Skip to main content
Mtoto ameketi kwenye kiti. Mkono mmoja unaelekeza herufi kwenye chati inayoelekeza na mkono mwingine unafunika jicho moja.
0% Complete
uoni

uoni na afya ya macho kwa watoto

Moduli hii inatoa utangulizi wa uoni, Matatizo ya kuona na afya ya macho na jinsi ya kutekeleza uoni na upimaji wa Afya ya macho kwa watoto.

Muda wa Moduli: Masaa 2 na dakika 30 mtandaoni, yakifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa mkufunzi/mshauri pale inapohitajika

Kabla ya kuanza, Hakikisha kuwa umekamilisha Moduli hii:

Rasilimali ambazo utahitaji wakati wa upimaji

  • Utepe wa kupimia (wenye urefu wa walau mita tatu)
  • Chati ya upimaji wa uoni (chati ya HOTV na kadi ya kuelekeza na chati E)
  • Kiziba jicho (si lazima)
  • Mkanda
  • Kiti
  • Vifaa vya kunawia mikono au kitakasa mikono

Maelekezo ya uchapishaji wa chati za uoni:

  • Chapisha chati ya ukubwa kamili. Chagua chapisha Ukubwa halisi. Usipunguze saizi ya nyaraka ili iweze kutosha kwenye karatasi
  • Chapisha kwenye kadi nyeupe ya A4 ambayo ni nene na imara
  • Hakikisha herufi zimechapishwa kwa rangi nyeusi ili kuzifanya zisomeke vizuri
  • Kama picha iliyochapishwa hainekani vizuri, au ina rangi ya kijivu, usiitumie
  • Ili kuangalia kama umechapisha chati kwa ukubwa sahihi, pima ukurasa kwa kutumia rula ya 10 cm ili kuthibitisha ukubwa wake.

Bonyeza kwenye linki hapa chini kupakua na kuchapa:

Nembo ya Raslimali Rasilimali

Bofya kwenye yafuatayo ili uweze kupakua na kuchapa taarifa zifuatazo: