanda ngazi au sehemu za kushikiria kupanda jengo lililoko kwenye muinuko
- Milango kwenda kwenye vyoo na maeneo ya kuoga ni nyembamba sana kwa watumiaji wa Kiti saidizi cha magurudumu kuweza kuingia ndani.
- Hakuna vyuma vya kushikiria msalani
- Vyoo vyote vilikuwa vyoo vya kuchuchumaa.
Kwa kutumia matokeo haya, mamlaka zilifanya kazi pamoja na wanajamii, ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha kuwa makazi hayo Yanapatikana kwa kila mtu. Baadhi ya hatua muhimu zilikuwa ni:
- Njia za kudumu za Kiti saidizi cha magurudumu zilijengwa bila vikwazo.
- Wakati jengo lijengwa, sakafu za juu, vifaa vya kupanda ngazi na sehemu za kushikilia ziliwekwa kando mwa ngazi.
- Sehemu za kupita kwenda msalani na sehemu ya kuoga ziliongezwa ukubwa
- Viti saidizi vya msalani na bafuni viliwekwa kwenye vyumba vya msalani kadhaa, ili kusaidia watu kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa usalama.
Kupunguza vikwazo vya mazingira
Kazi
Kwa kila picha iliyo hapa chini; Je, ni njia gani nzuri ya kuondokana na kizuizi?
1. Kizuizi: Sogea sehemu ya kupita ya mlango.
Kutumia kifaa saidizi cha kupandia ngazi kinachobebeka na kuongeza vyuma vya kushikilia au reli ya kupita ni suluhisho nzuri.
2. Kizuizi: Mlango unafunguliwa kwa ndani, unapunguza nafasi ndani.
Bana mlango ili ufungue kwa nje au badilisha mlango uwe wa kuteleza. Mambo yote mawili yaweza kuwa na ufumbuzi mzuri.
Rejea moduli ya vifaa saidizi vya kupanda ngazi vya TAP vinavyobebeka.
Rejea moduli ya vyuma vya kushikilia ya TAP ili kupata habari zaidi juu ya vyuma vya kushikilia
Umekamilisha Somo la Tatu!
Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.
Jukwaa la majadiliano Inafungua ukurasa mpya / dirisha jipya