Skip to main content
Uwezo wa kusikia

Kutambulisha upimaji wa TAP wa afya ya masikio

Somo: 3 ya 5
Mada: 1 ya 5
 Imekamilika  kwa 0%

Maelekezo

Ikiwa bado hujafanya hivyo, pakua Fomu ya upimaji wa TAP Ear kwenye kichupo au dirisha jipya na uchapishe nakala.

Kama huduma yako inatumia fomu tofauti na hii, jadili jambo hili na msimamizi wako.

Upimaji wa afya ya masikio wa TAP Ear ni mchakato rahisi kujua kama mtoto au mtu mzima ana tatizo la masikio na/au anasikia kwa taabu.

Upimaji wa afya ya maskio wa TAP husaidia kutambua kama mhusika anaweza kuhitaji:

  • Kusafishwa au kuoshwa masikio
  • Kukagua Uwezo wa kusikia ili kuangalia kama wanaweza kufaidika na Bidhaa saidizi za kusikia ambazo zimejumuishwa kwenye TAP
  • Rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia kwa ajili ya kufanyiwa tathmini
  • Rufaa kwenda kupata bidhaa saidizi nyingine.

Tumia fomu ya TAP ya upimaji wa afya ya masikio ili:

  • Kukuongoza kupitia hatua za upimaji wa afya ya masikio
  • Kuweka rekodi ya matokeo ya upimaji
  • Pangilia mambo ya kufanya.

Maelekezo

Kila uonapo hii alama inamaana kuwa mtu huyo anaweza kuhitaji kupewa rufaa.

Nafasi na vifaa vinavyohitajika kupima

Ili kutekeleza upimaji wa afya ya masikio unahitaji nafasi ambayo:

  • Ina kiti cha mgonjwa na chako wewe unayefanya kipimo
  • Ina mahali pa kunawa mikono yako kabla na baada ya kukagua kila mtu.

Unahitaji:

  • Otoskopu na Spekulamu
  • Tishu kwa ajili ya kusafisha masikio kwa kuyafuta
  • Seti /Mfuko wa vifaa vya kuosha masikio
  • Fomu moja ya TAP kuhusu upimaji wa afya ya masikio kila mtu anayepimwa.

Mweleze mtu anayepimwa:

Utakagua kuangalia dalili za Matatizo ya sikio.

Wakati wa ukaguzi utaangalia:

  • Afya ya masikio yao
  • Kama wanahitaji kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia au
  • Kama Unaweza kuwasaidia kwa kuwapima Uwezo wa kusikia.

Maelekezo

Muulize:

  • Je, una maswali yoyote?
  • Je, unatoa ruhusa ya kufanyiwa upimaji wa masikio?

Kama ni kuhusu kupima watoto, omba ruhusa kutoka kwa mtoto na mzazi au mlezi wa mtoto huyo.

Taarifa kuhusu mtumiaji

Sehemu ya kwanza ya upimaji wa afya ya TAP Ear inahusisha kukusanya taarifa za Mawasiliano kuhusu mtu huyo Ikiwa ni pamoja na jina lake, jinsia, umri, simu na anwani.

Maelekezo

Anza kwa kukusanya taarifa za msingi kuhusu mtu anayepimwa.

Umri

Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wana mahitaji makubwa zaidi. Kwa ruhusa kutoka kwa mwanafamilia wao wape rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na kusikia.

Maelekezo

Kabla ya kupima wa afya ya masikio ni muhimu kujua namna ya:

  • Tumia otoskopu
  • Futa na osha masikio ya mhusika.

Utajifunza kuhusu stadi hizi Katika mada ya tatu na ya nne.

0%
Kutambulisha upimaji wa TAP wa afya ya masikio
Somo: 3 ya 5
Mada: 1 ya 5