Skip to main content
 Imekamilika kwa 0%
Usikivu

Vifaa saidizi vya kusikia vinavyoweza kusetiwa

Moduli hii inajengwa juu ya moduli ya vifaa vya saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari na TAP na inajumuisha maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kutoa vifaa saidizi vya kusikia kwa watoto. Inafundisha huduma ya afya ya msingi na wafanyakazi wa jamii kutoa vifaa saidizi vya kusikia inayoweza kupangwa kufuatia hatua nne za huduma.

Muda wa Moduli: Masaa 2 mtandaoni, yakifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa mwezeshaji/mshauri.

Usaidizi wa vifaa saidizi vya kusikia kwa watoto mara nyingi unahitajika zaidi ikilinganishwa na watu wazima. Inahitaji kiwango cha juu cha mafunzo.

Kabla ya kuanza kusoma moduli hii, hakikisha kuwa umekamilisha Moduli zifuatazo:

Rasilimali ambazo utahitaji wakati wa upimaji

Kipimo cha kusikia:

  • Vipima sauti na spika za masikioni zinazochuja kelele
  • Chumba chenye utulivu
  • Uteuzi wa visaidizi vya usikivu vinavyoweza kusetiwa, ikijumuisha saizi tofauti za viunzi vya masikio na betri za vipuri
  • Midoli ya kuchezea vya kuhimiza watoto wadogo kushiriki au vibandiko vya kukamilisha mtihani

Ufungaji wa vifaa saidizi vya kusikia:

  • Vifaa saidizi vya kusikia katika ukubwa tofauti
  • Bomba la ziada la kutumia kwenye kifaa saidizi cha kusikia
  • Mikasi
  • Kalamu

Aina sita za sauti tofauti ambazo anapaswa kusikia ili kujua lugha

  • Kadi ya kuashiria sauti ya Lingi
  • Kadi (sentimita 20 x 20 sentimita) ya kufunika mdomo wa anayejaribu wakati wa jaribio la sauti za Lingii

Ukaguzi/utunzaji wa vifaa saidizi vya kusikia:

  • Bomba la kutumia kusikiliza (Stetoklipu)
  • Seti ya kusafishia Ikiwa ni pamoja na brashi, waya, kitambaa, chombo cha maji ya sabuni, kitambaa cha karatasi
  • Hifadhi ya kifaa saidizi cha kusikia (chombo cha kuondoa unyevu)

Bonyeza kwenye linki iliyo hapa chini ili kuweza kupakua na kuchapa:

Nembo ya Raslimali Rasilimali

Bofya kwenye yafuatayo ili uweze kupakua na kuchapa taarifa zifuatazo: