Upimaji wa hisia za kusikia na kuona
Maelekezo
Katika mada hii utajifunza juu ya Upimaji wa hisia za kusikia na kuona.
Upimaji wa hisia za kusikia na kuona ni nini?
Upimaji wa hisia za kusikia na kuona unahusisha vipimo rahisi na ukaguzi ili kuona kama mtoto anaweza kuwa na:
- Tatizo la uoni na/au uwezo wa kusikia
- Tatizo la afya ya macho au sikio.
Upimaji hauthibitishi uwepo wa maradhi au ugonjwa.
Upimaji hubainisha kuwa mtoto anahitaji kupewa rufaa kwenda kuonana na mtoa huduma ya afya ya macho na/au sikio ili kufanyiwa upimaji zaidi.
Dokezo
Watoto wote wanapaswa kushiriki kwenye upimaji wa hisia za kusikia na kuona. Zoezi hili inajumuisha watoto wenye ulemavu (kimwili, kujifunza na/au hisia).
Kutana na Ju
Walimu wa Ju walikuwa na wasiwasi kwamba hakuwa na uwezo wa kuona vizuri shuleni. Upimaji wa hisia za kusikia na kuona ulionyesha kuwa alihitaji rufaa kwenda kuonana na mtaalam ya huduma ya macho. Baada ya kufanyiwa tathmini, alishauriwa kuvaa miwani.
Upimaji unasaidia nini?
Upimaji unaweza kusaidia:
- Kutambua matatizo ya uoni pamoja na Matatizo ya kusikia mapema katika maisha ya mtoto
- kupata rufaa haraka kwenda kwenye huduma nyingine , ili kuzuia uharibifu zaidi wa uoni na uwezo wa kusikia
- Kuepuka au kupunguza athari mbaya kwa kusababisha matatizo ya hisia za uoni na uwezo wa kusikia kwenye maisha ya mhusika.
Kutana na Manuel
Manuel alikuwa na maambukizi ya macho alipokuwa mtoto; matatizo haya yalidumu kwa miezi kadhaa. Ugonjwa huo hatimaye ulitambuliwa na kutibiwa na mtaalamu wa afya. Kuchelewa huko kulisababisha uharibifu wa macho yake na kuathiri uwezo wake wa kuona vizuri.
Mpango wa upimaji wa shule ungeweza kutambua maambukizi mapema na kuzuia matatizo yake ya kuona.
Upimaji hufanyika mara ngapi?
Watoto wanapaswa kufanyiwa upimaji wa hisia za kusikia na kuona:
- Wakati wanapojiunga na shule
- Urudiwe kila mwaka 1 hadi miaka 2.
Kutana na Anju
Anju alipimwa hisia za kusikia na kuona alipoanza shule.
Kabla ya hapo, alikuwa na maambukizi ya mara kwa mara ya masikio ambayo yaliathiri uwezo wake wa kusikia kile ambacho mwalimu alikuwa akisema shuleni.
Mpimaji aliona dalili za maambukizi ya sikio na kumpa rufaa kwenda kuonana na mtaalam wa huduma ya sikio aliyekoeneo ambalo Anju anaishi.
Baada ya matibabu Anju hana maambukizi ya sikio tena. Anaendelea vizuri shuleni.
Anju ni mfano wa mtoto ambaye alinufaika na upimaji wa hisia za uoni na kusikia na rufaa ili kuzuia upotevu wa kusikia.
Ni mambo gani yako kwenye upimaji wa hisia za kusikia na kuona?
Upimaji wa Uoni na uwezo wa kusikia hufuata mchakato wa hatua kwa hatua.
Hii ni pamoja na:
- Kupata ridhaa na taarifa za msingi kutoka kwa wazazi/walezi kuhusu afya ya mtoto, Uoni na uwezo wake wa kusikia
- Kufanya upimaji:
- Kupima uwezo wa kuona na kusikia
- Kukagua afya ya macho na masikio
- Kutoa rufaa kwa watoto kwenda kuonana na mtaalam wa afya ya macho na masikio kama itahitajika.

Mchakato wa upimaji- chati inayoonyesha mtiririko wa hatua

Mchakato wa upimaji- chati inayoonyesha mtiririko wa hatua
Zana zinazotumiwa katika Upimaji wa hisia za kusikia na kuona
Mtu anayefanya upimaji ('Mpimaji') atatumia:
- Chati za Uoni za kupima Uoni
- Tochi ya kukagua macho
- Kipimo cha kiwango cha sauti ili kuangalia viwango vya kelele za chinichini
- Kipima sauti cha kupima uwezo kusikia
- Otoskopu cha kusaidia kukagua ndani ya masikio.

Chati ya Uoni (HOTV)

Kipima sauti

Otoskopu
Vipimo vya sauti
Aina ya kipima sauti kitakachotumika itategemea na kipima sauti kinachopatikana katika eneo husika na kama kuna umeme wa kutosha au huduma ya intaneti.

Mashine ya kupima sauti

Programu ya kipima sauti iliyoko kwenye simu janja
Mita za kupima kiwango cha sauti
Kipimo cha kiwango cha sauti kinatumika kupima kama kiwango cha kelele za chinichini ni ndogo ili upimaji wa uwezo wa kusikia uweze kufanyika
Dokezo
Mita ya kupima kiwango cha sauti inaweza kununuliwa au programu ya simu inaweza kupakuliwa kwenye simu ya mkononi: kwa mfano programu ya hearWHO.
Fomu ya vipimo
Matokeo ya Upimaji wa hisia za kusikia na kuona hurekodiwa kwenye fomu ya vipimo.
Mtoto anapaswa kupewa rufaa kwenda kumuona mtaalam wa huduma ya macho na/au sikio iwapo upimaji utaainisha tatizo linaloweza kutokana na:
- Uoni na/au afya ya macho
- Uwezo wa kusikia na/au afya ya masikio.
Maelekezo
Ikiwa bado hujafanya hivyo, chapisha fomu ya upimaji . Unaweza pia kupata fomu hiyo katika Kitabu cha utekelezaji wa upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wa umri wa kwenda shule .
Kwanini Upimaji wa Uoni na uwezo wa kusikia vinafanyika pamoja?
Upimaji wa Uoni na kusikia wakati mwingine hufanyika tofauti. Hatahivyo, upimaji wa pamoja ni bora zaidi.
Upimaji wa pamoja unaweza:
- Kuainisha matatizo ya kuona na/au kusikia mapema katika maisha ya mtoto
- Kupunguza gharama na wakati.