Maelekezo
Rekodi mpango sehemu ya chini ya fomu ya upimaji.
Rekodi mpango
Baada ya kukamilisha upimaji wa uwezo wa kusikia na kuona , rekodi mpango.
Hakuhudhuria
Ikiwa mtoto hayupo siku ya kufanyiwa vipimo, kamilisha sehemu ya 'hakuhudhuria' ya mpango na uweke alama kwenye kupanga upimaji siku za usoni.
Mratibu wa upimaji atakubaliana na mpango na shule wa kupanga upya upimaji wa watoto ambao hawako shuleni.
Amefaulu vipimo vyote
Ikiwa mtoto amefaulu :
- Upimaji wa kuona
- Upimaji wa Afya ya macho
- Upimaji wa kusikia
- Upimaji wa Afya ya masikio.
Chagua kuwa amefaulu vipimo vyote vilivyo katika sehemu ya mpango. Jaza fomu ya kutoa taarifa.
Mzazi/mlezi ana dukuduku
Ikiwa mtoto ana matokeo ya ufaulu na mzazi/mlezi wake alikuwa na wasiwasi kuhusu uoni na Uwezo wa kusikia wa mtoto wakati akijibu maswali awali kabla ya upimaji;
- Jadili matokeo na mzazi/mlezi
- Eleza kwamba mtoto wao alipitisha uoni na upimaji wa kusikia na utoe upimaji wa kufuatilia ndani ya mwezi mmoja
- Jaza fomu ya kutoa taarifa.
matokeo yanayoashiria kutoa rufaa kama
Ikiwa mtoto ana
matokeo yanayoashiria kutoa rufaa yoyote kati ya yafuatayo:- maswali awali kabla ya kuanza upimaji
- Upimaji wa kuona
- Upimaji wa Afya ya macho
- Upimaji wa kusikia
- Upimaji wa Afya ya masikio.
Jadili na wazazi/walezi umuhimu wa kupata rufaa .
Jaza fomu ya kutoa taarifa.
Maelekezo
Ikiwa mtoto ana ufaulu au matokeo yanayoashiria kupewa rufaa, wazazi wao wanapaswa kufahamishwa kuhusu matokeo kwa kujaza fomu ya kutoa taarifa .
Mtoto tayari anatumia miwani au vifaa saidizi vya kusikia
Ikiwa mtoto ambaye tayari ana miwani au vifaa saidizi vya kusikia ana
Matokeo yakupewa rufaa muombe mzazi/mlezi kumpeleka mtoto kwa mtoa huduma wake aliyepo.Orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa
Mratibu wa shule anaweka kumbukumbu ya maelezo ya mtoto yeyote ambaye ana
rejea matokeo katika orodha ya ufuatiliaji wa rufaa na mshirikishe mratibu wa upimaji.