Fundisha

viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa vinapaswa kutumika kwa usahihi. Matumizi sahihi Yanazuia:
- Jeraha jingine
- Uharibifu wa ngozi yao ndani ya kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa.
Wakati muafaka wa kuvaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa

Mpango wa mhitaji utabainisha utaratibu wa kuvaa, Ikiwa ni pamoja na viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa.
Kila mara

kama daktari ameshauri kutokuvua kiatu kigumu saidizi, kiatu hiki hakipaswi kuvuliwa Wakati wowote bila kuzungumza kwanza na daktari . Eleza yafuatayo kwa mtumiajimiaji wa kiatu hiki.
Kuvua kiatu Wakati wa: kulala na / au kuoga

Ikiwa daktari amesema kuwa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kinaweza kuvuliwa Wakati wa kuoga au kwenda kulala, mtumiaji anaweza kuvua kiatu chake akitaka kufanya shughuli hizo.
Mweleze mtu anayepimwa:
- Daima kukaa chini kabla ya kuvua kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa
- Usisimame wala kutembea bila ya kuvaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa
- kama ukivua kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kabla ya kulala, kitunze pembeni mwa kitanda chako.

UnamKumbuka Jess?
rufaa ya Jess ilisema anaweza kuvua kiatu kigumu saidizi wakati anapooga.
Ana kiti chake cha bafuni ambacho anaweza kukalia. Hii inamaanisha kuwa hana haja ya kusimama bila ya kuvaa kiatu kigumu saidizi wakati anapooga.
Utumiaji na utunzaji wa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa.

Kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kitadumu na kitakuwa salama kama kimetunzwa vizuri.
Wafundishe watumiaji kuhusu kutunza kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa ikiwemo:
- Futa nje ya kiatu kwa kutumia kitambaa chenye unyevunyevu
- Kuvaa soksi wakati mtumiaji anapovaa kiatu hupunguza ulazima wa kukiosha kama inawezekana kuvua kiatu hicho.
Namna ya kuvaa kiatu kigumu saidizi
Mfundishe mtu namna ya kuvaa kiatu kigumu saidizi kwa kufuata hatua Tatu.
1. Tayarisha
- Kila mara angalia ndani ya kiatu kigumu kama kuna vitu vyovyote kabla ya kukivaa.
- angalia sehemu ya kutembelea ya mguu wako na sehemu ya juu ya mguu kama kuna alama yoyote mpya au ngozi iliyoharibiwa
- Vaa soksi safi ndefu. kama mtoa rufaa amesema kuwa Unaweza kuvua kiatu kigumu saidizi, badilisha soksi kila siku.
2. Vaa
- Kaa chini huku ukiwa umekunja goti
- Weka mguu ndani ya kiatu kigumu huku ukiweka kisigino chini kwenye kitambaa.
- funga kitambaa kuzunguka mguu na Hakikisha hakuna mikunjo
- Fanya kamba za kiatu katika mpangilio sahihi:
- Kifundo cha mguu
- Mguu
- Msuli nyuma ya muundi.
3. angalia kama mvaaji wa kiatu anajisikia vizuri kwa kuvaa kiatu
Kamba za viatu vinapaswa kufungwa vizuri na ziwe imara lakini zisisababishe Maumivu yoyote.
Tazama Video ili uone namna Unaweza kuvaa mwenyewe viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa
Swali
Je, kauli hizi ni za kweli au sio za kweli?
1. Wakati mtu anapovaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa, anapaswa kutoa sehemu ya ndani ya kiatu habaricho.
Umekosea, iwapo umechagua Sio kweli kama ndio Jibu sahihi
Sehemu ya ndani ya kiatu inapaswa kutokuondolewa.
2. Wakati wa kuvaa kiatu kigumu saidizi mtumiaji wa kiatu kigumu saidizi anapaswa kuanza kufunga kamba za mguuni kwanza.
Umekosea, iwapo umechagua Sio kweli kama ndio Jibu sahihi
Kamba za kufungia kiatu kwenye kifundo zinapaswa kufungwa kwanza kabla ya kufunga kamba nyingine.
Namna ya kuvua kaitu kigumu saidizi
Muonyeshe mtumiaji mtarajiwa wa kiatu kigumu saidizi namna ya:
- Fungua sehemu zote za kufungia viatu
- Kunjua sehemu ya ndani
- Toa mguu kwa uangalifu kutoka kwenye kiatu kigumu saidizi taratibu kadri inavyowezekana.
Mfundishe mtumiaji wa kiatu kwamba asiondoe kitambaa cha ndani ya kiatu kigumu saidizi.
Tazama Video ili uone namna unavyoweza kuvua kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa
kufunga vizuri kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa

