Baada ya upimaji

Maendeleo ya usoMaji Mada:

Maelekezo

Katika mada hii utajifunza kuhusu shughuli zinazohitaji kukamilika baada ya siku ya upimaji.

Baada ya siku ya upimaji

Baada ya siku ya upimaji ,mpimaji na mratibu wa upimaji wa shule :

  • Atawataarifu wazazi/walezi kuhusu matokeo ya upimaji
  • Atawasiliana na wafanyakazi wanaopokea rufaa za wagonjwa ili kuwafahamisha ni watu wangapi watarajie kuwahudumia
  • Atafuatilia wafanyakazi ili kujua kama watoto waliopewa rufaa wamehudhuria
  • Ataweka mpango siku ya ufuatiliaji kwa watoto wowote ambao hawakuweza kupimwa

Maelekezo

Utajifunza zaidi kuhusu rufaa katika somo la tatu.

Ufuatiliaji na tathmini

Ni muhimu kuweka rekodi kamili na sahihi, kwani kumbukumbu hizi zitatumika kufuatilia na kutathmini jinsi programu inavyoendeshwa.

Utawekwa mfumo wa ndani wa ufuatiliaji na tathmini ambao utakusanya taarifa kwa njia ya siri.

Umekamilisha somo la pili!