Ni kitu gani cha kufanya kama watu wanapata changamoto katika Kujitunza
Kuwasaidia watu kumudu Kujitunza vizuri zaidi kunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye ubora wa mAISHA ya mhusikamiaji. Kwa mfano, watu wanaweza:
- Kutumia muda kidogo kwenye Kujitunza
- Kuwa huru zaidi
- Kushiriki katika mAISHA ya shule, kazi na kwenye jamii.
Kila mara Kumbuka kujadiliana na watu kuhusu namna ambayo wanaweza Kujitunza. Kwa pamoja mnaweza kutafuta ufumbuzi ambao unaweza kubadilisha mAISHA ya mhusikamiaji!
Mtu mwenyepata taabu kwenye Kujitunza anaweza kufaidika na baadhi ya vifaa saidizi vilivyoelezewa katika moduli hii.
Kila mara Kumbuka kufuata hatua Nne (kuchagua, kupata kipimo sahihi, kutumia, kufanya ufuatiliaji) katika kugawa vifaa saidizi.
taarifa zaidi katika kuhusu vifaa saidizi vya Kujitunza na namna ya kufuata harua Nne, kwa pamoja vimezungumziwa kwenye moduli za bidhaa za TAP
kuhusu bidhaa nyingine, angalia kama kuna huduma katika eneo lako; ambalo waweza kumpa mgonjwa rufaa aende kupata bidhaa hizo.
Ili kuifanya huduma ya Kujitunza iwe rahisi, vifaa saidizi vinaweza kuwa sehemu ya suluhisho la tatizo lao\.
Swali
angalia hapa chini ili kujua njia mbalimbali ambazo zinaweza kufanya Kujitunza kuwa rahisi.
Njia zote Tatu hapo juu zinaweza kuhitajika ili Kujitunza kuweze kufanyika kwa urahisi.
Kulingana na jukumu lako na huduma unayotoa, unaweza kusaidia watu kuzoea mazingira yao au kubadilisha namna Kujitunza kunavyofanyika
Unaweza pia kutoa rufaa wahitaji kwenda kwenye huduma nyingine, kama vile huduma ya utengamo, ili waweze kupata Msaada zaidi.
Majadiliano
Kuna rasilimali au huduma gani katika eneo lako ambazo zinaweza :
- Kutoa vifaa saidizi ambavyo havipo chini ya TAP (kwa mfano mito ya kupunguza mgandamizo na magodoro, vifaa vya kulia chakula vilivyoboreshwa\)?
- Kusaidia wahitaji kuzoea mazingira yao ya nyumbani (kwa mfano kuweka kifaa kinachosaidia kupanda ngazi, kuongeza vyuma vya kushikiria, upatikanaji wa Maji na maeneo ya kuoga kufikika kwa urahisi zaidi)?
- Kuwasaidia watu kujifunza njia tofauti za Kujitunza?
Sasa umekamilisha Somo la Tatu!
Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.