Kutoa na kufuatilia rufaa
Maelekezo
Katika mada hii utajifunza kuhusu rufaa na kwa nini ni muhimu kufuatilia rufaa zilizotolewa.
Kuwasiliana na wazazi/walezi
Iwapo mtoto anahitaji kupewa rufaa kwenda kuonana na wataalam wa huduma ya macho na/au sikio; uongozi wa shule utaweleza wazazi/walezi kuhusu uamuzi huu.
Wazazi/walezi hupewa taarifa kuhusu mahali pa kumpeleka mtoto wao kwa kutumia fomu ya kutoa taarifa.
Maelekezo
Ikiwa bado hujafanya hivyo, chapisha fomu ya kutoa taarifa .
Unaweza pia kupata fomu hiyo katika Kitabu cha utekelezaji wa upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule .
Kwa nini kufuatilia rufaa ni muhimu?
Madhumuni kuu ya programu ya upimaji ni kutambua watoto wanaohitaji rufaa kwenda kuonana na wataalam wa huduma ya macho na/au masikio.
Hata hivyo, yawezekana watoto wasipelekwe kwenye huduma waliyoelekezwa kwa mujibu wa rufaa. Kama hili litatokea, basi programu itakuwa haijafanikiwa.
Kwa bahati mbaya yawezekana matokeo kuwa makubwa.
Ni muhimu :
- Kufuatilia mahudhurio kwenye miadi inayofuatia baada ya upimaji
- Kuwasiliana na wazazi/walezi ili kuwatia moyo na kuwasaidia kutafuta njia za kuwapeleka watoto wao kwenye miadi ya rufaa.
Orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa
Orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa husaidia mpimaji na shule kufuatilia watoto ambao wamepewa rufaa.
- Tumia orodha ya mambo ya kuzingatia wakati wa rufaa ili kufuatilia kama watoto ambao wamepewa rufaa wameonana na mtaalamu wa masikio au macho
- Ikiwa watoto hawajahudhuria miadi, mratibu wa upimaji wa watoto shuleni anaweza kukutana au kuzungumza na wazazi/walezi ili kuelewa sababu zilizowafanya kutokuhudhuria.
Unamkumbuka Jabari?
Jabari (mratibu wa upimaji shuleni) alipokea ujumbe kuhusu mtoto ambaye hakurudi hospitali baada ya kupimwa kwa mara ya kwanza.
Jabari anawasiliana familia ya mtoto husika kwa njia ya simu. Wakati akiongea nao; anagundua kuwa wana wasiwasi kuhusu namna watakavyoomba ruhusa ya kutokwenda kazini. Jabari anawahakikishia kuwa huduma ya macho ambayo wamepewa rufaa kwenda kuipata, inapatikana pia wakati wa jioni.