Vifaa saidizi vya Kujitunza ambavyo havijajumuishwa kwenye TAP 

Maendeleo ya usoMaji Mada:

Baadhi ya vifaa saidizi vya Kujitunza havikuzungumziwa kwenye moduli za vifaa saidizi za TAP.
Hii ni kwa sababu wanahitaji mafunzo zaidi ili waweze kuvigawa

Endelea kusoma ili kujifunza kuhusu mfano mmojawapo wa aina za vifaa saidizi vya Kujitunza.

Vifaa saidizi vya Kujitunza vinasaidia kuzuia vidonda mgandamizo

Kidonda mgandamizo ni kuharibika kwa ngozi kwa kukatikakatika kunakosababishwa na mgandamizo. Kwa kawaida hii hutokea sehemu ya juu ya mfupa; na ni tatizo ambalo linawaathiri sana watu ambao hawana hisia au wale wanaopata taabu kusogea kutoka eneo moja hadi jingine; ili kubadilisha namna wAlivyokaa/ wAlivyolala.

Majeraha ya mgandamizo ni tatizo linalotekea Mara kwa mara kwa watu ambao Uwezo wao wa kuhisi umepungua au kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na ambao hutumia Kiti saidizi cha magurudumu au kulala kwa Muda mrefu.

Vifaa tofauti vya Kujitunza vinaweza kutumika kuzuia vidonda vitokanavyo na mgandamizo

Watu wanaotumia viti saidizi vya magurudumu na wako katika hatari ya kupata kidonda mgandamizo wanapaswa kutumia mto wa kupunguza mgandamizo wanapotumia viti saidizi vya magurudumu walivyoshauriwa na daktari.

Kiti saidizi cha magurudumu chenye kigodoro kinene kilichopachikwa ili kufanya mgandamizo unaotokana na mkaaji uwe sawa kwenye kiti.

Watu ambao wako katika hatari ya kupata vidonda vya mgandamizo wanapaswa pia kutumia godoro ili liwapunguzie mgandamizo Wakati wanapokuwa wamelala kwenye kitanda chao.

Godoro nene lenye safu ya ziada kwa juu. Kitambaa kimefunika  nusu ya godoro.

Kidonda kitokanacho na mgandamizo ambacho hakiponi ni hatari kubwa ya kiafya. Kukitibu mapema inavyowezekana ni muhimu ili kuzuia kidonda hiki kuzidi kuwa katika hAli

Mtu yeyote mwenye kidonda kinachotokana na mgandamizo anapaswa kupata matibabu.

Kwa habari zaidi kuhusu majeraha ya shinikizo, angalia moduli ya bidhaa za msaada wa TAP Mobility.

Umekamilisha Somo la Pili!

Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.

Jukwaa la majadiliano