Mambo yanayosababisha matatizo ya kiafya za macho
Maelekezo
Katika mada hii utajifunza kuhusu sababu za kawaida za matatizo ya afya ya macho.
Sababu zinazoweza kusababisha matatizo ya afya ya macho
Shida za kiafya za macho zinaweza kusababishwa na:
- Kisukari
- Maambukizi ya macho
- Vihatarishi vinavyotokana na mfumo wa maisha na mazingira.
Kisukari
Ugonjwa wa kisukari unaweza kuathiri afya ya macho. Tatizo hili linaweza kusababisha upotezaji wa uoni au upofu baada ya muda. Hata hivyo, linaweza kuzuiwa ikiwa matatizo ya uoni yatatambuliwa mapema.
Kwa sababu hii, ni muhimu kuwauliza wazazi/walezi kama mtoto ana kisukari.
Mtoto mwenye ugonjwa wa kisukari anapaswa:
- Kuwa chini ya uangalizi wa daktari au huduma ya kisukari
- Kufanyiwa upimaji na wataalam wa huduma ya macho mara kwa mara.
Majadiliano
Jadili na wanafunzi wenzako:
- Kwenye eneo unaloishi; watu wenye ugonjwa wa kisukari hupata wapi matibabu?
- Ni namna gani unawaelekeza watu kwenda kupata hizo huduma ?
Maambukizi ya macho
Ni kawaida watoto kupata maambukizi ya macho. Maambukizi haya yanaweza kusababisha uvimbe, uwekundu, na usumbufu kuzunguka macho. Baadhi ya maambukizi na uvimbe wa jicho huhitaji matibabu ya kawaida tu.
Ikiwa maambukizi haya yayatatibiwa mapema, yanaweza kusababisha:
- Umuhimu wa matibabu makubwa zaidi kama vile upasuaji
- Uharibifu wa kudumu kwa macho.
Swali
Maambukizi ni sababu mojawapo ya uvimbe karibu na macho. Ni Je, sababu zipi zingine zinaweza kusababisha uvimbe?
Chagua majibu matatu sahihi.
Ikiwa umechagua a, b na c uko sahihi!
d Sio sahihi.
Matatizo ya uoni hayasababishi uvimbe karibu na macho. Matatizo ya uoni yanaweza kukufanya upate shida kuona vizuri.
Vihatarishi vya mfumo wa maisha na vya mazingira
Mfumo wa maisha na mazingira ya mhusika vyanaweza kusababisha matatizo ya kuona na afya ya macho.
Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu vihatarishi vinavyotakana na mfumo wa maisha na mazingira kwenye mada ya Mambo ya kuzingatia ili kuwa na macho na masikio yenye afya bora . Kwa habari zaidi kuhusu jinsi matatizo mengi ya afya ya macho au masikio yanavyoweza kuzuiwa au kudhibitiwa, rejea nyenzo za kukuza afya za WHO katika Dira na uchunguzi wa kusikia kwa kijitabu cha utekelezaji wa watoto wa umri wa kwenda shule .
Kutana na Ionita
Ionita ni kijana. Anatumia miwani ili kuweza kuona karibu pamoja na kusoma kwa urahisi zaidi.
Ionita alipokuwa mdogo alipenda kusoma sana na ilikuwa nadra sana kutumia kutumia muda mwingi kucheza nje ya nyumba.
Alipata matatizo ya kuona alipokuwa na umri wa miaka saba.
Maelekezo
Kukagua ujuzi wako wa namna mfumo wa maisha pamoja na mazingira vinavyoweza kusababisha matatizo ya kuona na afya ya macho kwa kujibu maswali yafuatayo.
Swali
1. Kutumia muda mwingi kwenye mwangaza wa jua kunaweza kusababisha matatizo ya masikio baadaye maishani.
Je, kauli hii ni ya kweli au sio ya kweli?
Jibu la "Sio kweli" ndio sahihi!
Kutumia muda mwingi kwenye mwangaza wa jua kunaweza kusababisha matatizo ya macho baadaye maishani. Kuvaa kofia kubwa au miwani ya jua kunaweza kusaidia.
2. Kuwahimiza watoto kutumia dakika 90 nje kila siku kunaweza kupunguza uhitaji wa miwani.
Je, kauli hii ni ya kweli au sio ya kweli?
Jibu la "Kweli" ndio jibu sahihi!
Kuwa nje ya nyumba kwa muda kila siku ni muhimu ili kuwa na macho yenye afya bora na kunaweza kupunguza uhitaji wa miwani.
3. Rubela, surua, matumbwitumbw na uti wa mgongo vinaweza kusababisha uharibifu wa kuona na kusikia.
Je, kauli hii ni ya kweli au sio ya kweli?
Jibu la "Kweli" ndio jibu sahihi!
Chanjo zinaweza kusaidia kuzuia magonjwa haya ambayo yanaweza kuharibu uwezo wa kuona na/au kusikia kwa mtoto.