Kufuta na na kuosha masikio kUnaweza kuwa sehemu muhimu ya upimaji wa afya ya masikio.
Maelekezo
Jifunze kuhusu wakati gani unapaswa kufuta masikio, na wakati unapaswa kuosha masikio.
Kufuta masikio
Unapaswa kufuta masikio ya mgonjwa Ikiwa mtu huyu anatokwa uchafu.
Kufuta sikio ni njia salama ya kuondoa uchafu unaotoka kwenye sikio la mgonjwa.
Onyo
Usifute sikio la mgonjwa Ikiwa anapata maumivu makubwa unapofanya hivyo.
Elezea
Omba ruhusa kabla ya kufuta uchafu wa mgonjwa na mwelezee kile utakachofanya.
Nawa mikono yako
Osha mikono yako kila wakati kwa sabuni na kausha kabla na baada ya kufuta uchafu kwenye masikio.
Fanya maandalizi
Pinda sehemu ya mwisho ya kitambaa ambacho ni safi ili kutengeneza 'utambi wa tishu'.
Kufuta uchafu unaotoka kwenye sikio
Shikilia utambi wa tishu kwa mkono wako wa kulia kama unachunguza sikio la kulia la mgonjwa , na mkono wako wa kushoto Ikiwa unachunguza sikio la kushoto la mgonjwa.
- Taratibu vuta pina kwa juu na nyuma kama unampima mtu mzima au kwa nyuma kama unampima mtoto
- Zungusha taratibu utambi wa tishu kwenye mfereji wa sikio la mgonjwa kwa sentimeta 2 hadi 3.
- Uache kwenye sikio kwa takriban sekunde 10
- Vuta utambi na uone kama una usaha au umajimaji mwingine juu yake
- Tupa utambi ambao umeutumia hivi punde. Fuata miongozo ya eneo ulipo kuhusu kutupa utambi uliotumika kwenye masikio
- Rudia zoezi kwa kutumia utambi mwingine wa tishu
- Endelea kurudia zoezi hadi utambi wa tishu usiwe na unyevunyevu wowote
- Angalia katika sikio la mgonjwa kwa kutumia otoskopu ili kuthibitisha kama uchafu wote umeondolewa.




Maelekezo
Tazama Video ya kufuta uchafu kwenye sikio la mgonjwa.
Kazi
Washiriki wakiwa kwenye jozi:
- Eleza kwamba, kwa idhini yao, utasafisha masikio yao ili kuondoa majimaji
- Fanya mazoezi ya kuandaa utambi wa tishu
- Ingiza utambi wa tishu ili kusafisha sikio la mgonjwa.
Una maoni gani kuhusu kusafisha sikio kwa kufuta uchafu?
Kuosha masikio
Kuosha sikio hutumiwa kusafisha nnta au kitu kutoka nje ya mwili kilicho kwenye mfereji wa sikio la mgonjwa.
Haupaswi kuosha sikio Ikiwa mfereji wa sikio wa mgonjwa bado haujazibwa na nnta ya sikio.
Onyo
Uoshaji sikio haufai kufanywa kama mgonjwa:
- Amefanyiwa upasuaji wa sikio hivi karibuni
- Ana tundu kwenye ngoma ya sikio
- Maambukizi ya sikio
- Maumivu ya sikio.
Ikiwa jibu ni ndio kwa swali lolote hapo juu,
toa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa huduma ya masikio na kusikia.Seti /Mfuko wa vifaa vya kuosha masikio
Utahitaji:
- Maji safi (yaliyochemshwa na kupozwa hadi kuwa sawia na joto la mwili)
- Sindano ya mililita 20 (bila sindano)
- Sahani yenye umbo la figo au bakuli lingine
- Tishu
- Karatasi ngumu au kitambaa (kitakachofunika sehemu ya juu ya bega la mgonjwa).
Ni muhimu maji yawe na joto la mwili (joto kidogo).
Pima joto la maji kwa kumwaga maji ndani ya kifundo cha mkono wako. Yanapaswa kuwa na joto kidogo sio kuwa ya moto au ya baridi.
Onyo
Kila mara kagua joto la maji kabla ya kuosha sikio.
Kama mtu anapata kizunguzungu wakati wa akioshwa sikio, sitisha na kagua tena joto la maji.
Swali
Maji yanapaswa kuwa joto gani ili yafae kuosha sikio?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni Joto kidogo!
Kama maji ni moto au baridi, yanaweza kumfanya mgonjwa kuhisi kizunguzungu. Maji ya moto pia yanaweza kumuunguza.
Elezea
Kila mara omba ruhusa kabla ya kuosha masikio na ueleze kile utakachofanya.
Nawa mikono yako
Kila mara osha mikono yako kwa sabuni na uikaushe kabla na baada ya kuosha masikio.
Fanya maandalizi
- Kagua joto la maji
- Jaza sindano na maji
- Mwambie mtu huyo kushikilia sahani yenye umbo la figo au bakuli nyingine chini ya sikio lake na kuibana kwenye shingo yake
- Weka ncha ya sindano kwenye mfereji wa sikio wa mgonjwa
- Elekeza sindano ili ielekee juu ya mfereji wa sikio, na nyuma kidogo.
Dokezo
Ncha ya sindano imewekwa vizuri ndani ya mfereji wa sikio la mgonjwa.
Uelekep ni mbali na ngoma ya sikio la mgonjwa. Hii ni salama na humfanya mgonjwa ajisikie vizuri zaidi.
Kuosha sikio
- Bonyeza sindano kusukuma maji kwenye mfereji wa sikio la mgonjwa
- Maji yatamwagika ndani ya bakuli na yanaweza kuwa na nnta au kitu chochote kutoka nje ya mwili
- Kagua sikio la mgonjwa kwa mara nyingine kwa kutumia otoskopu
- Rudia kuosha hadi nta ya sikio iliyoziba au kitu kutoka nje ya mwili utolewe
- Kagua sikio la mgonjwa kila baada ya kuosha.
Ikiwa sikio la mgonjwa bado limezibwa na nnta baada ya majaribio matatu, muombe arudi siku inayofuata na rudia kuosha sikio.
Ikiwa nnta ya sikio haijaondolewa baada ya kuosha mara mbili, kwa ruhusa ya mgonjwa huyo,
toa ruhusa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia.Onyo
Sitisha kuosha masikio Ikiwa mgonjwa huyo aTAPata maumivu ya sikio unapjaribu kuosha sikio!
Maelekezo
Tazama Video ya mtoa huduma akionyesha jinsi ya kuosha sikio la mgonjwa.
Swali
Ni mara ngapi unapaswa kurudia kuosha sikio?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni Mara tatu !
Rudia kuosha sikio hadi mara tatu.
Kazi
Washiriki wakiwa katika vikundi, wafanye mazoezi ya hatua za kuosha masikio:
1. Panga vizuri mfuko wenye vifaa vya kuosha sikio
2. Tayarisha maji na sindano
3. Kagua ndani ya sikio la mgonjwa kwa kutumia otoskopu
4. Weka sindano, sahani yenye umbo la figo na kitambaa.
Onyo
Usisukume maji kwenye sikio la mgonjwa Ikiwa halijaziba.