Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Maono

vifaa saidizi vya uoni ambazo husaidia mtu kusogea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine

Somo: la 2 kati ya masomo 4
Mada: 3 kati ya Mada 3
0% Imekamilika

Fimbo nyeupe humsaidia mtu mwenye uoni hafifu, au asiye na uoni, kuweza kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Fimbo nyeupe humpa mtumiaji taarifa kuhusu mazingira anayopitia.

Fimbo mbili nyeupe, moja imenyooka na nyingine imekunjwa

Kutana na Michael

Michael anatumia fimbo nyeupe kwenda na kutoka shuleni, pamoja na kutoka eneo moja hadi eneo lingine darasani kwake na kwenye uwanja wa michezo.

Fimbo yake nyeupe pia ni njia nzuri kwa watu wanaomzunguka kujua kwamba hana Uwezo wa kuona.

Michael alikuwa na mtoa Msaada akimfundisha namna ya kutumia fimbo yake nyeupe. Walifanya mazoezi ya pamoja nyumbani, darasani na kwenye uwanja wa michezo. Alipokuwa na uhakika  kuwa anaweza kufanya hayo yote bila ya Msaada; walifanya mazoezi ya kutembea kwenda na kutoka shuleni. Sasa anaweza kufanya hivyo peke yake au na marafiki zake.

Majadiliano

Ni vifaa gani saidizi vya uoni vinazopatikana katika eneo lako unaloishi?

Umekamilisha somo la pili!