Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Maono

Taarifa kuhusu mtoto

Somo: la 4 kati ya masomo 5
Mada: 1 kati ya Mada 4
0% Imekamilika

Fomu ya vipimo

Fomu ya upimaji itakusaidia kupima mishipa ya fahamu kwa kila mtoto na kuandaa mpango wa matibabu.

Maelekezo

Kama bado hujafanya hivyo, pakua fomu ya upimaji na uchapishe nakala.

Usiwe na wasiwasi kama hautaweza kupakua fomu. Maswali yaliyoko kwenye fomu yataonekana kadri unavyosoma sehemu hii ya moduli.

Anza kwa kurekodi:

  • Jina la mpimaji
  • Tarehe ya upimaji
  • Mahali ambapo upimaji utafanyika.

Kusanya taarifa

  • Msalimie mtoto na muulize jina na namba ya darasa lake
  • Tafuta fomu yao ya ridhaa.

Dokezo

Ikiwa mtoto hakuhudhuria kipindi cha maandalizi ya kikundi; mwelezee kile utakachokifanya.

Taarifa kuhusu mtoto

Sehemu ya kwanza ya fomu ya upimaji inahusu kukusanya taarifa zinazomhusu mtoto, mzazi/mlezi wake na idhini ya kushiriki upimaji.

Jaza sehemu ya kwanza ya fomu ya upimaji kwa kunakili habari zote kutoka kwenye fomu ya Idhini.

Taarifa kuhusu mtoto ni pamoja na jina lake, tarehe ya kuzaliwa, anwani, shule na darasa.

Maelezo ya mzazi/mlezi yanajumuisha jina, simu ya mawasiliano na/au barua pepe na lugha zinazozungumzwa.

Swali

Kwa nini ni muhimu kujua lugha zinazozungumzwa na mzazi/mlezi wa mtoto?

Ni muhimu kumjulisha mzazi/mlezi kuhusu matokeo ya upimaji wa usikivu na uoni za mtoto wao katika lugha yao ya mazungumzo.

Ridhaa

Hakiki iwapo mtoto ameruhusiwa na mzazi/mlezi wake kushiriki katika upimaji.

Endelea tu iwapo mzazi ameridhia

Maswali ya awali kabla ya kuanza upimaji

Maelekezo

  • Kagua maswali ya awali kabla ya upimaji
  • Nakiri taarifa kutoka kwenye fomu ya ridhaa.

Ikiwa maswali kabla ya upimaji hayajajibiwa endelea kupima uoni.

Miwani ya macho

Maelekezo

Uliza kama mtoto anavaa miwani.

Ikiwa jibu ni ndiyo, hii ina maana kwamba tayari wameonana na mtoa huduma ya afya ya macho.

Ikiwa jibu ni ndiyo na tatizo limebainishwa wakati wa upimaji toa rufaa kwa wafanyakazi wa huduma ya macho katika huduma ambayo mtoto tayari anatumia.

Maelekezo

Ikiwa mtoto anatumia miwani, uliza sababu ya kutumia miwani:

  • Kuona vitu vilivyo mbali.
  • Kuona vitu vilivyo karibu.

Swali

Je, ni lini unaweza kumwomba mtoto avae miwani yake wakati wa upimaji wa uoni wa mbali?

Chagua majibu mawili.




Uko sahihi Ikiwa umechagua a na c kama majibu sahihi!

Ni muhimu kuchunguza uoni wa mtoto akiwa amevaa miwani yake ya umbali ili kuhakikisha kuwa anafanya kazi vizuri.

Kuvaa miwani ambayo ni, au inaweza kutumika kwa matatizo ya uoni wa karibu, itasababisha matokeo yasiyo sahihi (ya uwongo) ya kipimo cha uoni wa mbali.

Kama mtoto:

  • Hana miwani ya kusomea endelea
  • Huvaa miwani ya kuona mbali kumwomba mtoto kuvaa miwani kwa ajili ya upimaji
  • Huvaa miwani ya kuona vitu vilivyo karibu au visivyojua kumwomba mtoto asivae miwani kwa upimaji.

vifaa saidizi vya usikivu

Maelekezo

Hakiki iwapo mtoto amevaa vifaa saidizi vya usikivu.

  • Ikiwa jibu ni hapana; endelea
  • Ikiwa jibu ni ndiyo na tatizo litatambuliwa wakati wa upimaji toa rufaa kwa mtoa huduma ya ya masikio katika huduma ambayo mtoto tayari anatumia.

Kisukari na afya ya macho

Maelekezo

Uliza iwapo mtoto ana ugonjwa wa kisukari au mzazi/mlezi ana wasiwasi kuhusu maumivu/usumbufu/kuwashwa sana kwenye macho/macho ya mtoto wao.

  • Ikiwa jibu ni "hapana" kwa ,maswali yote mawili;  endelea
  • Kama jibu ni "ndiyo" kwa swali mojawapo  toa rufaa kwa mtoa huduma ya afya macho. Mtoto anahitaji kufanyiwa tathmini na mtoa huduma mwenye stadi na ujuzi zaidi.

Wasiwasi kuhusu uoni au Usikivu

Maelekezo

Hakiki kama mzazi/mlezi ana matatizo.

  • Ikiwa mzazi/mlezi hana wasiwasi wowote kuhusu uoni au Usikivu kwa mtoto Endelea
  • Ikiwa mzazi/mlezi ana wasiwasi kuhusu Usikivu au kuona Endelea na upimaji na upange ufuatiliaji.

Swali

Kutana na Do Yoon

Wazazi wa Do Yoon walitiki ndiyo kwa kwenye sehemu inayonyesha wasiwasi kuhusu uoni wa Do Yoon.

Hakuna matatizo yoyote yaliyogundulika baada ya vipimo.

Je, wewe ungempa Do Yoon rufaa kwa mtoa huduma ya afya ya macho?


Jibu sahihi ni hapana!

Ungetoa rufaa kwa Do Yoon kama ungegundua matatizo wakati wa upimaji wa uoni na/au upimaji wa afya ya macho.

Ni muhimu kusikiliza wasiwasi wa wazazi wa Do Yoon. Weka miadi ya upimaji wa ufuatiliaji shuleni au kwenye kliniki iliyoko kwenye jamii ndani ya mwezi mmoja.