Elezea:
kama kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kinalegea au kinabana, funga vizuri kamba ili kiweze kumkaa vizuri.
Ikiwa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa hakimkai vizuri mtumiaji, hakitaweza kufanya kifundo chake cha mguu na sehemu ya kutembelea ya mguu kuwa mahali pake.
Kazi
Mueleze mtumiaji mtarajiwa wa kiatu kigumu saidizi kwamba baadhi ya shughuli zinahitaji uangalizi wa ziada Wakati wa kuvaa kiatu kigumu saidizi.
- Mtumiaji wa kiatu kigumu saidizi anapaswa kutumia sehemu ya kushikilia Wakati wa kushuka kwenye ngazi
- mtu anaweza kuhitaji kifaa chwa kutembelea wakati anapopanda au kuteremka sehemu zenye miteremko mikAli
- mtu anaweza kuhitaji kiti cha bafuni wakati anapoenda kuoga kama hawezi kubeba uzito kwenye mguu/sehemu ya kutembelea ya mguu wake.
Baadhi ya shughuli haziwezekani kufanyika wakati mtumiaji wa kiatu kigumu saidizi bado amevaa hicho kiatu ni pamoja na:
- Kuendesha gari au pikipiki
- Kukimbia au kutembea kwa haraka
- Kuruka.
Utunzaji wa kiatu kigumu saidizi dhidi ya Maji.

Elezea:
viatu vigumu saidizi havipaswi kutumika kwenye sehemu ya Maji.
Kiatu kigumu saidizi kinaweza kutunzwa Wakati wa mtumiajimiaji kiatu anapooga kamad daktari ameshauri kutokuvua hicho kiatu.
Majadiliano
mtumiaji wa Kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa anapaswa kuendelea kukivaa, labda itokee kuwa daktari ameshauri kivuliwe wakati mtumiaji anapooga.
Mfuko wa plastiki uliowekwa juu ya kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa Unaweza kusaidia kuzuia Maji kuingia kwenye kiatu

Je, Unaweza kuFikiria njia nyingine zozote za kulinda kiatu saidizi kinachoweza kuvuliwa kama hakiwezi kuvuliwa pale mtumiaji anapotaka kuoga?
Swali

UnamKumbuka Josephina?
Josephina ni mvuvi na hutumia muda mwingi kwenye mashua yake na ufukweni. Alikuwa na jeraha la kwenye sehemu laini ya mguu wake na alihitaji kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa ili kumsaidia kupona.Josephina ana ugonjwa wa kisukari na unamweka katika hatari ya kupata vidonda vya mguu.
Je, ungeweza kumwambia Josephina kuhusu kutumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa karibu na Maji?
Chagua majibu sahihi tu.
Umepatia iwapo umechagua majibu sahihi kuwa ni "a" na "b"
Ni muhimu sana kuongea na Josephina juu ya hatari za kwenda ufukweni na kwenye Maji Wakati wa amevaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa. Mshauri Josephina kwamba hataweza kuendelea na shughuli zake za uvuvi, hadi hapo kidonda chake kitakapopona.
Josephina yuko katika hatari kubwa ya kupata kidonda cha mguuni. kama kiatu chake kigumu ambacho kinaweza kuvuliwa kitaingia Maji kwa ndani; jambo hili lInaweza kusababisha kidonda kwenye sehemu ya kutembelea ya mguu.
Ni muhimu pia kuelezea nini cha kufanya Ikiwa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kikiingia Maji.
c Sio sahihi.
Kiatu kigumu saidizi hakipaswi kutumika katika Maji.
Kutumia kiatu kigumu saidizi Wakati wa kulala
Elezea:
kama kiatu kigumu hakivuliwi Wakati wa kulala, jaribu kukizungushia kitambaa laini ili iwe rahisi kulala nacho.

