Baada ya kumaliza maswali upimaji, unahitaji:
- Kujua kama mtu huyo ana mahitaji mengine ya bidhaa saidizi
- Kuweka mpango na mgonjwa kuhusu hatua zinazofuata.
Bidhaa saidizi nyingine
mtu anaweza kufaidika na usaidizi katika maeneo mengine.
Maelekezo
Uliza: Je! una shida na:
- uoni
- Uwezo wa kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine
- Kujitunza
- Mawasiliano
- Utambuzi (kufikiri/kuKumbuka).
Ikiwa mtu huyo atakuambia ana Matatizo katika mojawapo ya maeneo yaliyotajwa hapo juu, eleza kwamba ungependa kuuliza maswali ili kupata taarifa zaidi.
Weka Mpango
Maelekezo
Rekodi mpango sehemu ya chini ya fomu ya upimaji.
Upimaji
Amua Ikiwa mtu huyo ana shida katika maeneo mengine na Ikiwa angefaidika na upimaji kwa ajili ya kupewa bidhaa saidizi nyingine zinazoweza kumsaidia
Maelekezo
Tumia vifaa vya upimaji na/au maswali kutoka kwa Moduli nyingine zilizotangulia za TAP ili kukusaidia.
UnamKumbuka Malicka?
Malika ana umri wa miaka 70. Ni bibi ambaye anaishi na familia yake.
Wakati wa upimaji wa afya ya masikio; Unamuuliza Malika kama ana Matatizo yoyote katika maeneo mengine. Anaeleza kuwa ana shida ya Kusoma na kushona. Hawezi kuona vizuri kuweza kushona kama ilivyokuwa awali.
Unauliza maswali zaidi na kwa pamoja mnakubali kukamilisha upimaji wa uoni ili kuona kama Bidhaa saidizi za uoni au rufaa kwa huduma zingine zinaweza kusaidia.
Tathmini
Ikiwa masikio ya mtu yote yana afya nzuri, kwa pamoja weka utaratibu kuendelea na kipimo cha kusikia.
Swali
UnamKumbuka John?
Angalia sehemu ya ukaguzi wa afya ya masikio iliyokamilishwa ya fomu ya upimaji wa Afya ya masikio ya John.
Je, ungepanga kufanya kipimo chaa kusikia kwa John?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
masikio ya John yalipoangaliwa yalionekana kuwa na afya njema pande zote mbili. Pia walikuwa na afya kwa ndani walipotazamwa kupitia Otoskopu. Unaweza kuendelea na kipimo cha Uwezo wa kusikia kwa John.
Toa rufaa
majibu ya mgonjwa kwa maswali upimaji atakayoulizwa yatasaidia kuamua kama rufaa itamsaidia.
Ni muhimu kujua wakati wa kutoa rufaa kwa mgonjwa na mahali pa kwenda kupata rufaa.
- Baadhi ya watu wanaweza kuhitaji matibabu kwa tatizo la afya ya masikio au huduma maalumu zaidi kuliko ile ambayo Unaweza kutuitoa. Wape rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.
- Ikiwa mtu tayari amepewa kifaa saidizi cha kusikia; atafaidika pia kwa kupewa rufaa kwenda kuonana na mtoa huduma anayepatikana. Mpe rufaa kwenda kwenye huduma ya vifaa saidizi vya kusikia.
- mtu anaweza kuwa na mahitaji mengine na kufaidika na rufaa kwenda kwenye aina nyingine ya huduma. Weka kumbukumbu hii kwenye fomu.
Rufaa zinapaswa kujadiliwa kila wakati na kukubaliana na mgonjwa.
Swali
Angalia maswali upimaji na usome kuhusu watuwalioelezewa hapa chini. Nani anafaa kupewa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia?
1. Ari ana umri wa miaka 4. Ameenda kuhudhuria upimaji wa afya ya masikio akiambatana na mama yake.
Je, Ari anapaswa kupata rufaa?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
Mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 5 anapaswa kupaewa rufaa kwenda kufanyiwa tathmini na mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.
2. Jae ni mvulana wa shule mwenye umri wa miaka 7 anayehudhuria upimaji wa afya ya masikio akiwa ameaambatana na baba yake. Alitokwa na usaha sikioni mara tatu kwa mwaka uliopita.
Je, Jae anapaswa kupewa rufaa?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
Jae ana umri zaidi ya miaka 5. Hata hivyo, anapata anatokwa na uchafu mara kwa mara kutoka mojawapo ya masikio yake na anapaswa kuwa
kupewa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.3. Ahmad ana umri wa miaka 25 na anahudhuria upimaji wa afya ya masikio akiwa ameambatana na mlezi wake. Hawezi kuzungumza ili kuwasiliana.
Je, Ahmad anapaswa kupata rufaa?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
Ahmad hawezi kuongea ili kuwasiliana. Ana mahitaji makubwa zaidi na anapaswa kupewa rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia.
4. Farah ni mzee mwenye umri wa miaka 65.Anasema kuwa amegundua kuwa ana Matatizo ya kusikia maongezi. Hana usaha wala hatokwi na maji maji masikioni mwake.
Je, Farah anapaswa kupata rufaa?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni hapana!
Farah anaweza kuendelea na upimaji wa Afya ya masikio pamoja na mfanyakazi wake wa afya.
Ufuatiliaji
Rudia upimaji wa Afya ya masikio
- Ikiwa mtu huyo amepewa rufaa ya kwenda kupata matibabu kwa tatizo la Afya ya masikio, weka kweka kumbukumbu ya kurudia upimaji wa afya ya masikio baada ya kukamilisha matibabu yake.
- Ikiwa sikio la mgonjwa lina afya bora, endelea kupanga siku ya kufanya kipimo cha kusikia.
- Ikiwa sikio la mgonjwa halina afya bora baada ya matibabu, mpe mgonjwa rufaa kwenda kwa mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.
Swali
UnamKumbuka Patryk?
Patryk ana umri wa miaka 6 na amekuwa na shida ya kusikia wakati akiwa shuleni.
Amekuja kupima afya ya masikio akiwa ameambatana na baba yake. Anaweza kujibu maswali. ya upimaji. Baba yake amethibitisha kuwa amekuwa na maambukizi ya masikio ya mara kwa mara pamoja na kutokwa na uchafu.
Je, ungependa kuendelea na upimaji wa afya ya masikio ya Patryk?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni hapana!
Unapaswa kusimamisha upimaji. Mweleze Patryk na baba yake kwamba kwa vile Patryk amekuwa na maambukizi ya mara kwa mara ya masikio, anapaswa kupelekwa kwa mtaalamu wa masikio na kusikia.