Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Kusikia

Ufuatiliaji wa vifaa saidizi vya usikivu

Somo: la 5 kati ya masomo 6
Mada: 1 kati ya Mada 4
0% Imekamilika

Wakati wa kufuatilia

Inashauriwa kumfuatilia mgonjwa mapema katiya wiki mbili na miezi miwili ili kumsaidia mtumiaji kuzoea vifaa saidizi vyake vya Usikivu na kupata faida kubwa. Inapaendekezwa kupima wa mara nyingine kila baada ya miaka miwili kwa watu wazima.

Enelo la kufanya ufuatiliaji

ufuatiliaji waweza kufanyika:

  • Kwa mbali kupitia Mawasiliano ya simu au simu ya Video; au
  • Kwa kibinafsI - Mhusika kufika kwenye kituo

Ufuatiliaji unaofanyika kwa mgonjwa kufika kituoni

Kwa ujumla, uamuzi kuhusu namna ya kufanya ufuatiliaji wa mbali au wa mtu mwenyewe kufika kwenye kituo, unategemea kile kinachofaa zaidi kwa kulingana na hali ya mhusika. Hatahivyo, baadhi ya ufuatiliaji lazima mgonjwa awepo mwenyewe kituoni. Kwa mfano, miadi ya kutathmini kwa mara nyingine.

Kwa nini tunafanya ufuatiliji?

Ufuatiliaji wa vifaa saidizi vya usikivu utakusaidia kujua kama:

  • vifaa saidizi vya usikivu vinakidhi mahitaji ya mtumiaji
  • vifaa saidizi vya usikivu vinahitaji kurekebishwa au kubadilishwa
  • vifaa saidizi vya usikivu bado vinafaa vizuri
  • mtumiaji anahitaji utatuzi wa shida yoyote kwa matumizi salama na sahihi.

Swali

Matatizo ya vifaa saidizi vya usikivu yanaweza kusababishwa na:

Chagua majibu matatu sahihi.




Umepatia iwapo umechagua b, c na d, kama majibu sahihi!

Mfundishe mtumiaji jinsi ya kusafisha na kutumia vifaa saidizi vyake vya Usikivu kwa usahihi ili kuepuka Matatizo.

a Sio sahihi.

Kujisikia aibu kuhusu kuvaa vifaa saidizi vya usikivu hakusababishi tatizo la vifaa saidizi vya usikivu. Hata hivyo, itaathiri ni kiasi gani mtu ananufaika kwa kutumia vifaa saidizi vya usikivu. Daima eleza faida za kutumia vifaa saidizi vya usikivu.

Nini cha kuangalia wakati wa ufuatiliaji

Angalia Ikiwa vifaa saidizi vya usikivu vinakidhi mahitaji ya mtu

Uliza maswali ili kujua kama mtu huyo ananufaika na vifaa saidizi vyake vya Usikivu katika maisha yake ya kila siku.

Angalia hali ya kifaa saidizi cha Usikivu

Angalia kila kifaa saidizi cha Usikivu ili kuona kama kitu chochote ni chafu au kimeharibika.

Maelekezo

Soma ili upate maelezo zaidi kuhusu matengenezo na uRekebishaji wa vifaa saidizi vya usikivu.

Angalia kifaa saidizi cha Usikivu kinafaa

Angalia kila kifaa saidizi cha Usikivu :

  • Kinamfanya mvaaji kujisikia vizuri anaokiweka katika mfereji wa sikio lake
  • Kinakaa vizuri sehemu ya nyuma ya sikio la mtumiaji.

Tatua tatizo

Iwapo mtu huyo anapata shida yoyote na vifaa saidizi vyake vya Usikivu, angalia jedwali la Utatuzi wa matatizo ili kutafuta suluhu pamoja.

Weka mpango wa mambo ya kufuatilia

Tumia taarifa iliyokusanywa kuamua na mhusika kama:

  • Kumfundisha zaidi/kutatua Matatizo kunahitajika
  • vifaa vya kisasa vya Usikivu vinahitaji kurekebishwa au kubadilishwa
  • vifaa tofauti vya Usikivu vinahitajika Ikiwa ndio, je, vinaweza kupatikana ndani ya nchi au mhusika anapaswa kupata rufaa ?
  • Rufaa kwa mtaalamuu wa masikio na Usikivu inahitajika.

Weka miadi ya ufuatiliaji unaofuata.