UnamKumbuka Wei?
Wei anatumia foronya ya zamani kufungia kiatu chake ili ajisikie vizuri wakati anapolala. Hii inazuia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kisichubue mguu mwingine. Wei pia hulala na mto katikati ya magoti yake ili kujisikia vizuri wakati anapolala.
Kuzunguka kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa usalama

Elezea:
Kabla ya kuanza kutembea na kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa:
- angalia kiatu kigumu kimevaliwa vizuri inavyopaswa
- Daima vaa kiatu kizuri chenye soli pana kwenye mguu mwingine
- Waweza kuhisi kuwa Mguu wako wenye kiatu kigumu saidizi ni mrefu kuliko mguu usio kuwa na kiatu. Kiatu kinachofaa kitakusaidia kujisikia kuwa imara zaidi Wakati wa kutembea.
Ni muhimu kuwa salama Wakati wa kusimama, kukaa chini na kutembea na kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa . Inaweza kuwa salama kuwa na mtu wa kukusaidia unapotembea kwa mara ya kwanza.
Wakati wa kutumia kiatu kigumu kisaidizi kwa mara ya kwanza:
- Utahisi kuwa ni kizito
- Inaweza kuwa vigumu kusimama bila kutetereka
- Kifaa saidizi cha kutembea, kama kitahitajika kinapaswa kutumika huku ukiwa na Uwezo wa kusimama bila kutetereka.

Kutembea huku umebeba uzito kamili
Jaribu kutembea kama kawaida, huku ukiwa na uzito kamili kupitia viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa.
Tazama Video ili uone namna ya kutembea na uzito kamili kwenye kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa.
Kutembea ukiwa umebeba uzito kiasi
Tumia vifaa saidizi vya kutembelea, kwa kubeba uzito kupitia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa.
Tazama video hii ili uone namna ya kutumia viatu vigumu saidizi wakati umebeba uzito kiasi.
Kutembea bila ya kubeba uzito wowote
Tumia kifaa saidizi cha kutembelea bila ya kubeba uzito wowote ukiwa umevaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa
Tazama video hii ili uone namna ya kutumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa bila ya kubeba uzito wowote.
Swali
UnamKumbuka Jess?
Ungejadili nini na Jess wakati anaanza kutumia kiati kigumu chake kwa mara ya kwanza.
Chagua majibu sahihi tu.
Umepatia iwapo umechagua b, c na d.
Jess anapaswa kufanya mazoezi kwenye ardhi tambarare kwanza na kisha kufanya mazoezi nje na kwenye ardhi isiyo tambarare. Inaweza kuwa vigumu kwa watu wengine kutembea bila kutetereka Wakati wamevaa viatu Vigumu saidizi
a Sio sahihi.
Sio rahisi kila wakati kwa watu wote kutumia viatu vigumu saidizi
Soma Moduli ya vifaa saidizi vya kutembelea vya TAP ili viwe kama ukumbusho wa Uwezo wa kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kumsaidia mtu kwa kumpa vifaa saidizi vya kutembelea.
Ishara za hatari

Mwambie mhitaji kuwasiliana na wewe au daktari wake Ikiwa ataona dalili zozote za hatari.
Swali
Unaweza kumfundisha nini Jess kuhusu wakati gani wa kupata Msaada kutoka kwa daktari wake?
Chagua majibu sahihi tu.
majibu yote ni sahihi\.
Ikiwa Jess ana shida yoyote au anaona kitu chochote tofauti kuhusu hisia (hisia\) ana Wakati wa kutumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa,anaweza kuwasiliana na mtoa huduma ya afya wa kwake; kama ana dukuduku kuhusu kiatu kigumu chake au kuhusu jeraha lake