Mweleze mtu huyo kwamba utauliza maswali kadhaa. majibu yake atakayotoa yatakusaidia kwenye kutengeneza mpango.
Shirikisha wanafamilia au walezi pale panapofaa.
Vifaa saidizi vya kusikia
Maelekezo
Uliza: Je, kwa sasa unatumia bidhaa saidizi za kusikia ambazo ulipewa ulipoenda kwenye huduma ya kusikia?
Kama mtumiaji tayari anatumia bidhaa saidizi za kusikia, mpima afya ya masikio. Kisha:
- Weka kumbukumbu ya aina ya bidhaa saidizi za kusikia wanazotumia
- Angalia kama wanapata Matatizo yoyote wanapotumia bidhaa zao.
Kama mtu ana Matatizo katika kutumia bidhaa saidizi yake ya kusikia, kwa ruhusa yake,
mpe rufaa kwenda kuonana na mtoa huduma katika eneo alipopata bidhaa hiyo.Swali
Kutana na Kaleisha
Kaleisha ana umri wa miaka 79 na anatembelea familia yake. Ana matatizo wakati wa kutumia vifaa saidizi vyake vya kusikia.
Kaleisha ameacha kuvaa vifaa saidizi vyake vya kusikia na ana matatizo ya kusikia. Anapata ugumu wa kujiunga na mazungumzo ya familia.
Kaleisha ametembelea kituo cha afya. Mhudumu wa afya amempima afya ya masikio. masikio yake yana afya bora.
Je, ungependekeza hatua gani baadaye?
Chagua jibu moja.
Uko sahihi kama umechagua " b" kama Jibu sahihi
Ni muhimu kumrejesha Kaleisha kwenye huduma ambayo ilitoa vifaa saidizi kusikia ikiwezekana. Huduma inaweza kurekebisha vifaa saidizi vya kusikia na kutoa vipuri ikihitajika.
Lugha inayozungumzwa
Maelekezo
Uliza: Je, una shida kufanya mazungumzo wakati wa kuwasiliana?
Baadhi ya watu wazima na watoto wanapata shida kungumza kama njia ya kuwasiliana.
mtu ambaye hawezi kufanya mazungumzo kama njia yao ya kawaida ya kuwasiliana ana mahitaji makubwa zaidi.
Mpe rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia.Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu watu wanaopata shida katika Mawasiliano katika Moduli ya bidhaa saidizi za Mawasiliano za TAP.
Mabadiliko ya ghafla katika uwezo wa kusikia
Maelekezo
Uliza: Je, katika miezi 3 iliyopita umekuwa na Mabadiliko ya ghafla kuhusu Uwezo wako wa kusikia?
Kwa kawaida mtu hupoteza Uwezo wa kusikia taratibu baada ya muda mrefu.
Onyo
Ikiwa mtu aTAPata Mabadiliko ya kusikia kwa ghafla ndani ya muda mfupi (kama miezi mitatu iliyopita), inaweza kuashiria tatizo kubwa la afya.
Mpe rufaa mara moja kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na kusikia .Kutokwa na uchafu kwenye masikio mara kwa mara
Maelekezo
Uliza: Je, kuna uchafu (majimaji)hutoka kwenye sikio/masikio yakomara kwa mara?
Kama mtu anatokwa na uchafu kwenye masikio yake mara kwa mara , inaweza kuwa ishara ya maambukizi ya sikio yanayojirudia.
Uchafu unaotoka waweza kuwa na rangi isiyo ya kawaida. Uchafu huu Unaweza pia kutoa harufu.
Maambukizi ya masikio ya mara kwa mara yanaweza kuharibu masikio na Uwezo wa kusikia kwa mhusika. Kwa idhini yao
toa rufaa kwenda kumuona mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia kwa ajili ya kufanyiwa tathmini.UnamKumbuka Garret?
Garret ana umri wa miaka 9 na anaishi katika kijiji cha wavuvi. Anapenda kuongelea pamoja na marafiki zake. Garret alipata maumivu kwenye sikio na anatokwa na uchafu mara kwa mara.
Swali
Je, mtu anayepata maambukizi ya mara kwa mara ya masikio anapaswa kupata rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia?
Chagua jibu moja.
Jibu sahihi ni "Ndiyo"!
mtu anayepata maambukizi ya masikio mara kwa mara na anatokwa na uchafu anapaswa kupelekwa kwenda kuonana na mtaalamu wa masikio na Uwezo wa kusikia.
Majadiliano
Je , ni wataalamu gani wa masikio na Uwezo wa kusikia wanaopatikana katika eneo unaloishi Unaweza kutoa rufaa kwa wahitaji kwenda kuonana nao?
Je! unajua jinsi ya kutoa rufaa kwenda kupata huduma hizi?