Siku ya upimaji
Maelekezo
Katika mada hii utajifunza juu ya kile kinachopaswa kupangwa vizuri siku ya upimaji.
Maandalizi ya upimaji
Maandalizi ya upimaji ni pamoja na:
- Kuandaa eneo la kufanyia upimaji na vifaa vya upimaji
- Kuandaa nyaraka
- Kupanga mtiririko mzuri wa upimaji
- Kipindi cha maandalizi ya kikundi
Kuandaa eneo la kufanyia upimaji na vifaa vya upimaji
Nafasi ya kufanya upimaji inapaswa kusafishwa (kuondoa vumbi, uchafu, na taka) na kuandaliwa kwa ajili ya upimaji.
Vifaa vya upimaji vinapaswa kuwa safi na tayari kutumika.
Kuandaa nyaraka
Nyaraka ziinapaswa kuwa tayari. Kwa mfano:
- Fomu za ridhaa za watoto zilizotiwa saini
- Nakala za upimaji ambazo bado hazijatumika.
Kupanga mtiririko mzuri wa upimaji
Panga mtiririko rahisi kwa watoto kupita katika mchakato wa upimaji.
Msaidizi wa upimaji atawaelekeza watoto wakati wa upimaji.
Mtu mzima mwingine ('mtu mzima anayesimamia zoezi') yupo kwa kila upimaji. Hii ni kuhakikisha usalama wa mtoto unakuwepo na kuheshimiwa.
Msaidizi wa upimaji au mtu mzima anayesimamia huhakikisha kwamba watoto wanaosubiri kupimwa hawawezi kuona kinachoendelea kwenye chumba cha upimaji hadi zamu yao ya kuingia ifike.
Kipindi cha maandalizi ya kikundi
Panga kipindi cha kikundi kwa kuandaa watoto watakaopimwa.
Kuwatayarisha watoto katika kikundi na kutumia mbinu rafiki itasaidia:
- Kupunguza wasiwasi wowote kuhusu upimaji
- Kupunguza muda unaohitajika kuandaa kila mtoto
- Kufanya upimaji kuwa mzuri zaidi.
Shughuli za upimaji zinaweza kuelezewa kwa njia rahisi, ya kufurahisha na ya kucheza.
Onyesha vifaa vya kukagua kwa watoto ili wajue kitakachotokea wakati wa upimaji.
Swali
Tazama picha hii ya mpimaji kwa kutumia mbinu rafiki kwa mtoto wakati wa upimaji.
1. Ni ni kitu gani kinaifanya mbinu hii kuwa rafiki kwa watoto'?
- Kuketi kwa urefu cha mtoto
- Kutabasamu na kumtazama mtoto
- Kuruhusu mtoto kuona vifaa vya upimaji
2. Ni njia gani zingine za kumhakikishia mtoto usalama katika hali hii?
Njia nyingine za kumhakikishia mtoto usalama ni pamoja na:
- Kutumia sauti rafiki
- Kueleza mambo polepole na kuangalia kama mtoto ameelewa
- Kumwambia mtoto kuwa anafanya vizuri kwenye kipimo.
Mwishoni mwa siku ya upimaji
Hakikisha kuwa nyaraka zimekamilika ikiwa ni pamoja na:
- Daftari la mahudhurio
- Fomu za upimaji (kurekodi matokeo ya upimaji)
- Fuatilia Orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa (kurekodi watoto wanaohitaji huduma ya macho na/au masikio).
Unapaswa pia kusafisha eneo la upimaji pamoja na vifaa vya upimaji.
Dokezo
Ikiwa mtoto hayupo siku ya upimaji na idhini imetolewa, upimaji unapaswa kupangwa kwa siku nyingine. Hii inapaswa kufanyika shuleni au eneo lingine.
Maelekezo
Ikiwa bado hujafanya hivyo, chapisha Orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa . Unaweza pia kupata fomu hiyo katika katika Kitabu cha utekelezaji wa upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule .